settings icon
share icon
Swali

Je! Ni namna gani rehema na haki ya Mungu vinafanya kazi pamoja katika wokovu?

Jibu


Haki na rehema ya Mungu zinaonekana kutoendana pamoja. Zaidi ya yote, haki inajumuisha kudhihirisha adhabu inayostahili kwa makosa, na rehema inahusu msamaha na huruma kwa mkosaji. Walakini, sifa hizo zote mbili za Mungu zinaudna umoja katika tabia yake.

Biblia ina wingi wa marejeleo ya rehema ya Mungu. Ziadi ya aya 290 katika Agano la Kale na 70 katika Agano Jipya zina maneno ya moja kwa moja ya rehema za Mungu kwa watu wake.

Mungu alikuwa wa huruma kwa watu wa Nineve waliotubu kwa mahubiri ya Yona amabye alimwelezea Mungu kuwa "Mungu mwenye neema na huruma, si mwepesi wa hasira na umejaa upendo, ni Mungu ambaye hughairi katika kupeleka maafa" (Yona 4:2). Daudi alisema kuwa Mungu ni "Bwana ni mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo. Bwana ni mwema kwa wote" (Zaburi 145:8-9).

Lakini pia Biblia inasungumzia juu ya haki ya Mungu na ghadhabu Yake kwa dhambi. Kwa kweli, haki kamilifu ya Mungu ndio kitambulisho cha tabia Yake: "Wala hapana Mungu mwingine zaidi yangu mimi, Mungu mwenye haki na Mwokozi; hapana mwingine ila mimi" (Isaya 45:21). "Yeye ni Mwamba, kazi zake ni kamilifu, njia zake zote ni haki. Mungu mwaminifu ambaye hakosei, yeye ni mnyofu na mwenye haki" (Kumbukumbu 32:4).

Katika Agano Jipya, Paulo anasimulia kwa upana ni kwa nini hukumu ya Mungu inakuja: "Kwa hiyo, ueni kabisa chochote kilicho ndani yenu cha asili ya kidunia: yaani uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya na ulafi, ambayo ndiyo ibada ya sanamu. Kwa sababu ya mambo haya, ghadhabu ya Mungu inakuja" (Wakolosai 3:5-6).

Kwa hivyo Biblia inaonyesha wazi kweli kwamba Mungu ni mwenye huruma, lakini pia inafunua kuwa Yeye ni mwenye haki na siku moja ataonyesha haki kwa dhambi ya ulimwengu.

Katika kila dini zingine ulimwenguni ambazo zinashikilia wazo la mungu mkuu, huruma ya mungu huyo hutumika kwa haki kila wakati. Kwa mfano, katia Uislamu, Mwenyezi Mungu anaweza kutoa huruma kwa mtu, lakini hiyo inafanywa kwa kuondoa adhabu ya kipengee chochote cha sheria kimevunjwa. Kwa maneno mengine adhabu ya mkosaji yenye alistahili kwa kweli, inaondolewa kando ili huruma iweze kufikia. Mwenyezi Mungu wa Uislamu na kila mungu katika dini zisizo za Kikristo huweka kando masharti ya sheria ya maadili ili kuwa na huruma. Hivyo huruam inaonekana kupingana na haki. Kwa kiwango, katika dini hizo, uhalifu unaweza kulipa.

Ikiwa hakimu yeyote mwanadamu angetenda namna hiyo, watu wengi wasema malalamishi yao. Ni jukumu la hakimu kuhakikisha kwamba sheria imefuatwa na kwamba haki imetendeka. Hakimu mwenye anapuuza sheria anasaliti ofisi yake.

Ukristo ni wa kipekee kwa kuwa rehema ya Mungu inaonyeshwa kupitia katika haki Yake. Hakuna kuweka haki kando ili kufanya nafasi ya rehema. Fundisho la Kikristo la adhabu kwa niapa inakauli kuwa dhambi na udhalimu viliadhibiwa katika msalaba wa Kristo ni kwa sababu kuwa adhabu ya dhambi iliridhishwa kupitia dhabihu ya Kristo kwamba Mungu alizidisha rehema zake kwa wenye dhambi wasiostahili na ambao wanamtafuta Yeye kwa wokovu.

Vile Kristo alikufa kwa ajili ya wenye dhambi, pia alionyesha haki ya Mungu; kifo chake msalabani kilidhihirisha haki ya Mungu. Hili ndilo hasa mtume Paulo anasema: "wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu. Yeye ambaye Mungu alimtoa awe dhabihu ya upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alifanya hivi ili kuonyesha haki yake, kwa sababu kwa ustahimili wake aliziachilia zile dhambi zilizotangulia kufanywa. Alifanya hivyo ili kuonyesha haki yake wakati huu, ili yeye awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yule anayemwamini Yesu" (Warumi 3:24-26).

Kwa maneno mengine, dhambi zote tangu Adamu hadi wakati wa Kristo zilikuwa chini ya uvumilivu na huruma za Mungu. Mungu kwa huruma zake aliamua kuiadhibu dhambi, ambayo ingestahili kuzimu milele yote kwa wenye dhambi wote, ijapokuwa alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo na angekuwa na haki kufanya hivyo. Adamu na Hawa hawakuangamizwa papo hapo wakati walikula lile tunda walilokatazwa. Badala yake, Mungu akafanya mpango wa Mkombozi (Mwanzo 3:15). Kwa upendo wake Mungu alimtuma Mwanawe (Yohana 3:16). Kristo alifidia kila aina ya dhambi ambayo iliwai kutendwa; na hivyo Mungu alikuwa wa haki kuiadhibu dhambi, na vile vile anaweze kuhesabia haki wenye dhambi ambao watampokea Kristo kwa imani (Warumi 3:26). Haki ya Mungu na huruma zilidhihirishwa kwa kifo cha Kristo msalabani. Msalabani haki ya Mungu ilitekelezwa kwa ukamilifu (juu ya Kristo), na rehema ya Mungu ilipanuliwa kwa ukamilifu (kwa wote watakaoamini). Kwa hivyo rehema kamili ya Mungu ilitekelezwa kupitia haki yake kamilifu.

Matokeo ya mwisho ni kuwa kila mtu ambaye anamwamini Bwana Yesu ameokolewa kutokana na ghadhabu ya Mungu na badala yake wanafurahia neema na huruma zake (Warumi 8:1). Vile Paulo anasema, "Basi, kwa kuwa sasa tumehesabiwa haki kwa damu yake, si zaidi sana tutaokolewa kutoka ghadhabu ya Mungu kupitia kwake!"

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni namna gani rehema na haki ya Mungu vinafanya kazi pamoja katika wokovu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries