Swali
Ni nini teolojia ya matendo?
Jibu
Theologia ya Vitendo, kama jina lake linamaanisha, ni utafiti wa theologia kwa njia ambayo inalenga kuifanya kuwa muhimu au inayofaa. Njia nyingine ya kusema ni kwamba ni utafiti wa teolojia ili iweze kutumiwa na iwe ya muhimu kwa haja za kila siku. Mwanaseminari mmoja anaelezea Mpango wake wa Theologia ya Ufanisi kama "kujitolea kwa matumizi kitheolojia katika vitendo " na kwamba "kwa ujumla inajumuisha vidokezo vya teolojia ya wachungaji, uhuburi, na elimu ya Kikristo, miongoni mwa zingine." Seminari nyingine inaona madhumuni ya teolojia ya vitendo kama kusaidia kuandaa wanafunzi kutafsiri ujuzi uliopatikana katika huduma bora kwa watu. Kufanya jambo hili linahusisha maisha ya kibinafsi na ya familia pamoja na huduma za utawala na elimu katika kanisa. Wanasema kwamba lengo la teolojia ya vitendo ni kuendeleza mawasiliano ya ufanisi wa Maandiko ambao yana maono kwa ukuaji wa kiroho wa waumini wakati wanakuwa viongozi wa watumishi.
Wengine wanaona teolojia ya vitendo kuwa tu jina la kiufundi zaidi kwa mafundisho ya maisha ya Kikristo. Mkazo wake ni juu ya jinsi mafundisho yote ya Maandiko yanapaswa kuathiri njia tunayoishi hii leo katika dunia hii ya sasa. Mkazo wa teolojia ya vitendo sio tu kutafakari au kuelewa mafundisho ya ya dini bali kukua zaidi ya hapo, kwamba tunayatumia mafundisho hayo katika maisha ya Kikristo ya kila siku ili tuweze "kuchangia ulimwengu kuwa kile ambacho Mungu anataka uwe."
Msingi wa mipango ya teolojia ya vitendo ni kwamba viongozi wa Kikristo wa baadaye wanahitaji kuwa na vifaa sio ujuzi tu wa kitheolojia lakini pia na ujuzi wa kitaaluma muhimu wa kuhudumia kwa ufanisi katika ulimwengu wa kisasa. Mara nyingi mipango hii inatumia mahubiri, elimu ya Kikristo, ushauri na mifumo ya kiliniki ili kutoa fursa ya kuwafunza na kuwandaa viongozi wa Kikristo wa baadaye.
English
Ni nini teolojia ya matendo?