Swali
Kwa nini ubikira ni muhimu sana katika Biblia?
Jibu
Wakati Biblia inatumia neno bikira, linamaanisha mtu asiyeolewa ambaye hajakuwa na mahusiano ya ngono (angalia Esta 2: 2 na Ufunuo 14: 4). Katika utamaduni wa leo, watu wengi hutumia neno ubikira kuelezea kutojihusisha na ngono; hata hivyo, wengine hutumia ufafanuzi wa neno hilo kupata vigezo vya viwango vya maadili, na kupunguza maana ya neno kuwa "hali ya kutofanya ngono kikamilifu" — basi wapenzi wanaweza kujihusisha katika ngono isiyo kamilifu na bado kusema wao ni "bikira." Huu ni mchezo wa neno ambao haufai. Utakaso unapaswa kuathiri moyo, akili, na nafsi, si tu sehemu fulani za mwili.
Msisitizo wa Biblia sio juu ya ufafanuzi wa kina wa bikira kama ilivyo katika hali ya moyo wa mtu. Maadili tunayotaka na matendo tunayochagua yanatoa ushahidi wa hali ya moyo wetu. Kiwango cha Biblia ni wazi: kuepuka ngono kabla ya ndoa na kuoa mke/mume mmoja.
Kuna sababu tatu kubwa za kuepuka ngono hadi wakati wa ndoa. Kwanza, kama waumini, tunapaswa kutii kile ambacho Mungu anatuambia kufanya. Wakorintho wa Kwanza 6: 18-20 inasema, "Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu."Ikiwa tumo ndani ya Kristo, ametukomboa kwa dhabihu ya maisha yake. Yeye ni Bwana wetu na sisi tunamheshimu Yeye.
Sababu ya pili ni kwamba tunapaswa kupigana vita vyetu vya kiroho huku tukivaa dirii ya haki kifuani (Waefeso 6:14). Tuko katika mashindano kati ya asili yetu mpya katika Kristo na tamaa zetu za kimwili. Wathesalonike wa kwanza 4: 3-7 inasema, "Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.
Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana. Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso." Kuruhusu mwili wako (badala ya Roho) kudhibiti vitendo vyako ni kitendo cha kukiuka amri ya Mungu. Ngono ya kimungu na upendo kati ya mume na mke haina ubinafsi. Kutumia mtu ili kutimiza tamaa ya mwili ni ubinafsi na kudhalilisha. Hata kama mpenzi wako amekubaliana na tendo hilo, bado unamsaidia kufanya dhambi na kuharibu uhusiano wa mtu huyo na Mungu na watu wengine.
Sababu ya mwisho inahusisha "siri" ya ndoa (Waefeso 5: 31-32). Wakati Mungu alizungumza kuhusu watu wawili kuungana kuwa kama mmoja, alikuwa akimaanisha kitu tunachoanza tu kuelewa kwa njia halisi, ya kisaikolojia. Wakati watu wawili wanakuwa na uhusiano wa karibu, katika ubongo hutoka kemikali ambazo zinafanya hisia za kushikamana na imani. Kuhusika kwa ngono nje ya ndoa husababisha huba na kuwa na Imani kwa mtu ambaye yeye hana uhusiano wa kujitolea. Ufafanuzi wa neno kuamini katika akili huharibika. Kuwa na uhusiano huo na mtu bila uhakika wa kufanya kazi pamoja kwa Mungu ni hatari. Watu wawili ambao-wameshikiliana kisaikolojia lakini hawana nia ya kukua katika Mungu kama wanandoa inawezakana kusonga mbali na Mungu na mipango yake kwa ajili yao.
Kinyume chake, kama watu wawili wanafanya uamuzi, kwa makusudi kujipeana kwa kila mmoja katika ndoa, na kisha kuruhusu urafiki unaosababisha kemikali hizi, mwili unaweza kuthibitisha uhusiano ambao akili imeufanya. Hisia za kisaikolojia za uaminifu na vifungo zinaimarishwa na ukweli wa uhusiano huo. Kwa njia hii, watu wawili huwa mmoja kimwili, na hilo linaonyesha kile Mungu amefanya kiroho.
Ndoa ni mfano wa uhusiano kati ya kanisa na Kristo. Wanandoa ni kumtumikia Mungu kwa ushirikiano wenye nguvu na umoja. Ngono, pamoja na kuzaa, iliundwa na Mungu ili kuimarisha ushirikiano huo. Ngono nje ya ndoa hujenga vifungo vinavyovunja mioyo ya watu badala ya kuiunganisha pamoja.
Hatimaye, tunahitaji kukumbuka mambo machache kuhusu ubikira, na ukosefu wake, kutokana neema ya Mungu. Wale wanaokuja kwa Kristo baada ya kujihusisha na mahusiano ya ngono kabla ya ndoa sio wabikira; hata hivyo, wao husafishwa kikamilifu na Kristo wakati wanaokolewa. Mungu anaweza kumkomboa mtu yeyote, na anaweza kuwaponya wale ambao wajuhusisha kwa tamaa zao za kimwili. Kwa wale ambao walifanya ngono baada ya kuwa wakristo, kuna msamaha katika Kristo. Anaweza kututakasa kutoka kwa udhalimu wote na kuleta uponyaji (1 Yohana 1: 9). Na, katika hali mbaya ya mtu aliyeathiriwa na unyanyasaji wa kimapenzi au ubakaji, ambaye anaweza kuhisi kuwa yeye hapati tena kiwango kizuri cha "ubikira, ingawa sio kosa lao wenyewe, ," Kristo anaweza kurejesha roho yake, kumponya na kumpa uzima.
English
Kwa nini ubikira ni muhimu sana katika Biblia?