settings icon
share icon
Swali

Kunayo nguvu katika jina la Yesu?

Jibu


Nguvu zozote zilizohuzishwa na jina la Yesu zinatoka na Utu wa Yesu. Wakati "tunaamini katika jina la Yesu," tunaamini katika kazi iliyokamilika msalabani ya Yesu aliyefufuka (1Yohana 5:13). Yesu sio jina la kimuijiza. Hakuna kitu cha maana katika mpangilio wa herufi kwa jina Lake. Yesu asingekuwa Mungu katika mwili ambaye aliishi maisha makamilifu, akafa kwa ajili ya dhambi za wote watakao mwamini, na kufufuka tena, hatungekuwa tunaongea kuhusu jina Lake. Nguvu zozote Wakristo wanapata kwa jina Lake zinatokana na imani ndani ya yule Yesu ni nani na chenye anafanya kwa niapa ya wenye dhambi.

Hakuna nguvu za kichawi katika jina la Yesu-kunazo nguvu moja tu katika Yesu Kristo pekee Yake. Kwa kuliita jina la "Yesu," tu mtu asitarajie nguvu maalumu, matokeo, au uhusiano mwema na Mungu. Jina la Yesu ni la thamani, ingawa, limejawa na maana. Tunaona dokezo la hili katika Mathayo 1:20-21 wakati malaika alimwambia Yusufu, "Yosefu, mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, maana amekuwa mjamzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. 21Atajifungua mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yesu, kwa kuwa yeye ndiye atakayewaokoa watu wake katika dhambi zao."

Nguvu ya Mungu iokayo, iponyayo, inayolinda, inatakza, na kukomboa inadumu ndani ya Utu wa Kristo na Yesu ndilo jina lake. Ni namna gani muumbaji wa ulimwengu, ajuaye mambo yote, ameenea pote, na mwenye enzi aliamua kuachilia nguvu zake? Kupitia Mwanawe aliyezaliwa katika hali nyenyekevu-mtoto aliye na nguvu zote za Mfalme (Luka 2:11-12). Yesu aliyatoa maisha yake ili kuokoa wenye dhambi, na akatumia nguvu zake kuyafufua tena (Yohana 10:18) ili kwamba yeyote aliitaye jina Lake kwa imani atapokea msamaha wa dhambi na wokovu wa milele yote (Warumi 10:13). Hiyo ndiyo nguvu ya ufufuo ya Mwokozi-Yeye pekee ndiyo shinizo nyuma ya jina Lake.

Ni kupitia jina la Yesu kwamba Mungu anatuamuru kuomba (Yohana 16:23-24). Waumini wamealikwa kuomba kwa jina la Yesu kwa matarajio kwamba Mungu atayajibu maombi (Yohana 14:13-14). Kuomba kwa jina la Yesu inamaanisha kuomba kwa uwezo wake (Luka 10:19) na kumuuliza Mungu Baba kutekeleza maombi yetu kwa sababu tumekuja kwa imani katika jina la Mwanawe Yesu. Kuomba kwa jina la Yesu inamaanisha kuomba kuomba sambamba na sifa za Yes una mapenzi Yake. Kuomba kwa jina la Yesu kunaonyesha Imani yetu kwa nguvu za Mungu kutenda wakati tunaamini kuwa jina la Yesu ni zaidi ya mkusanyiko wa kundi la herufi bali uwakilishi wa kile alicho.

Yesu lilikuwa jina la kawaida katika karne ya kwanza Israeli. Kitu pekee kinachotenga jina la Yesu wa Nazareti ni Mtu ambaye lilikuwa lake na chenye alitufanyia. Katika Kristo "Maana, ndani yake Kristo katika ubinadamu wake, umo ukamilifu wote wa Mungu" (Wakolosai 2:9). Yesu ndiye "Yeye ni mngao wa utukufu wa Mungu na mfano kamili wa hali ya Mungu mwenyewe" (Waebrania 1:3). Lakini mahali hamna imani, hamna uhusiano, au unyenyekevu kwa mamlaka yake, jina Yesu litakuwa tu neno.

Tunahekima ya kujilinda tokana na jaribio la kulitumia jina la Yesu vibaya. Bibilia inatuambi hadhiti ya kuvutia ya kikundi cha Wayahudi saba katika Efeso ambao walijaribu kuyakemea mapepo wakitumia jina la Yesu. Watu hawa hakumjua huyu Yesu. Hawakuwa wameokoka. Hawakuwa wamejitia chini ya Mungu na kwa hiyo wakakosa kumfanya pepo atoweke (Yakobo 4:7). Mara tu yule pepo aliwadhihaki wale saba waliojaribu kumpunga, ambao walijaribu kufanya masingaombwe wakitumia "Yesu" kama uganga bora: "Ninamfahamu Yesu, ninamjua pia Paulo, lakini nyinyi ni nani?" ule pepo mbaya akajibu. Ule pepo ukamtia nguvu yule mtu aliyemtawala akawapiga wale saba hadi wakatokwa damu na kuwaacha uchi (Matendo 19:13-16). Hawa watu saba walijaribu kulitumia vibaya nguvu katika jina la Yesu kwa manufaa yao wenyewe, lakini tunamtumikia Mungu ambaye hawezi kufanyishwa na kudanganywa (Ayubu 12:16).

Jina la Yesu, ambaye hukomboa watu Wake kutoka dhambini mwao, anaashiria nguvu zote za Muumba kwake mwenyewe. Yesu anawapa waumini mamlaka ya kutumikia, kufanya kazi, na kuomba kwa jina Lake wakati tunapofanya hivyo tukiamini katika nguvu za Yesu zinazookoa na kutamani mapenzi ya Mungu. Yesu kwa mamlaka ya Baba, alitumia nguvu hizo kuokoa wenye dhambi, na jina Lake pekee ndilo jina pekee tutakalo liita kwa wokovu (Matendo 4:12). Kama wana na binti walionyakuliwa kwa familia ya Mungu, Wakristo hupatana na neema ya Mungu inayookoa kupitia kwa imani katika Utu wa Yesu. Wakati tunaliita jina Lake, tunashikiriki katika nguvu Zake na kupata kwamba "Jina la Bwana ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama" (Methali 18:10).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kunayo nguvu katika jina la Yesu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries