settings icon
share icon
Swali

Bibilia inasema nini kuhusu uchumba?

Jibu


Ingawa neno “uchumba” halipatikani katika Bibilia, tumepewa kanuni kwamba Wakristo wanastahili kupitia kabla ya ndoa. Kanuni ya kwanza ni kwamba ni lazima tutafautishe mtazamo wa dunia kuhusu uchumba kwa sababu mtazamo wa Mungu wahitilafiana na ule wa dunia (2 Petero 2:20). Huku ikiwa mtazamo wa dunia juu ya uchumba huenda usiwe na jinsi tunavyo taka, cha muimu ni kutambua tabia ya mtu kabla tufanye ahadi naye. Lazima tujue ikiwa huyu mtu ameokoka katika roho wa kristo (Yohana 3:3-8) na kama huyo mtu ako na nia ile kama ya kristo (Wafilipi 2:5). Lengo kuu la uchumba ni kumtafuta mpenzi wa maisha. Bibilia inatuambia kwamba, kama Wakristo tusioe wasio Wakristo (2 Wakorintho 6:14-15) kwa sababu hii itafanya uhusiano wetu na Kristo na tuaibishe tabia zetu na kanuni zetu ziwe hafifu.

Wakati mtu amejitoa kw uhusiano, hata kama ni wa uchumba, ni muimu kukumbuka kumpenda Mungu kuliko vitu vyote (Mathayo 10:37). Kusema au kuamini kuwa mtu mwingine ni “vitu vyote” au kitu cha maana katika maisha ni kuabudu sanamu, ambayo ni dhambi (Wagalatia 5:20; Wakolosai 3:5). Pia hatustahili kuichafua miili yetu kwa kufanya usherati (1 Wakorontho 6:9, 13; 2 Timotheo 2:22). Dhambi ya usherati sio dhambi kwa mwili pekee bali ni kinyume na Mungu (1 Wakorintho 6:18). Ni muimu kuwaeshimu na kuwachukulia kuwa watu wa heshima vile tunavyojipenda wenyewe (Warumi 12:9-10). Na hii ni kweli kwa uhusiano wa uchumba. Hata kama mnachumbiana, kuifuata kanuni hii ndio njia nzuri kuwa na msingi salama wa ndoa. Mojawapo ya maamuzi tutakayofanya, kwa sababu wakati watu wawili wanaoana, hushikana na kuwa mwili mmoja kwa uhusiano ambao Mungu anaunuia uwe wa kudumu na usiovunjika (Mwanzo 2:24; Mathayo 19:5).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Bibilia inasema nini kuhusu uchumba?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries