settings icon
share icon
Swali

Ni mara ngapi wanandoa wanapaswa kufanya ngono?

Jibu


Biblia haituambii ni mara ngapi wanandoa wanapaswa kufanya ngono, lakini inatuambia kwamba wanandoa wanapaswa kujizuia tu wakati uamuzi wao ni wa pamoja. Wakorintho wa Kwanza 7: 5 inatuambia, "Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu." Kwa hivyo, kuwa na kiasi ni "sheria" ya ni mara ngapi wanandoa watakuwa na ngono. Sheria ni kuwa kujisuia lazima kuwe kwa makubaliano, na kwamba hata wakati umekubaliana, ni lazima tu kuwe kwa muda mfupi.

Ngono haipaswi kuzuiwa au kulazimishwa. Ikiwa mwanandoa mmoja hataki kufanya ngono, mwenzi mwingine anapaswa kukubaliana naye. Ikiwa mwanandoa mmoja anataka kufanya ngono, mwenzi mwingine anapaswa kukubaliana. Yote ni jambo la maelewano. Lazima tukumbuke kwamba miili yetu ni ya washirika wetu, kama 1 Wakorintho 7: 4 inatuambia, "Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe." Kwa wazi, "maelewano ya ngono" katika ndoa lazima yawe ya busara. Ikiwa mwenzi mmoja anatamani ngono kila siku, na mwenzi mwingine mara moja kwa mwezi au chini, wanapaswa kwa upendo na dhabihu kukubaliana. Uchunguzi unaonyesha kwamba kuzingatia kila umri wa miaka, wanandoa wa kawaida wanajamiiana mara 2 kwa juma.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni mara ngapi wanandoa wanapaswa kufanya ngono?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries