settings icon
share icon
Swali

Bibilia inasema nini kuhusu kuwa mzazi mwema?

Jibu


Uzazi waweza kuwa ugumu na wa changa moto, lakini kwa wakati huo huo unaweza kuwa wa tuzo na jukumu la kutimiza ambalo tutakuwa tukilifanya. Bibilia iko na mengi ya kusema kuhusu njia tunayoweza kuwalea watoto wetu wawe wanaume na wanawake wa Mungu. Kitu cha kwanza tunastahili kufanya ni kuwafunza ukweli kuhusu neno la Mungu.

Pamoja na kumpenda Mungu na kuwa mfano mwema kwa kujitoa sisi wenyewe kwa amri zake, tunastahili kuzitii amri za Kumbukumbu 6:7-9 kuhusu kuwafunza watoto wetu kufanya hivyo. Ufahamu huu unasisitiza jambo linaloendelea wa maelekezo hayo. Lazima lifanywe kila wakati, tukiwa nyumbani, njiani, usiku na hata asubuhi. Ukweli wa Bibiia lazima uwe wa msingi wa jamii zetu. Kwa kufuata kanuni ya amri hizi, tunawafunza watoto wetu kuwa kumwabudu Mungu lazima kuendelee, sio kuwekewa jumapili asubuhi au usiku wa maombi.

Ingawa watoto wetu wanajifunza mambo mengi kupitia mafunzo ya moja kwa moja, wanajifunza mengi sana kupitia kututizama. Hii ndio sababu tunastahili kuwa waangalifu kwa kila jambo tunalolifanya. Kwanza lazima tutambue majukumu yetu tumepewa na Mungu. Mume na mke kwa ukomavu wanastahili kuwa wa heshima na kunyenyekea kwa wao wenyewe (Waefeso 5:21). Kwa wakati huo huo, Mungu ameanzisha mkondo wa uongozi ambao unafuatwa. “Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu” (1 Wakorintho 11:3). Tunajua kuwa Kristo si duni mbele za Mungu, kama vile mwanamke si duni kwa mume wake. Mungu anatambua, ingawa bila kunyenyekea kwa mamlaka yake, hamna mtindo. Jukumu la mwanamume kama kichwa cha nyumba ni kumpenda mke wake vile anavyoupenda mwili wake, kwa jitiada zile Kristo alizipenda Kanisa nazo (Waefeso 5:25-29).

Kuambatana na huu uongozi wa upendo, si kitu kigumu kwa mwanamke kunyenyekea kwa uongozi wa mume wake (Waefeso 5:24; Wakolosai 3:18). Jukumu lake la kwanza kabisa ni kumpenda na kumweshimu mume wake, kukaa kwa maarifa na utakatifu na kutunza boma (Tito 2:4-5). Wanawake kwa maumbile jukumu lao ni kutunza kuliko wanaume kwa sababu wamepangiwa kuwa walinzi wa watoto wao.

Nidhamu na maonyo ndio kitu cha muimu katika uzazi. Methali 13:24 yasema, “Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema.” Watoto wanao kua kwa boma isiyowarudi wanajihisi kuwa hawatakikani na si wa maana. Wanokosa mwelekeo na kujizuia, na wanapokuwa wakubwa wanaasi na hawana/wako na heshima kidogo sana kwa uongozi wowote ule, ukiwemo ule wa Mungu. “Murudi mwanao, kwa maana liko tumaini; Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake” (Methali 19:18). Kwa wakati huo huo, nidhamu lazima iwe sawa na upendo, au watoto wakue na; chuki, wasio na tumaini, na wa kuasi (Wakolosai 3:21). Mungu anatambua kuwa nidhamu ni chungu wakati inapeanwa (Waebrania 12:11), lakini ikifuatwa kwa maonyo ya upendo, hakika ni ya manufaa kwa mtoto. “Nanyi , akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana” (Waefeso 6:4).

Ni vizuri kuwahuzisha watoto katika kanisa ya nyumbani na huduma bado wakiwa wadogo. Kila mara kuenda katika Kanisa linalo amani Bibilia (Waebrania 10:25), inawawezesha kukuona ukilisoma neno la Mungu, na pia kujifunza nao. Jadiliana nao ulimwengu unaowazunguka vile wanavyouona, na wafunze kuhusu utukufu wa Mungu kila siku. “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee” (Methali 22:6). Kuwa mzazi mwema wahusika na kuwalea watoto ambao wataufuata mfano wako katika kumtii na kumwabudu Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Bibilia inasema nini kuhusu kuwa mzazi mwema?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries