Swali
Je, Je, kuna tofauti gani kati ya urafiki wa kimapenzi na uchumba?
Jibu
urafiki wa kimapenzi na uchumba ni njia mbili za kuanza mahusiano na jinsia tofauti. Ingawa kuna wasiokuwa Wakristo ambao wanakuja na nia ya kuwa na mfululizo wa mahusiano ya kimwili, kwa Mkristo hii haikubaliki na haipaswi kamwe kuwa sababu ya urafiki wa kimapenzi kabla ya ndoa.Wakristo wengi wanaona kuwa urafiki wa kimapenzi ni zaidi ya urafiki na kudumisha uhusiano wa urafiki wao mpaka marafiki hao wanakua tayari kujitolea kama washirika kwa ndoa. Kwanza kabisa, urafiki wa kimapenzi kabla ya ndoa ni wakati ambapo Mkristo anapata kujua kama mchumba wake ni mwaminifu katika Kristo. Biblia inatuonya kwamba waumini na wasioamini hawapaswi kuoana, kwa sababu wale wanaoishi katika mwanga (wa Kristo) na wale wanaoishi katika giza hawawezi kuishi kwa umoja (2 Wakorintho 6: 14-15). Kama ilivyoelezwa hapo awali, wakati huu wapenzi hawapaswi kuwasiliana kimwili , kwa kuwa hii ni jambo ambalo linapaswa kusubiri mpaka ndoa (1 Wakorintho 6: 18-20).
Katika uchumba wahusika wawili hawawezi kuwasiliana kimwili wakati wote (hakuna kugusa, hakuna kushikilia mkono, hakuna kubusu) mpaka wakati wa ndoa. Wengi katika uchumba hawatumii wakati wowote pamoja isipokuwa machoni mwa familia, hasa wazazi, wakati wote. Kwa kuongeza, wapenzi wanaweka wazi nia yao ni kuoana ikiwa mwenzi ni mpenzi mzuri wa ndoa. uchumba unawezesha watu wawili kupata kujuana kwa upana bila kuweka shinikizo la urafiki wa kimwili au hisia zinazozidi mtazamo wao.
Kuna matatizo ya asili na mitindo yote miwili. Kwa wachumba, kutumia muda peke yao na mtu wa jinsia tofauti ambaye anayepata kuvutia inaweza kutoa majaribu ambayo inaweza kuwa ngumu sana kupinga. Wachumba wa Kikristo wanapaswa kuweka mipaka mahali na kujitolea kutovuka mipaka hio. Ikiwa wanaona kuwa ni vigumu kufanya hivyo, wanapaswa kuchukua hatua ili kuhakikisha kuwa Kristo ataheshimiwa wakati wote pamoja na kwamba dhambi haipati nafasi yoyote katika uhusiano wao. Kama ilivyo kwa wapezi wawili wa ndoa, wazazi wa wapenzi wa ndoa wanapaswa kushiriki katika uhusiano, kupata kujua rafiki wa mtoto wao na kuwa chanzo cha ushauri wenye hekima na ufahamu na mwongozo kwa wote wawili.
Mtindo wa uchumba huwa seti yake ya matatizo. Wakati wengi huona kuwa uchumba kuwa ni chaguo pekee la kutafuta mwenzi, wengine wanaipata kuwa ni ya kufinyilia na ya udhibiti mkubwa. Kwa kuongeza, inaweza kuwa vigumu kujua mtu "halisi" mbele ya umma au mbele ya familia nzima. Hakuna yeyote aliye sawa katika umma na vilevile mnaoshiriki moja kwa moja. Ikiwa wanandoa hawana wakati pamoja, wao hawapati kuwa na fursa ya moja kwa moja ya kuwasiliana na kujuana kwa hisia na kiroho. Kwa kuongeza, baadhi ya uchumba zimesababisha ndoa za mpangilio "zilizopangwa" na wazazi na zimesababisha hasira katika moja au wawili wa vijana wahusika.
Ni muhimu kukumbuka kuwa uhusiano wa kimapenzi au uchumba haujaamrishwa katika Maandiko. Mwishoni, tabia ya Kikristo na ukuaji wa kiroho wa wanandoa ni muhimu sana kuliko hali halisi ya jinsi wanavyotumia wakati pamoja . Kuzungumza kimaandiko, matokeo ya mchakato-wanaume na wanawake wa Kikristo wanaoona na kukuza familia kwa utukufu wa Mungu-ni muhimu zaidi kuliko njia wanayoyatumia ili kufikia matokeo hayo. "Kwa hiyo, ikiwa mna kula au kunywa, au chochote mnachofanya, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu" (1 Wakorintho 10:31).
Hatimaye, ni lazima tuwe makini ili kuepuka kuamini mapendekezo ya mtu binafsi kwamba urafiki wa kimapenzi au uchumba-ni "pekee njia" na kudharau wale wanaofanya uchaguzi tofauti. Biblia haijazungumzia mambo mawili haya lakini umoja wa mwili wa Kristo unapaswa kuwa muhimu sana katika akili zetu, bila kujali uchaguzi wa kibinafsi ambao wengine hufanya.
English
Je, Je, kuna tofauti gani kati ya urafiki wa kimapenzi na uchumba?