Swali
Siku ya Upatanisho ni nini (Yom Kippur)?
Jibu
Siku ya Upatanisho (Mambo ya Walawi 23: 27-28), pia inajulikana kama Yom Kippur, ilikuwa siku takatifu sana ya sikukuu zote za Israeli na sherehe, iliyofanyika mara moja kwa mwaka siku ya kumi ya Tishri, mwezi wa saba wa kalenda ya Kiebrania. Siku hiyo, kuhani mkuu alifanya ibada kuu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi za watu. Kama ilivyoelezwa katika Mambo ya Walawi 16: 1-34, ibada ya upatanisho ilianza na Haruni, au makuhani wakuu wa Israeli waliokuja, wakiingia katika mahali patakatifu. Sherehe ya siku hiyo imethibitishwa na Mungu akimwambia Musa amuonye Haruni asiingie mahali patakatifu sana wakati wowote alipohisi kufanya hivyo, tu siku hii maalum mara moja kwa mwaka, asije akafa (mstari wa 2). Hii haikuwa sherehe ya kuchukuliwa kiholela, na watu walipaswa kuelewa kuwa upatanisho wa dhambi ulifanyika katika amri ya Mungu.
Kabla ya kuingia katika hema, Haruni alikuwa aoge na kuvaa mavazi maalum (mstari wa 4), kisha atamtoa yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake, na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake (mstari wa 6, 11). Damu ya ng'ombe huyo alipaswa kuinyunyizia kwenye sanduku la agano. Kisha Haruni alikuwa alete mbuzi mbili, moja ya dhabihu "Kwa sababu ya mambo machafu ya wana wa Israeli, na kwa sababu ya makosa yao" (mstari wa 16), na damu yake ikanyunyuziwa juu ya sanduku la agano. Mbuzi mwingine alikuwa kutumika kama sadaka. Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari. (mstari wa 21). Mbuzi huyo aliungama juu yake, dhambi zote za watu, ambazo zilisamehewa kwa mwaka mwingine (mstari wa 30).
Umuhimu wa mfano wa ibada, hasa kwa Wakristo, unaonekana kwanza katika kuosha na kutakaswa kwa kuhani mkuu, mtu ambaye alimtoa mbuzi, na mtu ambaye alichukua wanyama waliotolewa nje ya kambi ili kuchoma mizoga (mstari wa 4 , 24, 26, 28). Sikukuu za Israeli za kuosha zilihitajika mara nyingi katika Agano la Kale na zinaonyesha haja ya wanadamu kusafishwa dhambi. Pindi tu Yesu alikuja kufanya dhabihu ya "mara moja kwa wote" ambayo ilipelekea kuti kikomo sherehe za kutakasa. (Waebrania 7:27). Damu ya ng'ombe na mbuzi ingeweza kufuta dhambi tu ikiwa ibada ilifanyika kila mwaka, ilhali dhabihu ya Kristo ilikuwa ya kutosha kwa dhambi zote za wote ambao wangeweza kumwamini Yeye. Wakati dhabihu yake ilifanyika, alisema, "Imekamilishwa" (Yohana 19:30). Kisha akaketi chini ya mkono wa kuume wa Mungu, na hakuna dhabihu zaidi iliyohitajika (Waebrania 10: 1-12).
Utoshelezi na ukamilifu wa dhabihu ya Kristo pia huonekana katika mbuzi hawa wawili. Damu ya mbuzi wa kwanza ilinyunyiziwa kwenye sanduku la agano, ikiondoa ghadhabu ya Mungu kwa mwaka mwingine. Mbuzi wa pili aliondoa dhambi za watu jangwani ambako zilisahaulika na hazikushikamana tena na watu. Dhambi ilipatanishwa na kulipiwa katika njia ya Mungu-tu kwa dhabihu ya Kristo msalabani. Upatanishi ni tendo la kuondoa ghadhabu ya Mungu, utakaso ni tendo la kuondoa dhambi na kuitoa kutoka kwa mwenye dhambi. Yote mawili yanapatikana kwa milele katika Kristo. Alipokuwa akijitolea nafsi yake msalabani, aliondoa ghadhabu ya Mungu juu ya dhambi, akichukua ghadhabu juu yake mwenyewe: " Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye!" (Warumi 5: 9). Kuondolewa kwa dhambi kwa mbuzi wa pili ilikuwa mfano wa ahadi ya kwamba Mungu ataondoa makosa yetu Kama vile mashariki ilivyo mbali na magharibi.(Zaburi 103: 12) na kwamba hatazikumbuka tena (Waebrania 8: 12; 10:17). Wayahudi leo bado wanaadhimisha Siku ya Upatanisho ya kila mwaka, ambayo hufanyika siku tofauti kila mwaka katika mwezi wa Septemba-Oktoba, kwa kawaida wakiadhimisha siku hii takatifu kwa kipindi cha saa 25 cha kufunga na kuomba sana, mara nyingi wakitumia wakati huu katika huduma za sinagogi.
English
Siku ya Upatanisho ni nini (Yom Kippur)?