Swali
Nini maana ya nguo ya magunia na majivu?
Jibu
Nguo ya magunia na majivu yalitumiwa katika nyakati za Agano la Kale kama ishara ya kushusha hadhi, maombolezo, na / au toba. Mtu anayetaka kuonyesha moyo wake wa kutubu mara nyingi huvaa nguo ya magunia, kukaa katika majivu, na kuweka majivu juu ya kichwa chake. Nguo ya magunia ilikuwa nyenzo isiyo laini ambayo kawaida hutengenezwa kwa nywele nyeusi za mbuzi, na kuifanya isio na raha kabisa kuivaa. Majivu yalionyesha majonzi na maangamizi.
Mtu alipopokufa, tendo la kuvaa nguo ya magunia lilionyesha huzuni kubwa kwa kupoteza mtu huyo. Tunaona mfano wa hili wakati Daudi aliomboleza kifo cha Abneri, jemadari wa jeshi la Sauli (2 Samweli 3:31). Yakobo pia alionyesha huzuni yake kwa kuvaa nguo ya magunia wakati alidhani mwanawe, Yusufu, alikuwa ameuawa (Mwanzo 37:34). Matukio haya ya maombolezo kwa wafu hutaja nguo za magunia lakini si majivu.
Mjivu yaliambatana na nguo ya magunia katika nyakati wa msiba wa kitaifa au kutubu kutoka kwa dhambi. Esta 4:1, kwa mfano, inaelezea Mordekai akirarua nguo zake, akivaa nguo ya magunia na majivu, na kuingia mjini "akilia kwa sauti kubwa na kwa uchungu." Hili ndio lilikuwa jibu la Mordekai kwa tangazo la Mfalme Ahasuero kutoa mamlaka kwa Hamani dhaifu kuharibu Wayahudi (tazama Esta 3:8-15). Mordekai sio peke yake ambaye aliomboleza. "Na katika kila jimbo, ambako amri ya mfalme na mbiu yake imewasili, palikuwako msiba mkuu kwa Wayahudi, na kufunga, na kulia, na kuomboleza; hata na wengi wakalala juu ya gunia na majivu "(Esta 4:3). Wayahudi wakajibu habari haribifu kuhusu mbio zao na nguo ya magunia na majivu, kuonyesha huzuni kali sana na dhiki.
Nguo ya magunia na majivu pia hutumika kama ishara ya umma ya toba na unyenyekevu mbele ya Mungu. Wakati Yona aliwaambia watu wa Ninawi kwamba Mungu angeenda kuwaangamiza kwa sababu ya uovu wao, kila mtu kutoka kwa mfalme hadi kwa raia wa chini kabisa alijibu kwa toba, kufunga, na nguo ya magunia na majivu (Yona 3:5-7). Waliweka nguo ya magunia hata kwenye wanyama wao (mstari wa 8). Mawazo yao yalikuwa, "Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe?"(mstari wa 9). Hii ni ya kushangaza kwa sababu Biblia haisemi kamwe kwamba ujumbe wa Yona unahusisha kutaja kwokwote kwa huruma ya Mungu; lakini rehema ndio waliyopokea. Ni wazi kwamba uvaaji wa nguo ya magunia na majivu kwa watu wa Ninawi haikuwa maonyesho yasio na maana. Mungu aliona mabadiliko ya kweli-mabadiliko ya unyenyekevu ya moyo yaliyowakilishwa na nguo ya magunia na majivu-na ilisababisha Yeye "kuacha" na kutoleta mpango Wake wa kuwaangamiza (Yona 3:10).
Watu wengine Biblia inataja walivaa nguo ya magunia ni pamoja na Mfalme Hezekia (Isaya 37:1), Eliakimu (2 Wafalme 19:2), Mfalme Ahabu (1 Wafalme 21:27), wazee wa Yerusalemu (Maombolezo 2:10), Danieli (Danieli 9:3), na mashahidi wawili katika Ufunuo 11:3.
Kwa urahisi sana, nguo ya magunia na majivu yalitumiwa kama ishara ya nje ya hali ya ndani ya mtu. Ishara kama hiyo ilifanya mabadiliko ya moyo wa mtu kuonekana na kuonyesha uaminifu wa huzuni na/au toba. Haikuwa tendo la kuvaa nguo ya magunia na majivu yenyewe ambayo yalimshawishi Mungu kuingilia kati, lakini unyenyekevu kwamba hatua kama hiyo imeonyeshwa (angalia 1 Samweli 16:7). Msamaha wa Mungu kwa mjibu wa toba ya kweli husherehekewa na maneno ya Daudi: "Ulinivua nguo ya magunia, ukanivika furaha" (Zaburi 30:11).
English
Nini maana ya nguo ya magunia na majivu?