settings icon
share icon
Swali

Je! Ni nini maana ya siku ya hukumu?

Jibu


Siku ya hukumu ni siku ya hukumu ya mwisho ya Mungu juu ya mwandamu mwenye dhambi. Kunazo baadhi za vifungu katika Maandiko ambavyo hurejelea hukumu ya mwisho baada ya kifo wakati wa nyakati za mwisho wakati kila mtu atasimama mbele za Mung una atawatolea hukumu ya maisha yao.

Biblia inatuonya dhidi ya Siku ya Hukumu. Malaki nabii aliandika, "'Hakika siku inakuja, itawaka kama tanuru. Wote wenye kiburi na kila mtenda mabaya watakuwa mabua makavu, na siku ile inayokuja itawawasha moto," asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. "Hakuna mzizi wala tawi litakalosalia kwao'" (Malaki 4: 1). Yohana Mbatizaji alisema juu ya hitaji la "kuikimbia ghadhabu inayokuja" (Luka 3: 7). Paulo aliwaandikia wale wasiotubu: "Lakini kwa sababu ya ukaidi wenu na mioyo yenu isiyotaka kutubu, mnajiwekea akiba ya ghadhabu dhidi yenu wenyewe kwa siku ile ya ghadhabu ya Mungu, wakati hukumu yake ya haki itakapodhihirishwa. 6Kwa maana Mungu atamlipa kila mtu sawasawa na matendo yake" (Warumi 2: 5-6; linganisha na Zaburi 62:12). Siku ya Hukumu ni jambo la uhakika.

Maandiko yamenakili mara kadhaa wakati Mungu alitoa hukumu kwa watu binafsi na mataifa. Kwa mfano, Isaya 17-23 ni safu ya hukumu iliyotangazwa dhidi ya Dameski, Misri, Kushi (Uapeshi), Babeli, Misri, Uarabuni, Yerusalemu, na Tiro. Hukumu hizi za kila taifa binafsi hutumika kama kielelezo cha hukumu itakayokuja (Isaya 24 inaelezea hukumu ya Mungu juu ya ulimwengu wote). Mara nyingi huwa kuna hukumu ya muda juu ya dhambi ambayo hufanyika katika maisha haya, lakini hukumu ya mwisho itatokea mwishoni mwa wakati. Ufunuo 19: 17-21 inarekodi vita kubwa ambavyo maadui wa Mungu wanachinjwa (na hii inaweza kuwa taswira ambayo watu wengi hufikiria wanapofikiria Siku ya Hukumu). Walakini, hii ni hukumu ya muda tu kwa watu walio hai wakati wa vita kubwa. Hukumu ya mwisho itajumuisha kila mtu ambaye amewahi kuishi na itawasalimisha watu kwa hatima yao ya mwisho.

Ufunuo 20:11-15 ina mojawapo ya maelezo kabambe ya Siku ya Hukumu: "Kisha nikaona kiti kikubwa cheupe cha enzi pamoja na yeye aliyeketi juu yake. Dunia na mbingu zikaukimbia uso wake wala mahali pao hapakuonekana. Nami nikawaona wafu wakubwa na wadogo, wakiwa wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi na vitabu vikafunguliwa. Pia kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni kitabu cha uzima. Hao wafu wakahukumiwa sawasawa na matendo yao kama yalivyoandikwa ndani ya hivyo vitabu. Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake, nayo mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Kila mtu akahukumiwa kulingana na yale aliyoyatenda. Kisha mauti na Kuzimu zikatupwa katika ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. Iwapo mtu jina lake halikuonekana katika kile kitabu cha uzima, alitupwa ndani ya lile ziwa la moto."

Katika kifungu hiki, tunaona kuwa Mungu ndiye hakimu mkuu. Kulingana na Yesu, ni Mwana ambaye atatoa hukumu ya miwsho, kwa hivyo ni lazima iwe ni yule ambaye ameketi katika kiti cha enzi (Yohana 5:16-30; linganisha Ufunuo 7:17).

Pia, tunaona kwamba hukumu hii ni yenye mambo mengi. Hawa ni wale wote waliokufa, wadogo na wakubwa (wasio na maana na walio na maana). Hakuna atakaye hepa Siku ya Hukumu.

Hukumu ya Siku ya Hukumu itafanywa kulingana na yale ambayo watu binafsi wamefanya katika maisha yao-wanahukumiwa kulingana na matendo yao. Mtu hatahukumiwa kulingana na kile wengine walifanya au hawakufanya; anasimama mbele ya hukumu peke yake, akiwajibika kwa matendo yake mwenyewe.

Ijapokuwa hukumu ni kwa misingi ya matendo, haitakuwa ni harakati ya kuweka mizani kati ya mazuri na mabaya. Mwishowe, kuingia kwetu mbinguni au Jahannam ni kwa misingi ya ikiwa majina yetu yameandikwa katika kitabu cha uzima. Wale ambao majina yao hayajaandikwa katika kitabu cha uzima watatupwa katika ziwa la moto. Ufunuo 21:27 inasisitiza kuwa ni wale tu pekee ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo wataingia mbingu mpya nan chi mpya.

Kwa mjibu wa viwango virefu vilivyohusika (hatima ya milele) itampasa mtu ahakikishe kuwa amejiandaa mapema kwa Siku ya mwisho ya Hukumu. Je! Ni namna gani mwenye dhambi aliya na hatia (na sisi sote tuna hatia) atapata jina lake liandikwe katika Kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo na hivyo kuweza kusimama mbele Yake katika hukumu ya mwisho na kutangazwa "kuwa huna hatia"? Je! ni namna gani mtenda dhambi anaweza kuhesabiwa haki mbele za Mungu mtakatifu na mwadilifu na kujiepusha na ghadhabu yake? Biblia inatupa jibu la wazi.

"Kwa hiyo, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa imani, tuna amani na Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo" (Warumi 5:1). Mtu aliye na imani katika Kristo huku imekwisha tolewa. Mtu amekwisha hesabiwa haki-hivyo ni kusema, ametangazwa kuwa mwenye haki- na Mungu kulingana na kazi kamilifu ya Yesu kwa niapa yake. Ni kana kwamba huku ya mwisho ambayo ingetokea Siku ya Hukumu imekwisha tolewa. Wale wote walio na imani katika Kristo wametangazwa kuwa wenye haki, na majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo. Hawana lolote la kuogopa Siku hiyo ya Hukumu kwa sababu adhabu yao imekwisha bebwa na Kristo msalabani (Warumi 8:1). Kwa wale walio na imani katika Kristo, Siku ya Hukumu itakuwa siku yao ya mwisho ya kuokolewa wakati watakapokombolewa kutoka kwa madhara yote ya dhambi (Malaki 4:2-3).

"Kama vile mwanadamu alivyowekewa kufa mara moja tu na baada ya kufa akabili hukumu, vivyo hivyo Kristo alitolewa mara moja tu kuwa dhabihu ili azichukue dhambi za watu wengi. Naye atakuja mara ya pili, sio kuchukua dhambi, bali kuwaletea wokovu wale wanaomngoja kwa shauku" (Waebrania 9:27-28).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni nini maana ya siku ya hukumu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries