settings icon
share icon
Swali

Biblia inasemaje juu ya ndoa ya watu wa asili tofauti?

Jibu


Sheria ya Agano la kale iliwaamuru waIsraeli wasioe watu wa mataifa mengine (kumbukumbu la torati 7:3-4). Sababu ya haya ni kwambawangeoa mataifa mengine wangepotoshwa na kumgeuka Mungu wao kiasi cha kuabudu miungu ya uongo/sanamu. Kanuni kama hiyo insisitizwa katika agano jipya: “msifungwe nira na wasioamini. Kwani kuna ushirika gani baina ya nuru na giza?” wakorintho wa pili 6:14). Kama waisraeli (wanaomini Mungu mmoja wa kweli) waliamuriwa kutooa watu wa mataifa mengine ysiyoamini, vivyo hivyo wakristo wanaamuriwa wasioe wasioamini. Kwa kujibu swali lenyewe nikwamba biblia haikatazi ndoa ya watu wa asili tofauti.

Mtu ni ahukumiwe kutokana na tabia zake binafsi wala sio rangi. Sote natujihadhari tusije tukaonyesha ubaguzi wa rangi kwa wengine (yakobo 2: 1-10, tazama aya ya 1 na 9). Mkristo anapotaka kuoa ama kuolewa ni vyema kwanza akitafuta kujua kama anayetaka kushikana naye ni mkristo pia. (wakorintho wa pili 6:14), aliyezaliwa mara ya pili kwa imani ndani ya Yesu kristo (Yohana 3:3-5). Imani katika kristo wala sio rangi ya ngozi ndiyo kigezo cha biblia cha kuchagulia mchumba. Ndoa za watu wa asili tofauti ni za kutumia hekima, kutambua na maombi.

Jambo linalofanya ndoa za watu wa asili tofauti kuwa za uangalifu ni kwa sababu ya ugumu watakao upata katika hali ya kuchaganya mila hizo mbili, Ubaguzi na kejeli kutoka kwa watu wa jamii pia. Wengine huzaa watoto wenye shida za rangi katika ngozi. haya ni baadhi ya mambo ambayo wanaooana sharti wajiandae nayo kabla kushikamana katika tofauti zao za asili ama rangi. Biblia inakaza tu ndoa ya muumini na asiyeamini.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasemaje juu ya ndoa ya watu wa asili tofauti?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries