settings icon
share icon
Swali

Je! Nambari saba/7 ina umuhimu gani wa kibiblia?

Jibu


Katika Biblia nzima, Mungu mara nyingi hutoa umuhimu wa mfano kwa vitu au dhana za kawaida. Kwa mfano, katika Mwanzo 9: 12-16, Mungu anaufanya upindi wa mvua kuwa ishara ya ahadi Yake kwa Nuhu (na, kwa kujumuisha wanadamu wote) kwamba hataigharisha dunia yote tena. Mungu hutumia mkate kama kielelezo cha uwepo wake na watu wake (Hesabu 4: 7); ya karama ya uzima wa milele (Yohana 6:35); na mwili wa Kristo uliobondwa, uliotolewa dhabihu kwa ajili ya dhambi zetu (Mathayo 26:26). Upindi wa mvua na mkate ni ishara dhahiri katika Maandiko. Maana zisizo dhahiri zinaonekana kuhusishwa na nambari zingine katika Biblia, haswa nambari 7, ambayo wakati mwingine hutoa msisitizo maalum katika andiko.

Matumizi ya kwanza ya nambari 7 katika Biblia inahusiana na juma la uumbaji katika Mwanzo 1. Mungu alichukua siku sita katika kuumba mbingu na nchi, na akapumzika siku ya saba. Hii ndio kielezo chetu cha juma la siku saba, ambayo inazingatiwa kote ulimwenguni hadi leo hii. Siku ya saba ilipaswa "kutengwa" kwa Waisraeli; Sabato ilikuwa siku takatifu ya kupumzika (Kumbukumbu 5:12).

Kwa hivyo, mwanzoni mwa Biblia, nambari ya 7 inatambulika na kitu "kilimilika" au "kilichokamilika." Kuanzia hapo, ushirika huo unaendelea, kwa kuwa nambari 7 hupatikana mara nyingi katika muktadha unaojumuisha ukamilifu au ukamilifu wa kiungu. Kwa hivyo tunaona amri ya kuwa Wanyama wanapaswa kuwa na angalau siku saba kabla ya kutumiwa kwa dhabihu (Kutoka 22:30), amri ya Naamani mwenye ukoma kuoga katika Mto Yorodani mara saba ili kukamilisha utakaso kamili (2 Wafalme 5:10) , na amri kwa Yoshua kuzunguka Yeriko kwa siku saba (na siku ya saba kutengeneza mizunguko saba) na makuhani saba kupiga tarumbeta saba nje ya kuta za mji (Yoshua 6: 3-4). Katika visa hivi, nambari 7 inaashiria kukamilika kwa aina fulani: agizo la kiungu linatimizwa.

Cha kufurahisha ni kuwa, mwanadamu aliumbwa siku ya sita ya uumbaji. Katika vifungu vingine vya Biblia, nambari 6 inahusishwa na wanadamu. Katika Ufunuo "nambari ya mnyama" inaitwa "nambari ya mwanadamu. Nambari hiyo ni 666" (Ufunuo 13:18). Ikiwa nambari ya Mungu ni 7, basi ya mwanadamu ni nambari 6. Sita kila wakati huwa imepungukiwa na alama moja kutoka kwa saba, kama vile "kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu" (Warumi 3:23). Mwanadamu sio Mungu, vile nambari 6 sio nambari 7.

Mfululizo wa mambo saba hutokea mara nyingi katika Biblia. Kwa mfano, tunapata jozi saba za kila mnyama asiye na mawaa kwenye safina (Mwanzo 7:2); shina saba juu ya kinara cha taa cha hema (Kutoka 25:37); sifa saba za Masihi katika Isaya 11:2; ishara saba katika Injili ya Yohana; mambo saba ambayo Bwana huyachukia katika Mithali 6:16; mifano saba katika Mathayo 13; na ole saba katika Mathayo 23.

Ongezeko la 7 pia huonekana katika simulizi ya kibiblia: unabii wa "majuma sabini" katika Danieli 9:24 unahusu miaka 490 (7 mara 7 mara au 10/7x7x10). Yeremia 29:10 alitabiri Utumwa wa Babeli ungedumu kwa miaka sabini (7 mara 10). Kulingana na Mambo ya Walawi 25:8, Mwaka wa Yubile ulipaswa kuanza baada ya kutimia mwaka wa arobaini na tisa (mara 7 mara 7).

Wakati mwingine, ishara ya 7 ni faraja kubwa kwetu: Yesu ndiye "mimi ndimi" mara saba katika Injili ya Yohana. Wakati mwingine, inatupa changamoto: Yesu alimwambia Petro asamehe atakayemkosea "mara sabini mara saba" (Mathayo 18:22). Pia kuna vifungu ambavyo nambari 7 inahusishwa na hukumu ya Mungu: bakuli saba za Dhiki Kuu, kwa mfano (Ufunuo 16:1), au onyo la Mungu kwa Israeli katika Walawi 26:18.

Kuzungumzia juu ya kitabu cha Ufunuo, nambari 7 inatumiwa pale zaidi ya mara hamsini katika muktadha anuwai: kuna barua saba kwa makanisa saba huko Asia na roho saba mbele ya kiti cha enzi cha Mungu (Ufunuo 1:4), vinara vya taa saba vya dhahabu (Ufunuo. 1:12), nyota saba katika mkono wa kulia wa Kristo (Ufunuo 1:16), mihuri saba ya hukumu ya Mungu (Ufunuo 5:1), malaika saba wenye tarumbeta saba (Ufunuo 8:2), n.k kwa njia zote sawia, idadi 7 tena inawakilisha ukamilifu au ujumla: makanisa saba yanawakilisha ukamilifu wa mwili wa Kristo, mihuri saba kwenye kitabu inawakilisha ukamilifu wa adhabu ya Mungu juu ya dunia yenye dhambi, na kadhalika. Na, kwa kweli, kitabu cha Ufunuo chenyewe, pamoja na hesabu yake yote ya nambari 7, ni jiwe kuu la Neno la Mungu kwa mwanadamu. Pamoja na kitabu cha Ufunuo, Neno lilikamilika (Ufunuo 22:18).

Kwa jumla, nambari 7 imetumiwa katika Biblia zaidi ya mara mia saba. Ikiwa pia tutajumuisha maneno yanayohusiana na saba (maneno kama mara saba au sabini au mia saba), hesabu itakuwa kubwa zaidi. Kwa kweli, sio kila tukio la nambari 7 katika Biblia linabeba umuhimu mkubwa. Wakati mwingine, nambari7 ni nambari 7 tu ya kawaida, na lazima tuwe waangalifu katika kuambatanisha maana za mifano kwa maandishi yoyote, haswa wakati Maandiko hayaelezei wazi juu ya maana kama hizo. Walakini, kuna wakati inaonekana kwamba Mungu anawasilisha wazo la ukamilifu wa kiungu, ukamilifu, na umoja kupitia nambari 7.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Nambari saba/7 ina umuhimu gani wa kibiblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries