settings icon
share icon
Swali

Sala ya Yabezi ni gani?

Jibu


Sala ya Yabezi inapatikana katika maelezo ya kihistoria ndani ya kizazi: "Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni. Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba" (1 Mambo ya Nyakati 4: 9-10). Sala imejulikana sana kwa sababu ya kuchapishwa katika kitabu kilichouzwa sana, Sala ya Yabesi: Kuvunja kwa Uhai wa Heri (The Prayer of Jabez: Breaking Through to the Blessed Life) (2000), na Dr Bruce Wilkinson na David Kopp.

Mambo machache yanajulikana kuhusu Yabesi, mbali na yeye kuwa mzaliwa wa Yuda, alikuwa mtu mwenye heshima, na mama yake akamwita "Yabesi" (maana yake "huzuni" au "msababisha huzuni") kwa sababu alikuwa amezaliwa kwa unchungu. Katika sala yake, Jabezi analia kwa Mungu kwa ajili ya ulinzi na baraka. Kutumia kucheza kwa maneno, Jabez, "mtu wa huzuni," anamwomba Mungu kumzuia kutokana na huzuni hiyo ambayo jina lake limekumbuka na lilipangiwa.

Sala ya Yabesi katika 1 Mambo ya Nyakati 4:10 ina ombi la haraka kwa vitu vinne:

1) baraka za Mungu. Yabesi anakubali kwamba Mungu wa Israeli ndiye chanzo cha baraka zote, na anamwomba Mungu kwa neema Yake. Bila shaka, ombi hili msingi wake ulikuwa angalau katika sehemu ya ahadi ya Baraka ya Mungu kwa Ibrahimu na wazao wake (Mwanzo 22:17).

2) Upanuzi wa eneo. Yabesi anaomba kwa ushindi na ustawi katika jitihada zake zote na kwamba maisha yake yataonekana kuwa na ongezeko.

3) kuwepo kwa mkono wa Mungu. Hii ilikuwa njia ya Yabesi ya kuomba mwongozo wa Mungu na nguvu zake kuwa dhahiri katika maisha yake ya kila siku.

4) Ulinzi dhidi ya madhara. Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kuomba kwa njia hii: "Baba yetu uliye mbinguni. . . Tuokoe kutoka kwa mwovu " (Mathayo 6: 9, 13). Yabesi anamtazama kwa Mungu kwa ujasiri kama mlinzi wake.

Lengo la Yabesi katika sala yake ilikuwa kuishi bila huzuni, na jambo la mwisho tunalojifunza juu yake ni kwamba Mungu aliisikia na akajibu sala yake. Kama sala ya Sulemani ya unyenyekevu kwa ajili ya hekima (1 Wafalme 3: 5-14), sala ya Yabesi ya kujishughulisha kwa baraka ilijibiwa. Mafanikio Yabesi aliyofurahia yalikuwa zaidi ya huzuni wa mwanzo wake. Sala ya Yabesi ilishinda jina la Yabesi.

Sala ya Yabesi ni mfano mzuri wa jinsi tunapaswa kufanya sala kuwa kipaumbele katika maisha yetu. Tunapaswa daima kumtafuta Mungu kwa msaada wetu wakati wa haja, na tunaweza kuchukua maombi yetu moja kwa moja kwenye kiti cha neema (Waebrania 4:16). Pamoja na maombi ya Hana, Yona, Hezekia, Paulo-na kwa kweli maombi ya mfano wa Bwana (Mathayo 6: 9-13) - Sala ya Yabesi inatoa mfano mzuri wa mtoto wa Mungu akikaribia Aliye Mkuu kwa unyenyekevu, imani, na kutegemea wema wa Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Sala ya Yabezi ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries