Swali
Je, ndoa huzuia uhusiano wako na Mungu?
Jibu
Suala kwamba ndoa inaweza kuzuia huduma ya mtu kwa Mungu lilikuwa la wasiwasi kwa Paulo katika 1 Wakorintho 7. Kwa sababu hii, alisema kuwa ni vyema kwa mtu kubaki mtawa vile yeye alikuwa. Lakini alielewa kwamba uwezo wa kubambana na maisha ya utawa bila "kusumbuliwa" na hisia sio kibali kilichozawadiwa kila mtu (mistari 7-9). Anasema katika mstari wa 32-35 kwamba watu wasioolewa wanaweza kumtumikia Bwana katika "fikra" isiyosaidiwa kwa sababu hawana haja ya kuzingatia sehemu ya maisha yao kwa kuwapendeza wapenzi wao. Lakini pia alisema kuwa, ikiwa sisi ni wana ndoa au la, tunapaswa kuzingatia kumtumikia Kristo (mistari 28-31).
Lakini ukweli kwamba Yesu hakuwaita watawa tu — na hata kumchagulia Petro, mtu aliyeoa (Mathayo 8:14), kama mwendani wa karibu kati ya wanafunzi — inaonyesha kuwa ndoa haipaswi kuzuia urafiki wa mtu na Kristo. Vivyo hivyo, katika Agano la Kale kuna watu wawili (kati ya wengine) ambao walikuwa karibu na Mungu. Mmoja alikuwa Danieli; mwingine alikuwa Musa. Mmoja hakuwa ameoa; na mwingine alikuwa ameoa. Kwa hiyo, ndoa haikuwa sababu katika kuamua urafiki na Mungu.
Kitu muhimu cha ndoa kuwa haiaribu urafiki wa mtu na Kristo ni kuhakikisha kuolewa "kwa Bwana" (1 Wakorintho 7:39) au, kwa kuiweka katika njia nyingine, kutoshikanishwa na jukumu la kutofautiana (2 Wakorintho 6:14) kwa kuolewa ama asiyeamini au muumini ambaye hana msingi sawa wa mafundisho au tamaa moja ya kumtumikia Kristo kwa moyo wake wote. Ikiwa mtu anaoa "katika Bwana," Maandiko huahidi faida za urafiki mzuri (Mithali 27:17; Mhubiri 4: 9-12), na mwenzi huwa msaada na faraja katika kutembea na Kristo.
English
Je, ndoa huzuia uhusiano wako na Mungu?