settings icon
share icon
Swali

Je! Ni nini maana ya tumaini lenye baraka?

Jibu


Tito 2:12-13 inasema kuwa neema ya Mungu hutufunza "Nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, ili tupate kuishi maisha ya kiasi, ya haki na ya utaua katika ulimwengu huu wa sasa, huku tukilitazamia tumaini lenye baraka na ufunuo wa utukufu wa Mungu wetu Mkuu, aliye Mwokozi wetu Yesu Kristo." Kifungu hiki kinaitambua "tumaini lenye baraka" kuwa ujio wa utukufu wa Yesu Kristo, Mungu wetu mkuu na Mwokozi.

Neno baraka linaweza maanisha "furaha" au "manufaa"; tumaini letu limebarikiwa kiasi kwamba kurudi kwa Yesu kutakuwa kwa ajabu, furaha kwa waumini wote katika Kristo. Tutabirikiwa kupita kiwango wakati tutakapomwona Kristo. Majaribu ya maisha haya yataisha, na tutaona kuwa "Nayahesabu mateso yetu ya wakati huu kuwa si kitu kulinganisha na utukufu utakaodhihirishwa kwetu" (Warumi 8:18). Neno tumaini haliwasilishi kutokuwa na uhakika, kama ilivyo katika msemo "Natumai kuwa kitu kinaweza kutokea"; badala yake, ni uhakikisho wa furaha kwamba kitu kitatokea. Yesu ndiye tumaini letu, na hakuna mtu yeyote anaweza kuchukua matumaini hilo. "wala tumaini halitukatishi tamaa, kwa sababu Mungu amekwisha kumimina pendo lake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ametupatia" (Warumi 5:5).

"Tumaini lenye baraka," basi, ni hakikisho la kufurahisha kwamba Mungu atapanua faida zake kwetu na kwamba Yesu Kristo atarudi. Tunasubiria hafla hii sasa. Yesu alisema atarudi (Yohana 14: 3), malaika walisema atarudi (Matendo 1:11), na barua zinasema atarudi. Yesu anaweza kurudi wakati wowote kulichukua kanisa Lake, ambalo linajumuisha waumini wote wa Kristo tangu Siku ya Pentekoste katika Matendo 2 na kuendelea. Tukio hili linaitwa unyakuzi. Utatangazwa na sauti ya malaika mkuu na sauti ya tarumbeta ya Mungu. Miili ya wale waliokufa itafufuliwa ili kuunganishwa na roho zao, na kisha miili ya wale waumini wanaoishi duniani itabadilishwa kuwa umbo kama mwili wa Bwana wati wa kufufuliwa. Waumini waliofufuliwa kutoka kwa wafu na waumini wanaoishi wakati wa kurudi kwa Kristo watakutana na Bwana mawinguni na kuchukuliwa mbinguni (taz. 1 Wathesalonike 4: 13-18). Hii itatokea kwa mpepeso wa jicho (1 Wakorintho 15:52).

Je! hili tumaini lenye baraka la kurudi kwa Yesu wakati wowote lina athari yeyote kwa muumini katika Yesu Kristo? Yohana aliandika, "Kila mmoja mwenye matumaini haya ndani yake hujitakasa, kama vile yeye alivyo mtakatifu" (1Yohana 3:3). Muumini anayetarajia ujio wa baraka wa Yesu atatafua kuishi katika maisha ya ujazo wa nguvu ya Roho Mtakatifu, maisha ya uadilifu. Sisi wote tutasimama mbele za Bwana na kutoa hesabu ya jinsi tulivyoishi kwa ajili yake hapa dunia (2 Wakorintho 5:10).

Ujio wa Yesu unapaswa kutia moyo muumini kuishi maisha ya kiungu huku duniani. Neno tazamia katika Tito 2:13 ndilo kuu kwa hilo kutokea. "Kutazamia" inamaanisha kwamba tuishi kila siku katika kutwaa na matarajio, na tukiwa na uhakika kuwa Yesu anaweza kurudi wakati wowote. Tumaini hilo linakuwa ukweli unaobadilisha katika maisha haya, na matokeo yake ni Mungu kutukuzwa kupitia kwetu (1 Wakorintho 10:31). tumaini lenye baraka hutuletea furaha na kutupa shangwe wakati wa majaribu ya ulimwengu huu. Pia linapaswa kutufanya kupumua na kulizwa fikira zetu, maneno, na matendo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni nini maana ya tumaini lenye baraka?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries