Swali
Je! Kutakuwa na uasi mkuu/kuanguka wakati wa kipindi cha nyakati za mwisho?
Jibu
Biblia inaonyesha kwamba kutakuwa uasi mkuu wakati wa kipindi cha nyakati za mwisho. "uasi huu mkuu" umetajwa katika 2 Wathesaloniki 2:3. Uasi ni kukaidi, kukataa ukweli. Nyakati za mwisho zitajumuisha katalio la ufunuo wote wa Mungu, ambayo ni "mwanguko zaidi" wa dunia ambayo bado imeshaanguka.
Tukio la wakati Paulo anawaandikia Wathesaloniki ilikuwa kurekebisha baadhi ya makosa kuhusu nyakati za mwisho ambayo kwayo waumini walikuwa wamekwisha sikia kutoka kwa walimu wa uwongo. Miongoni mwa uwongo ilikuwa ni "kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwako" (2 Wathesalonike 2:2). Wakristo katika Thesalonike walikuwa na woga kwamba Yesu alikuwa amekwisha kuja, na walikuwa wamekosa unyakuzi, na sasa walikuwa katika kipindi cha dhiki. Paulo alikuwa amekwisha waelezea juu ya unyakuzi katika barua yake ya (1 Wathesalonike 4:16-17). Paulo anaandika barua yake ya pili kuwahakikishia kwamba, kinyume na kile walikuwa wamekwisha sikia, na mbali na mateso waliyokuwa wakistahimili, "siku ya Bwana" haikuwa imekuja.
Katika 2 Wathesalonike 2:3, Paulo anaiweka wazi kwamba siku ya Bwana, wakati wa hukumu wa dunia yote (Isaya 13:6; Obadia 1:15), haiwezi fanyika hadi mambo mawili yatokee. Kwanza, kuanguka, au uasi mkuu, lazima utokee. Pili, "mtu mwasi sheria" lazima adhihirishwe, ambaye anaitwa "mwana wa upotevu," ambaye pia anaitwa Mpinga Kristo. Pindi mtu huyu atajitambulisha mwenyewe, nyakati za mwisho hakika zitakuwa zimekuja. Kuna kisio nyingi juu ya utambulisho wa mtu wa dhambi, kuanzia karne ya kwanza kisio hizo zinajumuisha Caligula, Caius Caesar, Mohammed, Napoleon na idadi yoyote ya mapapa wa Kirumi. Hakuna hata mmoja wao alikuwa Mpinga Kristo.
Mtu mwasi sheria kulingana na 2 Wathesalonike 2:4, ni yule mmoja ambaye ni "Yeye atapingana na kujitukuza juu ya kila kitu kiitwacho Mungu au kinachoabudiwa, ili kujiweka juu katika Hekalu la Mungu, akijitangaza mwenyewe kuwa ndiye Mungu." Ni wazi kuwa hii haijatokea; hakuna mtu yeyote tangu enzi za Paulo amejizimamisha kama Mungu katika hekalu ya Kiyahudi. Miaka elfu mbili imepita tangu nyaraka hii iliandikwa, na "siku ya Bwana" bado haijakuja. Paulo anatuhakikishia kuwa siku hiyo haitakuja hadi kuanguka kuje kwanza.
Neno la Kiyunani lilitafsiriwa "uasi" au "kuanguka" katika aya ya 3 ni apostasia. Linarejelea kuasi kwa kawaida kutoka kwa Mungu wa kweli, Biblia, na imani ya Kikristo. Kila kizazi kina waasi wake, lakini kuanguka katika nyakati za mwisho utakamilika na utakuwa katika ulimwengu kote. Sayari yote itaasi dhidi yake Mungu na Kristo. Kila upinduzi unahitaji kiongozi, na kwa uasi huu wa kiulimwengu atainuka Mpinga Kristo. Tunaamini kuwa hii itatokea baada ya kanisa limekwisha nyakuliwa kutoka duniani.
Yesu aliwaonya wanafunzi kuhusu siku ya mwisho katika Mathayo 24:10-12: "Wakati huo, wengi wataacha imani yao, nao watasalitiana kila mmoja na mwenzake na kuchukiana. Watatokea manabii wengi wa uongo, nao watawadanganya watu wengi. Kwa sababu ya kuongezeka kwa uovu upendo wa watu wengi utapoa." Hizi ndizo dalili za uasi mkuu katika nyakati za mwisho.
English
Je! Kutakuwa na uasi mkuu/kuanguka wakati wa kipindi cha nyakati za mwisho?