settings icon
share icon
Swali

Ikiwa mtu anataka kubatizwa, lakini hawezi kutumbukizwa kwa maji kwa sababu ya kuwa mgonjwa, kilema, mzee sana nakadhalika-ni nini inafaa kufanywa?

Jibu


Pengine njia bora ya kushughulikia swali hili ni kuanza na ubatizo wenyewe- kile ubatizo ulicho na kile hauko. Ubatizo wa Kikristo kulingana na Biblia ni ushuhuda wa nje wa kile kimekwisha tendeka ndani ya maisha ya muumini. Ni taswira ya muumini kujitambulisha na kifo, kuzikwa na kufufuka kwa Yesu Kristo. Warumi 6:3-4 inaelezea tendo hili kuwa nafsi yetu ya kale ya dhambi imezikwa pamoja na Kristo na utu wetu upya umefufuliwa kutembea Naye katika maisha mapya.

Ubatizo sio sharti la wokovu, wala hauna nguvu yoyote ya kuokoa. Badala yake, ni ishara ya wokovu ambayo tayari imekwisha fanyika. Tunabatizwa ili tuonyeshe wengine ukweli huo, ambayo ndiyo sababu batizo nyingi zinaambatanishwa na kukiri kwa mdomo kuliotolewa na mtu anayebatizwa. Ni ushuhuda ambao ndio sehemu muhimu zaidi ya kawaida ya dini, sio ibada yenyewe.

Huku Biblia ikiwa wazi kuwa kutumbukizwa ndioi njia bora ya kubatizwa, hamna mahali Biblia inasungumzia juu ya kile tutafanya mahali ambapo mtu anastahili kubatizwa lakini hawezi kutumbukizwa kwa maji. Baadhi hupendekeza ubatizo wa kunyunyuzia au kumwagia maji. Huku kunyunyuzia na kumwagia hakuambatani na kile ubatizo unaashiria-kifo, kuzikwa na kufufuka kwake Yesu Kristo-hakika kunazo hali zingine ambapo kutumbukiza halisi hakuwezi fanyika. Mtu ambaye hawezi kubatizwa kwa kutumbukizwa anapaswa aende mbele cha kikundi cha waumini na kukiri hadharani kuwa imani katika Yesu Kristo pekee ndio inaokoa, kujitolea kwake, na kujitambulisha naye. Hiyo itakamilisha kile ubatizo unamaanisha.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ikiwa mtu anataka kubatizwa, lakini hawezi kutumbukizwa kwa maji kwa sababu ya kuwa mgonjwa, kilema, mzee sana nakadhalika-ni nini inafaa kufanywa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries