Swali
Roho ya binadamu ni gani?
Jibu
Roho ya mwanadamu ni sehemu isiyo ya mwili ya mwanadamu. Biblia inasema kwamba roho ya mwanadamu ni pumzi ya Mungu Mwenye Nguvu na ilipumlizwa kwa mwanadamu mwanzoni mwa uumbaji wa Mungu: "Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo" (Mwanzo 2: 7). Ni roho ya kibinadamu ambayo inatupa ufahamu wa nafsi na mambo mengine ya ajabu, ingawa ni finyu, sifa "za Mungu". Roho ya binadamu inajumuisha akili zetu, hisia, hofu, tamaa, na ubunifu. Ni roho hii inatupa uwezo wa pekee wa kuwaza na kuelewa (Ayubu 32: 8, 18).
Maneno ya roho na pumzi ni tafsiri ya neno la Kiebrania neshamah na neno la Kigiriki pneuma. Maneno hayo yanamaanisha "upepo mkali, mlipuko au msukumo." Neshamah ni chanzo cha uzima ambacho kinathamisha ubinadamu (Ayubu 33: 4). Ni roho isigusika, isiyoonekana, ambayo huongoza uhai wa kiakili na kihisia. Mtume Paulo alisema, "Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake?" (1 Wakorintho 2:11). Baada ya kifo "roho hurudi kwa Mungu aliyeiumba" (Mhubiri 12: 7; tazama pia Ayubu 34: 14-15; Zaburi 104: 29-30).
Kila mwanadamu ana roho, na ni tofauti na "roho" au uhai wa wanyama. Mungu alimfanya mwanadamu tofauti na wanyama kwa kuwa Yeye alituumba "kwa mfano wa Mungu" (Mwanzo 1: 26-27). Kwa hiyo, mtu anaweza kufikiria, kujisikia, kupenda, kubuni, kujenga, na kufurahia muziki, ucheshi, na sanaa. Na kwa sababu ya roho ya mwanadamu tuna "uhuru wa bure" ambao kwamba hakuna kiumbe mwingine duniani anao.
Roho ya kibinadamu iliharibiwa katika kuanguka. Adamu alipofanya dhambi, uwezo wake wa ushirika na Mungu ulivunjika; yeye hakukufa kimwili siku hiyo, lakini alikufa kiroho. Tangu wakati huo, roho ya binadamu imebeba madhara ya kuanguka. Kabla ya wokovu, mtu anajulikana kawa "mfu" kiroho (Waefeso 2: 1-5; Wakolosai 2:13). Uhusiano na Kristo huwamamiza roho zetu na hutuwezesha kila siku (2 Wakorintho 4:16).
Cha kushangaza, kama roho ya binadamu ilivuviwa kiungu kwa mmwanadamu wa kwanza, hivyo Roho Mtakatifu alivuviwa kwa wanafunzi wa kwanza katika Yohana 20:22: "Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu" (Yohana 20:22; tazama pia Matendo 2:38). Adamu alifanywa hai kwa pumzi ya Mungu, na sisi, kama "viumbe vipya" katika Kristo, tunafanywa kiroho hai na "Pumzi ya Mungu," Roho Mtakatifu (2 Wakorintho 5:17, Yohana 3: 3; Warumi 6: 4). Katika kumkubali Yesu Kristo, Roho Mtakatifu wa Mungu hujiunga na roho zetu kwa njia ambazo hatuwezi kuelewa. Mtume Yohana alisema, "Katika hili tunafahamu ya kuwa tunakaa ndani yake, naye ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho wake" (1 Yohana 4:13).
Tunaporuhusu Roho wa Mungu kuongoza maisha yetu, "Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu" (Waroma 8:16). Kama watoto wa Mungu, hatuongozwi tena na roho wetu wenyewe bali kwa Roho wa Mungu, ambaye anatuongoza kwenye uzima wa milele.
English
Roho ya binadamu ni gani?