Swali
Je! Kuna nguvu yoyote katika fikira ya kujenga?
Jibu
Ufafanusi moja wa fikira ya kujenga ni "tendo la kuchunguza njia za mawazo ili kutambua maeneo ambayo yanahitaji kuboreshwa, na kisha kutumia zana zinazofaa kubadilisha mawazo hayo kwa njia ya kujenga, yenye lengo." Bila shaka, kufikiria kwa kujenga sio vibaya. Tatizo inayohusishwa na "fikira ya kujenga" ni kuamini kuwa kuna aina fulani ya nguvu isiyo ya kawaida katika fikira za kujenga. Katika kipindi hiki cha mafundisho ya uongo yaliyoenea na kufanya hafifu teolojia, nguvu za fikira za kujenga imesimama kuwa moja ya makosa maarufu zaidi. Mafundisho ya uwongo yanafanana kwa kuwa ni mawazo ya kibinadamu yanayojifanya kama ukweli. Dhana moja ya kibinadamu ni nguvu ya fikira ya kujenga.
Dhana ya nguvu ya fikira ya kujenga ilienezwa na Dk Norman Vincent Peale katika kitabu chake cha Nguvu ya Fikira ya Kujenga (1952). Kulingana na Peale, watu wanaweza kubadilisha matokeo ya baadaye na matukio kwa "kuyafikiria" kuwepo. Nguvu ya fikira ya kujenga inakuza kujiamini na imani kwa nafsi; inaongoza kwa kawaida kwa imani ya uongo katika "sheria ya mvuto," vile Peale alivyoandika, "wakati unatarajia bora, unaajilia nguvu sumaku katika akili yako ambayo kwa sheria ya mvuto inaonekana kukuleta bora kwako." Bila shaka, hakuna chochote kibiblia juu ya akili ya mtu kuanzia "nguvu sumaku" inayovuta vitu vyema katika mzunguko wa mtu. Kwa kweli, kuna mengi yasiyo ya kibiblia kuhusu wazo kama hilo.
Katika Nguvu ya Fikira ya Kujenga, Peale alitumia dhana za kidini zilizo dosari na nadharia za kisaikolojia za kukubaliana ili kuendeleza toleo la uwongo la imani na matumaini. Nadharia yake ni sehemu ya harakati ya "kujisaidia mwenyewe" ambapo mtu anajaribu kuunda uhalisi wake mwenyewe kwa jitihada za kibinadamu, picha nzuri ya akili, na nguvu ya hiari. Lakini uhalisi ni ukweli, na ukweli hupatikana katika Biblia. Watu hawawezi kuunda ukweli wao wenyewe kwa kuiwaza au kuifikiria kuwapo. Nadharia ya Peale ni kosa kwa sababu hakuiweka juu ya ukweli.
Wafuasi wa nguvu ya fikira ya kujenga wanadai utafiti wao unasaidia uhalali wa nadharia. Hata hivyo, mwili wa data unajadiliwa kwa upana. Baadhi ya matokeo hayo yanapendekeza kuwa kuna uwiano mzuri kati ya mtazamo na utendaji mzuri, lakini hii ni kilio cha mbali kutoka kwa mawazo ya kujenga kuunda matokeo. Utafiti unapendekeza kuwa watu wenye mtazamo mzuri wanaonekana kujitukuza kwa juu na uzoefu bora ikilinganishwa na watu ambao wana mtazamo wa bila rajua. Kwa upande mwingine, hakuna ushahidi wa kuthibitisha kuunga mkono wazo kwamba mawazo yanaweza kudhibiti matokeo. Fikira ya kujenga haina nguvu ya asili ya kubadili wakati ujao.
Kila kipawa kizuri ni kutoka kwa Mungu juu (Yakobo 1:17), sio kutokana na nguvu ya fikira ya kujenga. Kipawa bora ya zote ni Roho Mtakatifu aliyekaa ndani (Luka 11:13). Biblia inasema kwamba mtu hawezi kuwa "mwema" kwake mwenyewe (Isaya 64:6). Nzuri tu ndani yetu hutoka kwa haki ya Yesu Kristo iliyotumika kwa akaunti yetu (Waefeso 2:1-5; Wafilipi 3:9). Mara tu Roho Mtakatifu anaishi ndani yetu, anaanza mchakato wa utakaso, ambapo nguvu ya kubadilisha ya Roho Mtakatifu inatufanya zaidi kama Yesu.
Ikiwa tunataka kujiboresha wenyewe na kufanya mabadiliko mazuri, tunahitaji kuwa zaidi ya nguvu ya fikira ya kujenga. Ukweli wa kiroho utaanza kila wakati na kutamatika na husiano wetu kwa Kristo. Ni Roho Mtakatifu ambaye ni ufunguo wa kubadilisha maisha ya mtu, si mawazo yetu, na si juhudi zetu pekee. Tunapojitolea kikamilifu kwa Roho, atatubadilisha. Badala ya kutafuta msaada kutoka kwa maono bwabwaja, vitabu vya kidini bandia, au nguvu ya kujitegemea ya fikira ya kujenga, tunapaswa kutegemea kile ambacho Mungu ameshatupa tayari kupitia Roho Wake: "Tuna akili ya Kristo" (1 Wakorintho 2:16).
English
Je! Kuna nguvu yoyote katika fikira ya kujenga?