settings icon
share icon
Swali

Je, ni aina gani ya taaluma ambazo Mkristo anapaswa kuzingatia?

Jibu


Wakati mwingine tunadhani kwamba Wakristo wanapaswa kutamani "taaluma za Kikristo" kama vile kufanya kazi kwenye kanisa au huduma ya kanisa. Tunaweza kutambua kwamba Wakristo wanaweza pia kufanya kazi nje ya kuta za kanisa au jina la Kikristo, lakini huwa tunapenda kujiekea mipaka kwa "kazi" za taaluma. Wakristo wanaweza kuwa madaktari, wauguzi, walimu, wafanyakazi wa huduma za watoto, wafanyakazi wa kijamii, maafisa wa sheria, au washauri. Lakini mfanyabiashara? Mwanasheria? Mtaalamu? Mvumbuzi? Wajenzi? Mtengenezaji wa mtindo? Nakala ya habari? Mtayarishaji wa TV? Muziki? Msanii? Tunapenda kutoorodhesha kazi hizi kati ya kazi muhimu sana kwa Wakristo. Hakuna kisuizi kibiblia kuhusu msimamo kama huo.

Wakristo wanaweza kufikiria kala kazi yoyote. Paulo aliwaandikia Wakorintho, " Lakini kama Bwana alivyomgawia kila mtu, kama Mungu alivyomwita kila mtu…. Ndivyo ninavyoagiza katika makanisa yote... Kila mtu na akae katika hali ile ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa… Je! Uliitwa u mtumwa? Usione ni vibaya lakini kama ukiweza kuwa na uhuru, afadhali kuutumia (Lakini ikiwa unaweza kupata uhuru wako, uwe na fursa yako.) ... Ndugu zangu, kila mtu na akae mbele za Mungu katika hali iyo hiyo aliyoitwa nayo" (1 Wakorintho 7:17, 20-21, 24). Paulo hawaambii waumini kuacha kazi zao za sasa na kuwa wamishonari au wachungaji. Anawaambia waendelee kuwa kwenye wako na wamtumikie Mungu huko. Paulo aliandika kitu sawa kwa Wakolosai, "Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye" (Wakolosai 3:17). Sio kile tunachofanya ambacho ni muhimu, bali ni kwa yule tunayemfanyia. Tunamtukuza Mungu tunapofanya kazi kwa bidii na kwa furaha, iwe ni uchungaji, mwekezaji, mwigizaji, mama wa kukaa nyumbani, karani wa mauzo, au kazi nyingine.

Kuchagua kazi inaweza kuwa vigumu. Kwa wazi, ni suala la maombi. Unapaswa kutafuta mwongozo wa Mungu kwa mapenzi Yake kwa maisha yako. Inaweza pia kusaidia kuchunguza karamai maalum ambazo Mungu amekupa. Ametuumba kila mmoja wetu tofauti (1 Wakorintho 12, Warumi 12: 4-8) na tamaa za kipekee, vipaji, na maslahi, na kwa madhumuni ya pekee. Pia ni muhimu kuzungumza na wale wanaokujua vizuri. Watu hao wanaweza kuwa kama washauri wenye hekima (Mithali 15:22), mara nyingi hutoa ufahamu wenye manufaa. Inaweza pia kuwa na manufaa kuhojiana na mtu kuhusu nyanja ya taluuma yako au ikiwa kuna uwezekano wa kushinda pamoja nao siku mzima kazini mwao au kujitolea katika uwanja unaojihisi kufutiwa.

Wakristo wanaweza kuzingatia kazi yoyote ambayo wanaweza kumheshimu Mungu na kutumia ujuzi wa kipekee ambayo Mungu aliwaumbia. Bila shaka, kuna baadhi ya kazi ambazo humdhalilisha Mungu-wingi wa hizo sio za sheria, kama uzinzi au ponografia. Lakini kazi yoyote ambayo haihuzishi dhambi katika utekelezaji wake ni kazi ya Kikristo yenye utukufu na inaweza kufanywa kwa utukufu wa Mungu (Wakolosai 3:23).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni aina gani ya taaluma ambazo Mkristo anapaswa kuzingatia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries