settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu tofauti za umri katika mahusiano?

Jibu


Biblia mara chache inatupa mifano ya umri katika mahusiano ya ndoa (au katika hali nyingine yoyote, kwa jambo hilo). Tunajua kwamba Ibrahimu alikuwa na umri wa miaka 10 zaidi ya Sarah (Mwanzo 17:17), lakini hakuna wanandoa wengine katika Biblia ambapo umri wa watu wote unaangaziwa. Mara nyingi hufikiriwa, kwa mfano, kwamba Yosefu alikuwa na umri zaidi kuliko Maria. Hata hivyo, hakuna kitu chochote katika Biblia kinachoonyesha jambo hili.

Umri unaweza kuwa muhimu katika ndoa, lakini sio muhimu sana kuliko masuala mengine kama wokovu, ukomavu wa kiroho, utangamano, na mengine . Watu wanapozeeka, tofauti ya umri inakuwa maana kidogo. Kwa hakika, mwenye umri wa miaka 40 kuolewa na umri wa miaka 20 atazua maswali tofauti, wakati huohuo haitakuwa jambo la kushangaza wakati mtu wa umri wa miaka 80 akifunga ndoa mwenye umri wa miaka 60. Onyo pekee kuhusu umri katika ndoa ni kuepuka kuolewa na mtu mdogo kwa madhumuni ya kutamani, na kuepuka kuolewa na mtu mzee kwa sabau ya fedha. Njia bora ni kumwomba Mungu kwa hekima juu ya uhusiano wowote unaotarajiwa (Yakobo 1: 5).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu tofauti za umri katika mahusiano?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries