settings icon
share icon
Swali

Uadilifu wa Njia ya Vikundi Nane vya Waumini ni Nini?

Jibu


Uadilifu wa Njia ya Vikundi Nane vya Waumini ni harakati ya mazoezi ya mfuasi wa budha. Dhana nane zilizomo katika Uadilifu wa Njia ya Vikundi Nane vya Waumini ni mtazamo na tabia ambazo Wafuasi wa budha wanajitahidi kuiga kama njia ya kuishi Ukweli Nne Adilifu. Dhana hizi nane huanguka katika makundi matatu makuu: Hekima, Maadili mema, na Umakinifu. Kwa mujibu wa Ukweli Nne Adilifu, maisha yote yanayoteseka yamesababishwa na tamaa za vitu visivyo vya kudumu, na kwa kuwa vitu vyote si vya kudumu-hata yenyewe-- njia pekee ya kuwa huru kutokana na mateso ni kumwaga tamaa zote. Hii inafanywa, kulingana na Ubudha, kwa Njia Nane za Waumini zifutazo.

Ingawa inatwa "njia," sehemu hizi nane hazikusudiwi kufuatiliwa kwa utaratibu wowote maalumu. Badala yake, zinakusudiwa kufuatwa sawia, ili kuondoa tamaa na kufikia Nirvana. Njia ya Nane za Waumini, na Ubudha yenyewe, mara nyingi inawakilishwa na gurudumu nane, lililofanana na usukani wa meli ya matanga. Vipengele vya Uadilifu wa Njia ya Vikundi Nane vya Waumini ni mtazamo sahihi, nia njema, hotuba sahihi, tabia sahihi, maisha sahihi, jitihada sahihi, ufahamu sahihi, na tafakuri sahihi.

Vipengele vya mtazamo sahihi na nia nzuri wakati mwingine hujulikana kama mambo ya hekima ya Uadilifu wa Njia ya Vikundi Nane vya Waumini.

"Mtazamo sahii" kimsingi inamaanisha kuamini katika Ukweli Nne Adilifu: kwamba maisha ni mateso; mateso husababishwa na kutamani mambo ya muda; kila kitu ni cha muda; na tu kwa kufuata njia nane za waumini kunaweza kuondoa tamaa zote. Pia ni inajumuhisha ufahamu wa dhana kama vile kuzaliwa upya (kuzaliwa upya kiroho katika mwili mwingine) na sheria ya karma. Kibiblia, ni kweli kwamba mtu lazima awe chini ya ukweli fulani ili apate kuokolewa (Yohana 8:32), lakini Biblia inakataa kwamba ujuzi maalumu kwa namna fulani sehemu ya kazi ya wokovu wa mtu (Waefeso 2:8, 1 Wakorintho 3:19).

"Nia njema" inamaanisha nia ya kubadilika kwa wema, kwa mujibu wa Ukweli Adilifu na Njia Nane za Waumini. Mtu mwenye nia njema amejitolea kwa maagizo ya Ubudha na anajaribu kulinganisha mawazo na tabia zake nayo. Kibiblia, waumini wanaitwa kulinganisha imani na matendo yao kwa viwango vya Kristo (2 Wakorintho 13:5; Warumi 13:14; Yohana 15:14). Hata hivyo, Biblia pia inakubali kwamba kile mtu anataka, moyoni, sio kila wakati anapaswa kutaka (Yeremia 17:9). Ubudha haitoi jibu kwa jinsi mtu anapaswa kubadilisha tamaa zake za ndani ili kupata kuelimika (angalia 2 Wakorintho 10:12).

Vipengele vya hotuba sahihi, tabia sahihi, na maisha sahihi wakati mwingine hujulikana kama mambo ya kimaadili ya Uadilifu wa Njia ya Vikundi Nane vya Waumini.

"Hotuba sahihi" inahusu kutumia maneno kwa uaminifu, kwa upole, na kwa makusudio. Hii ina maana ya kuepuka uvumi, uongo, au hotuba ya maneno ya matusi. Hotuba sahihi hutumiwa kwa maneno yaliyoandikwa kama vile yaliyosemwa. Athari moja ya kuvutia ya njia ya mfuasi wa Budha kwa hotuba sahihi ni kuepuka majadiliano ya mada fulani ya kiroho au ya udhanifu. Kwa mujibu wa Ubudha, baadhi ya maswali ya ukweli halisi hayana maana ya mmoja kufuata Njia ya Vikundi Nane vya Waumini, hivyo kuzijadili sio "hotuba sahihi." Kibiblia, tunaambiwa kuendeleza udhibiti wa maneno yetu (Mithali 10:19) na kuepuka migogoro isio na maana (1 Timotheo 6:4).

"Tabia sahihi" inajumuhisha kuepuka vitendo kama vile mauaji, wizi, uzinzi, na kadhalika. Kanuni ya jumla inayoongoza kile kilicho sawa dhidi ya kile ambacho si sahihi ni ikiwa tendo litaleta madhara kwa mtu mwingine au la. Bila shaka, Biblia inatoa njia ngumu kwa maadili ya tabia (Mathayo 7:12, 1 Wakorintho 9:27), kuchanganya tabia na mtazamo chini ya njia moja ya uadilifu na maadili (Mathayo 5:21-22, 27-28). Kiwango cha Biblia cha haki dhidi ya kinyume ni mwisho sio ikiwa huleta madhara kwa mtu mwingine lakini ikiwa inakiuka asili takatifu ya Mungu.

"Maisha sahihi" ni sawa na tabia sahihi, lakini inalenga hasa kazi ya mtu. Kwa mujibu wa kanuni hii, mtu hapaswi kudanganya, kusema uwongo, au kushiriki katika biashara ambazo huwadhuru au kuwadhulumu watu. Kwa sababu ya mbinu za mfuasi wa Budha kwa maisha ya wanyama na vurugu, sheria hii inazuia kazi yoyote inayohusisha kuchinjwa kwa wanyama, kuuza nyama, au kutengeneza au kuuza silaha. Kwa mujibu wa Biblia, mtu anapaswa kushughulikia sehemu zote za maisha yake, ikiwa ni pamoja na biashara, na wasiwasi sawa wa uadilifu na kimaadili (Zaburi 44:21, Warumi 2:16; 2 Wakorintho 4:2). Mungu anatutarajia pia kuwa watumishi wazuri wa asili (Mambo ya Walawi 19:25; 25:2-5, Habakuki 2:8, 17). Hata hivyo, Biblia haizuii matumizi ya wanyama (Marko 7:19, Mwanzo 1:28) au njia halali za kujitetea (Luka 22:36).

Vipengele vya jitihada sahihi, ufahamu sahihi, na tafakuri sahihi wakati mwingine hujulikana kama masuala ya umakinifu ya Uadialifu wa Njia ya Vikundi Nane vya Waumini.

"Jitihada sahihi" inahitaji hisia ya kuendelea na tahadhari katika kutumia mambo mengine ya Njia ya Vikundi Nane vya Waumini. Inamaanisha uendeshaji ili kuepuka kufikiri bila rajua na hisia hasi kama vile hasira. Mara nyingine tena, hii inaonyesha tatizo kwamba asili ya mwanadamu inajitokeza kuwa binafsi na vivu. Ubudha hautoi njia maalumu ya kubadili mambo hayo kwa mtu ambaye hana mwelekeo wa kubadili. Biblia inasema juu ya nia ya Mungu na uwezo wa kubadilisha moyo, hata wakati sisi ni kinzani (2 Wathesalonike 3:13; 1 Wakorintho 6:11).

"Ufahamu sahihi" ni sawa na jitihada sahihi lakini inazingatia zaidi juu ya mambo ya ndani ya akili na falsafa. Ubudha unahimiza ngazi ya juu ya kujitambua, na tahadhari maalumu iliyotolewa kwa jinsi mtu anavyoitikia kwa uzoefu na mazingira yake. Aina hii ya uzingatifu umewekwa msingi juu ya sasa, na msisitizo mdogo juu ya siku za nyuma au za baadaye. Kibiblia, sisi pia tunatakiwa kulinda mawazo yetu na kuwa makini jinsi mazingira yetu yanavyoathiri maisha yetu ya kiroho (1 Wakorintho 15:33; 6:12).

"Tafakuri sahihi" ni mazoezi ya msingi ya Ubudha, yanayohusisha kupumua, kuimba, na mbinu nyingine za kuzingatia. Lengo la mtindo huu wa kutafakuri ni kufuta akili kabisa ya kila kitu lakini kitu cha ukolezi. Onyesho la mwisho la fomu hii ya tafakuri ni samadhi, wakati mtu anaendelea kupitia viwango mbalimbali vya kutafakari hadi atakapokuwa na hali kamili isiyo na utambuzi na isiyo na hisia. Hii inawakilisha mgogoro mwingine na mafundisho ya kibiblia. Biblia inaunga mkono wazo la kutafakuri na kuakisi (Zaburi 1:2, 119:15) lakini si kwa lengo la "kuondoa" akili. Badala yake, lengo la kutafakuri wa Kikristo ni kuzingatia ukweli wa Neno la Mungu. Kibiblia, kutafakuri ni kujaza akili na Neno la Mungu lililofunuliwa.

Kwa muhtasari, kuna baadhi ya mambo ya makubaliano kati ya Ukristo wa kibiblia na Uadilifu wa Njia ya Vikundi Nane vya Waumini wa Kibudha. Hata hivyo, tofauti nyingi ni za msingi na zisizopanishwa. Kulingana na Njia ya Vikundi Nane vya Waumini, mtu ambaye hawezi kujisaidia kutimiza mambo yote hawezi tu kufuata njia. Chaguo lake la pekee ni kutumaini kwamba tamaa zake, malengo yake, na jitihada zake kubadilika wenyewe. Biblia inaelezea kwamba moyo wa mtu hauwezi kuaminika kutafuta mema ndani na yenyewe (Yeremia 17:9; Warumi 3:10-12; 7:18-24), lakini moyo wowote unaweza kubadilishwa kupitia uhusiano na Kristo (Warumi 7:25; Wagalatia 3:13).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Uadilifu wa Njia ya Vikundi Nane vya Waumini ni Nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries