Swali
Ni nini ilikuwa umuhimu wa hekalu pazia kuwa vipande viwili wakati Yesu alikufa?
Jibu
Wakati wa uhai wa Yesu, hekalu takatifu katika Yerusalemu lilikuwa ndilo nguzo muhimu katika maisha ya kidini ya Kiyahudi. Hekalu ilikuwa mahali ambapo dhabihu za wanyama zilikuwa zinafanyiwa na ibada kwa mujibu wa sheria ya Musa iliyofuatwa kwa uaminifu. Waebrania 9: 1-9 inatuambia kwamba katika hekalu pazia ilitenganisha pahali takatifu zaidi ya patakatifu – mahali ambapo uwepo wa mungu uishi ulimwenguni- kutoka kwa mahali pengine Hekaluni ambapo watu waliishi. Hii iliashiria kuwa binadamu alitenganishwa kutoka Mungu na dhambi (Isaya 59: 1-2). Ni kuhani mkuu tu aliyeruhusiwa kupita zaidi ya hii pazia mara moja kila mwaka (Kutoka 30:10, Waebrania 9: 7) aingie katika uwepo wa Mungu kwa ajili ya waisraeli wote na kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zao (Mambo ya Walawi 16).
Hekalu la Sulemani lilikuwa dhiraa 30 kuelekea juu (1 Wafalme 6: 2), lakini Herode alikuwa amezidisha urefu hadi dhiraa 40, kulingana na maandiko ya Josephus,mhisitoria Myahudi wa karne ya kwanza. Hakuna uhakika kwa kipimo halisi cha dhiraa moja, lakini ni salama kudhani kwamba pazia hili lilikuwa mahali fulani karibu futi 60 juu. Josephus pia anatuambia kwamba pazia hili lilikuwa na upana wa inchi nne na kwamba farasi hata wafungwe kwa kila upande hawangeweza kuirarua dhiraa hii . Kitabu cha Kutoka kinafundisha kwamba pazia hii pana iliundwa kwa mtindo kutoka samawati( buluu), zambarau, na nyekundu, na kitani kizuri cha kusokotwa.
Ukubwa na unene wa pazia unafanya matukio yanayotokea wakati wa kifo cha Yesu juu ya msalaba kuwa wa maana sana. "Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama, pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka."(Mathayo 27: 50-51a).
Hivyo, je,tunafanya nini kwa hili? Ni umuhimu gani dhiraa hii ilyopasuka inayo kwetu siku hizi? Zaidi ya yote, kuraruriwa kwa dhiraa wakati wa kifo cha Yesu kuliashiria kidrama kwamba kafara yake, kumwaga damu yake mwenyewe,kulikuwa upatanisho wa kutosha kwa ajili ya dhambi.Kuliashiria kwamba sasa njia ya kuingia Patakatifu pa Patakatifu ilikuwa wazi kwa watu wote, kwa wakati wote, Wayahudi na Mataifa.
Wakati Yesu alikufa, dhiraa iliraruka, na Mungu akatoka mahali pale kwamba kamwe hangeishi tenai katika hekalu zilizojengwa na binadamu (Matendo 17:24). Mungu alikuwa amemalizana na hekalu hilo na mfumo wake wa kidini, na hekalu na Yerusalemu ziliachwa "zikiuzunika kwa ukiwa" (kuharibiwa na Warumi) katika mwaka 70 A.D., tu kama Yesu alitabiri katika Luka 13:35. Bora tu Hekalu lilisimama, liliashiria kuendelea kwa Agano la Kale. Waebrania 9: 8-9 inarejelea umri uliokuwa unapita mara tu agano jipya liliimarishwa (Waebrania 8:13).
Kwa maana, dhiraa iliashiria Kristo mwenyewe kama njia ya pekee kwenda kwa Baba (Yohana 14: 6). Hii imeonyeshwa kwa ukweli kwamba kuhani mkuu alipaswa kuingia Patakatifu pa Patakatifu kupitia kwa dhiraa . Sasa Kristo ni Kuhani wetu mkuu zaidi, na kama waumini katika kazi yake iliyokamilika,tunashiriki katika Ukuhani wake bora.Tunaweza sasa kuingia Patakatifu pa Patakatifu kupitia kwake. Waebrania 10: 19-20 inasema kwamba “Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, njia ile aliyotuanzia ilyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia , yaani, mwili wake."Tunaona mwili wa Yesu ukiraruriwa kwa ajili yetu tu kama alivyorarua pazia kwa ajili yetu.
Pazia kupasuliwa kutoka juu hadi chini ni ukweli wa hisitoria. Umuhimu mkubwa wa tukio hili umeelezewa kwa undani kwa utukufu katika Waebrania. Mambo ya hekalu yaliashiria mambo ambayo yangekuja, na yote yatuashiria kwa Yesu Kristo. Alikuwa pazia kwa Patakatifu pa Patakatifu, na kupitia kifo chake waaminifu sasa wanaweza kumpata Mungu bila gharama.
Pazia katika hekalu ilikuwa ukumbusho wa mara kwa mara kwamba dhambi ilimfanya binadamu kutofaa kwa uwepo wa Mungu. Ukweli kwamba sadaka ya dhambi ilitolewa kila mwaka na mara kwa mara dhabihu zingine zilirudiwa kila siku ilionyesha bayana kwamba dhambi kwa kweli haingeweza kupatanishwa kwa au kufutika na sadaka za wanyama tu. Yesu Kristo,kupitia kwa kifo chake,ameondoa vikwazo vilivyo kati ya Mungu na mwanadamu, na sasa tunaweza kumkaribia kwa kujiamini na ujasiri (Waebrania 4: 14-16).
English
Ni nini ilikuwa umuhimu wa hekalu pazia kuwa vipande viwili wakati Yesu alikufa?