settings icon
share icon
Swali

Toba ni nini na ni muhimu kwa ajili ya wokovu?

Jibu


Wengi huelewa neno toba kuwa na maana ya "kugeuka kutoka dhambi" Hii si tafsiri ya Biblia ya toba. Katika Biblia, neno toba lina maana ya "kubadili mawazo ya mtu." Biblia pia inatuambia kwamba toba ya kweli itasababisha mabadiliko ya vitendo (Luka 3:8-14; Matendo 3:19). Matendo 26:20 inasema, "bali kwanza niliwahubiri wale wa Dameski na Yerusalemu, na katika nchi yote ya Uyahudi, na watu wa Mataifa kwamba watubu na kumwelekea Mungu, wakiyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao." Ufafanuzi kamili wa Biblia wa toba ni badiliko la nia akilini ambayo matokeo yake yamo katika matendo yaliyobadilika.

Basi, kuna uhusiano gani kati ya toba na wokovu? Kitabu cha Matendo kinaonekana kuzingatia toba hasa inayo husu wokovu (Matendo 2:38; 3:19; 11:18; 17:30; 20:21; 26:20). Kutubu, kuhusiana na wokovu, ni kubadili akili yako katika suala la Yesu Kristo. Katika mahubiri ya Petro siku ya Pentekoste (Matendo 2), anamalizia na wito kwa watu watubu (Matendo 2:38). Tubu kutokana na nini? Petro anawaita watu walio mkataa Yesu (Matendo 2:36 ) wabadili mawazo yao kumhusu, kutambua kwamba hakika Yeye ni "Bwana na Kristo" (Matendo 2:36 ). Petro anawaita watu wabadili mawazo yao kutoka kumkataa Kristo kama Masihi na kuwa na imani kwake kama Masihi na mwokozi wetu.

Toba na imani inaweza kueleweka kama vile "pande mbili za sarafu moja." Haiwezekani kuiweka imani yako katika Yesu Kristo kama mwokozi bila kwanza kubadilisha mawazo yako kumhusu yeye na chenye amefanya. Hata kama ni toba ya katao ya makusudi au toba ya kutojua au kutokua na haja, ni badiliko la akili. Toba ya kibiblia, uhusiana na wokovu, ni kubadilisha mawazo yako kutoka kwa kumkataa Kristo hadi kuwa na imani katika Kristo.

Ni muhimu sana tuelewe kuwa toba si kazi sisi huifanya ili tupate wokovu. Hakuna mtu anayeweza kutubu na kuja kwa Mungu, isipokuwa Mungu amvute huyo mtu kwake (Yohana 6:44). Matendo 5:31 na 11:18 zinaonyesha kwamba toba ni kitu ambacho Mungu anatoa - inawezekana tu kwa sababu ya neema yake. Hakuna mtu anaweza kutubu, isipokuwa Mungu ampe toba. Wokovu wote, ikiwa ni pamoja na toba na imani, ni matokeo ya Mungu kutuvuta kwake, kuyafungua macho yetu, na kubadilisha mioyo yetu. Uvumilivu wa Mungu hutuongoza sisi kutubu (2 Petro 3:9), kama ilivyo wema wake (Warumi 2:4).

Huku toba ikiwa si kazi inayotuletea wokovu, toba kwa ajili ya wokovu huishia katika matendo. Ni vigumu sana kubadili akili yako kikamilifu bila ya kusababisha mabadiliko katika matendo. Katika Biblia, toba matokeo yake ni mabadiliko ya tabia. Hiyo ndio sababu ni kwa nini Yohana Mbatizaji aliwaita watu "kuzaa matunda yapasayo toba" (Mathayo 3:8). Mtu ambaye kwa kweli ametubu kutoka kwa kumkataa Kristo hadi imani katika Kristo atatoa ushahidi wa maisha yaliyobadilishwa (2 Wakorintho 5:17, Wagalatia 5:19-23; Yakobo 2:14-26). Toba, ikieleweka vizuri, ni muhimu kwa wokovu. Toba ya kibiblia ni kubadilisha mawazo yako kuhusu Yesu Kristo na kumgeukia Mungu katika imani kwa wokovu ( Matendo 3:19). Kugeuka kutoka dhambi sio fafanuzi sahihi ya toba, lakini ni mojawapo ya matokeo ya kweli, toba iliyoweka misingi yake katika kuelekea kwa Bwana Yesu Kristo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Toba ni nini na ni muhimu kwa ajili ya wokovu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries