settings icon
share icon
Swali

Je, kutakuwa na nafasi ya pili ya wokovu baada ya Unyakuo?

Jibu


Watafsiri wengine wa Biblia wanaamini kuwa hakutakuwa na nafasi kabisa ya wokovu baada ya Unyakuo. Ingawa, hakuna mahali katika Biblia ambayo inasema haya au hata inaonyesha dalili ya dhana hii. Kutakuwa na watu wengi wanaokuja kwa Kristo wakati wa dhiki. Ishara 144,000 ya Wayahudi (Ufunuo 7: 4) ni waumini wa Kiyahudi. Ikiwa hakuna mtu anaweza kuja kwa Kristo wakati wa dhiki, basi kwa nini watu wanatezwa kwa sababu ya imani yao (Ufunuo 20: 4)? Hakuna kifungu cha Maandiko kinachosema kinyume kwa watu kuwa na nafasi ya kuokolewa baada ya Unyakuo. Vifungu vingi vinaonyesha kinyume.

Mtazamo mwingine ni kwamba wale wanaoisikia injili na kuikataa kabla ya Unyakuo hawawezi kuokolewa. Wale waliokolewa wakati wa dhiki, basi, ni wale ambao hawakuwahi kusikia Injili kabla ya Unyakuo. "Nakala ya ushahidi" kwa mtazamo huu ni 2 Wathesalonike 2: 9-11, ambayo inasema Mpinga Kristo atafanya miujiza kudanganya "wale wanaoangamia" na kwamba Mungu Mwenyewe atawatuma "udanganyifu wenye nguvu" ili kuwahakikishia kwa kutoamini. Sababu iliyotolewa ni kwamba "hawakuupokea na kuupenda ule ukweli ili waokolewe" (mstari wa 10). Kwa hakika, wale walio na moyo mgumu kwa Injili kabla ya Unyakuo kuna uwezekano wao kubaki hivyo. Na Mpinga Kristo atadanganya wengi (Mathayo 24: 5). Lakini "wale waaokataa kupenda kweli" hii haswa haiashirii wale watu walioisikia Injili kabla ya Unyakuo. Anaweza kuwa mtu yeyote ambaye anakataa kabisa wokovu wa Mungu, wakati wowote. Kwa hiyo, hakuna ushahidi wa wazi wa maandiko wa kuunga mkono mtazamo huu.

Ufunuo 6: 9-11 inazungumzia wale waliouawa wakati wa mateso "kwa sababu ya neno la Mungu, na kwa sababu ya ushuhuda waliyokuwa waliotoa." Wafuasi hawa wataelezea kwa usahihi yale wanayoyaona wakati wa dhiki na wataamini injili wenyewe na Wito wengine wapate kutubu na kuamini pia. Mpinga Kristo na wafuasi wake hawatashikilia uinjilisti wao na watawaua. Wafuasi wote hawa ni watu ambao walikuwa hai kabla ya Unyakuo, lakini ambao hawakuwa waumini hadi baadaye. Kwa hivyo, kutakuwa fursa ya kuokelwa kwa Kristo kwa imani baada ya Unyakuo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kutakuwa na nafasi ya pili ya wokovu baada ya Unyakuo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries