settings icon
share icon
Swali

Je, ni taji gani za mbinguni ambazo waumini wanaweza kupokea mbinguni?

Jibu


Kuna taji tano za mbinguni zilizotajwa katika Agano Jipya ambazo zitazawadiwa waumini. Ni taji zisizoharibika, taji ya kufurahi, taji ya haki, taji ya utukufu, na taji ya uzima. Neno la Kiyunani lililotafsiriwa kuwa "taji" ni stephanos (chanzo cha jina lake Stefano) na ina maana ya "beji ya kifalme, tuzo katika michezo ya umma au alama ya heshima kwa ujumla." Taji zilitumiwa wakati wa michezo ya Kigiriki ya kale; shada la maua au shada la maua ya majani iliwekwa kwenye kichwa cha mshindi kama tuzo ya kushinda mashindano ya riadha. Heshima hii ya riadha inatumiwa kistiari katika Agano Jipya kwa tuzo za mbinguni Mungu anaahidi kwa wale ambao ni waaminifu. 1 Wakorintho 9: 24-25 hufafanua bora zaidi jinsi taji hizi zinavyopeanwa.

1) Korona isiyoharibika — (1 Wakorintho 9: 24-25) "Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmjo? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate. Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika". Mambo yote juu ya dunia hii yataharibika na yataangamia. Yesu anatuhimiza tusiweke hazina zetu duniani "nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba" (Mathayo 6:19). Hii ni sawa na kile Paulo alichosema kuhusu shada la maua ya majani ya mchezaji ambayo yaligeuka ngumu lakini nyepesi kuvunjika na ikaanguka. Sio hivyo kwa taji ya mbinguni; uvumilivu wa uaminifu unashinda tuzo ya mbinguni ambayo ni "urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu" (1 Petro 1: 3-5).

2) Taji ya Kufurahi — (1 Wathesalonike 2:19) "Maana tumaini letu, au furaha yetu, au taji ya kujionea fahari, ni nini? Je! Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu, wakati wa kuja kwake?" Mtume Paulo anatuambia katika Wafilipi 4: 4 "Furahini katika Bwana siku zote" kwa baraka nyingi Mungu wetu mwenye neema amemimina juu yetu. Kama Wakristo tunayo zaidi katika maisha haya kufurahia zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Luka anatuambia kuna furaha hata sasa mbinguni (Luka 15: 7). Taji ya kushangilia itakuwa zawadi yetu ambapo "Mungu ataifuta kila chozi . . . wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita "(Ufunuo 21: 4).

3) Taji ya haki — (2 Timotheo 4: 8) "Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake." Tunarithi taji hii kwa njia ya haki ya Kristo; bila haki ya Kristo, taji hii haiwezi kupatikana. Kwa sababu inamilikiwa katika haki, na haipatikani kwa nguvu na udanganyifu kama taji za kidunia wakati mwingine zinakuwa, ni taji ya milele, iliyoahidiwa kwa wote wanaompenda Bwana na wanasubiri kwa hamu kurudi Kwake. Kupitia kuvumilia kwetu wa kuvunjwa moyo, mateso, kuteseka, au hata kifo, tunajua kwa hakika tuzo yetu ni pamoja na Kristo milele (Wafilipi 3:20). Taji hii sio kwa wale ambao wanategemea haki zao wenyewe. Tabia hiyo inazalisha tu ufidhuli na kiburi, sio na hamu ya kuwa pamoja na Bwana.

4) Taji ya Utukufu — (1 Petro 5: 4) "Na Mchungaji Mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka." Neno hili utukufu ni neno la kupendeza, linalorejelea asili ya Mungu na matendo Yake. Inahusisha utukufu Wake mkubwa na mwangaza. Kumbuka Stefano ambaye, wakati alipigwa mawe hadi kufa, alikuwa na uwezo wa kuangalia mbinguni na kuona utukufu wa Mungu (Matendo 7: 55-56). Neno hili pia linamaanisha kwamba sifa na heshima tunayotoa kwa Mungu ni kutokana Naye kwa sababu ya Yule ako (Isaya 42: 8; 48:11; Wagalatia 1: 5). Waumini wamebarikiwa sana kuingia katika ufalme na kupokea taji ya utukufu, kupokea mfano wa Kristo mwenyewe. Vile Paulo alisema, "Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu" (Warumi 8:18).

5) Taji la Uzima — (Ufunuo 2:10) "Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima." Taji hili ni kwa waumini wote lakini ni bora hasa kwa wale ambao huvumilia mateso, ambao ni jasiri kwa mateso kwa ajili ya Yesu, hata kwa kiwango cha kufa. Katika Maandiko neno uzima mara nyingi hutumiwa kuonyesha uhusiano unaofaa na Mungu. Yesu alisema, "Nimekuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele" (Yohana 10:10). Kama vile hewa, chakula, na maji ni muhimu kwa maisha ya kimwili, Yesu ni muhimu kwa maisha ya kiroho. Yeye ndiye anatoa "maji yaliyo hai." Yeye ndiye "mkate wa uzima" (Yohana 4:10; 6:35). Maisha yetu ya kidunia yataisha. Lakini tuna ahadi ya kushangaza kwa wote wanaokuja kwa Mungu kwa njia ya Yesu: "Na hii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani, uzima wa milele" (1 Yohana 2:25).

Yakobo anasema kwamba taji hii ya maisha ni kwa wote wanaompenda Mungu (Yakobo 1:12). Swali basi ni, jinsi gani tunavyoonyesha upendo wetu kwa Mungu? Mtume Yohana anajibu hili: "Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito"(1 Yohana 5: 3). Kama watoto wake tunapaswa kushika amri zake, kumtii kwa uaminifu. Kwa hivyo, tunapovumilia majaribio yasiyoepukika, uchungu, maumivu ya moyo, na taabu – kwa muda wote tutakapoishi-tuweze kusonga mbele, daima "tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu" (Waebrania 12: 2) na kupokea taji ya uzima ambayo inatungojea.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni taji gani za mbinguni ambazo waumini wanaweza kupokea mbinguni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries