Swali
Je! Kanisa linapaswa kutoa sehemu ya kumi ya sadaka inayopokea?
Jibu
Watu chini ya sheria ya Agano la Kale walihitajika kutoa zaka (hasa, "kumi") ya ongezeko lao lote. Sehemu ya kumi ilielewaka kuwa ni jibu sahihi kwa baraka za Mungu. Watu wengi leo wanajiuliza kama zaka bado zinatumika kwa waumini kwani hatuko "chini ya sheria." Ingawa makanisa hayajapewa asilimia katika Agano Jipya, kanuni ya kutoa kwa uwiano inafundishwa (1 Wakorintho 16: 2; 2 Wakorintho 8), na waumini wengi wanaona kuwa ni fursa ya kutumia zaka kama ruwaza ya kutoa. Agano Jipya pia linaandika kuwa waumini katika kanisa walikuwa wakikusanya ili kutoa kwa huduma zingine.
Ingawa inaweza kuwa hakuna mstari fulani unaoashiria kuwa kanisa linapaswa kutoa zaka kwa huduma zingine, inaonekana kwamba makanisa yanapaswa kutoa ukarimu katika kusaidia huduma zingine kama Bwana anawasitawisha. Makanisa mengine yanaweka kiasi fulani katika bajeti yao kuelekea "huduma za nje" kama njia ya kuwasaidia kuzingatia uwiano kwa mahitaji makubwa ya ulimwengu unaowazunguka. Sio kawaida kwa kanisa kutoa sehemu ya kumi (asilimia 10) au asilimia nyingine kwa ujumbe wa kigeni, kwa mfano. Hii haipaswi kuwa sharti la kisheria. Badala yake, inapaswa kuwa sherehe ya furaha ya utoaji wa Bwana.
English
Je! Kanisa linapaswa kutoa sehemu ya kumi ya sadaka inayopokea?