settings icon
share icon
Swali

Nini maana ya mwenye dhambi?

Jibu


Kwa maana pana, mwenye dhambi ni mtu anayetenda dhambi (Luka 18:13). Neno la Kigiriki lililotafsiriwa “mwenye dhambi” katika Biblia lina maana ya mtu ambaye “amekosa alama,” kama vile mshale unaokosa shabaha yake.Kwa hiyo, mwenye dhambi amekosa alama ya Mungu na kwa kweli amekosa lengo zima la maisha yake.

Kawaida, tunamfikiria mwenye dhambi kama mtu ambaye hana maadili, mwovu, au mpotovu. Lakini Biblia inatuambia kwamba kila mtu ni mwenye dhambi: “Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu”(Warumi 3:23). Kupitia tendo la kwanza la kutotii la Adamu, wanadamu wote walirithi asili ya dhambi ( Warumi 5:12-14) na kuhesabiwa kuwa na hatia ya dhambi ya Adamu (Warumi 5:18). Yesu Kristo pekee ndiye hakuwa na dhambi: “Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake” (1 Petro 2:22).

Katika maneno ya theolojia, ni sahihi kuelewa neno ‘mwenye dhambi’ si kama jina la maadili au hukumu bali, kama neno la mahusiano. Kila mtu aliyetengwa na Mungu kupitia dhambi ni mwenye dhambi. Kuwa mwenye dhambi hufafanua hali iliyovunjika ya uhusiano wa mtu na Mungu. Wenye dhambi ni wale ambao wamevunja sheria ya Mungu (1 Yohana 3:4). Wenye dhambi ni watumwa wa dhambi (Yohana 8:34). Wanakabiliwa na hukumu ya Mungu (Yuda 1:14-15). Wako njiani kuelekea kifo na uharibifu (Ezekieli 18:20; Yakobo 1:5).

Pengo kati ya wenye dhambi na Mungu lingeweza kuunganishwa tu kupitia tendo la ukombozi wa Bwana-kwa Mungu mwenyewe kuja upande wa pengo la kibinadamu kupitia Yesu Kristo( ambaye ni “Mungu pamoja nasi”) na Roho Mtakatifu ambaye ,Yesu alimtuma mahali pake. Kwa upande wa mgawanyiko wa binadamu, watu wema, wenye fadhila zaidi ni wenye dhambi, na watu wabaya, waovu pia ni wenye dhambi. Wote ni wenye dhambi. Lakini Mungu anawapenda wenye dhambi na alimtuma Mwanawe afe kwa ajili yao (Warumi 5:8).

Wale wanaomwamini Yesu Kristo wamesamehewa dhambi zao na wamepewa uzima wa milele: “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye” (Yohana 3:16-17).

Biblia inawaonyesha wenye dhambi kwa hali mbalimbali na njia za kuwepo. Watu ambao hawaishi kulingana na sheria za Mungu wanachukuliwa kuwa wenye dhambi (Zaburi 1). Wale ambao hawakuwa waaminifu kwa agano la Israeli na Mungu na walifuata miungu mingine wanaelezewa kuwa wenye dhambi na manabii (Hosea 1-3).

Wayahudi wa kidini waliwachukulia Mataifa kuwa wenye dhambi (Wagalatia 2:15) na vilevile yeyote ambaye hakufuata mila na maagizo ya sherehe za Mafarisayo. Wakiukaji sheria wanatajwa kuwa wenye dhambi katika Biblia (1 Timotheo 1:9). Watu waliochafuliwa na uhalifu au maouvu fulani walionekana kuwa wenye dhambi (Luka 15:2; 18:13;19:7). Mwenye dhambi ni neno lililotumika kwa watu wasioamini (Mathayo 26:45), hasa wenye dhambi (Wagalatia 2:17), na wanawake waliokuwa na sifa mbaya (Luka 7:37)

Yesu alipoingia katika ubinadamu, Alipinga maoni yaliyotawala wakati wa siku Zake kuhusu wenye dhambi, hasa ya wasomi wa kidini. Yesu alitikisa hali ilivyo kwa kushiriki ushirika wa karibu na wenye dhambi: “ Basi watoza ushuru na wenye dhambi wote walikuwa wanakusanyika ili wapate kumsikiliza Yesu. Lakini Mafarisayo na walimu wa sheria wakanungʼunika wakisema, “Huyu mtu anawakaribisha wenye dhambi na kula nao” (Luka 15:1-2). Mafarisayo nao walimshtaki Yesu kuwa mwenye dhambi (Yohana 9:24).

Utume wa Kristo duniani, Utimilifu Wake wa kusudi la milele la Mungu, ulikuwa ni urejesho na wokovu wa wenye dhambi. Yesu alisema, “Watu wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio wagonjwa. Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi” (Marko 2:17; ona pia 1 Timotheo 1:15). Hakuna kitu kinacholeta furaha zaidi moyoni mwa Bwana au shangwe mbinguni kuliko pale mwenye dhambi anaporejeshwa katika uhusiano sahihi na Mungu (Luka 15:7, 10)

Kama watenda dhambi, sisi sote tumekosa ile alama ya Mungu. Sisi sote tunastahili hatia kama ilivyoshtakiwa: “Kama tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu” (1 Yohana 1:8). Dhambi- uasi dhidhi ya Mungu, kutotii, ukiukaji wa sheria ya Mungu-lazima iadhibiwe. Wenye dhambi hawawezi kulipa adhabu ya dhambi bila kuangamia, kwa sababu adhabu inayohitajika ni kifo (Warumi 6:23). Ni ukamilifu usio na dhambi, usio na doa wa yesu kristo pekee ndiyo unaogonga alama ya kimungu. Kristo amelipa kikamilifu dhambi. Kupitia kifo chake msalabani, Yesu aliridhisha haki ya Mungu, akiwaokoa kikamilifu na kuwaweka huru kutoka kwa laana wote wanaompokea kwa imani (Warumi 3:25).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nini maana ya mwenye dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries