Swali
Ufafanuzi wa uovu ni upi?
Jibu
Uovu kwa kawaida hufikiriwa kuwa kile ambacho kimaadili ni kibaya, dhambi, au uasi; ijapokuwa, neno uovu linaweza pia rejelea kitu chochote abacho husababisha madhara, kiwe au kisiwe na mwelekeo wa maadili. Neno hilo limetumika njia zote mbili katika Biblia. Chochote kinachopingana na tabia takatifu ya Mungu ni uovu (soma Zaburi 51:4). Kwa upande mwingine, mkasa wowote, ajali, au msiba unaweza kuitwa “uovu” (tazama 1 Wafalme 17:20).
Tabia za uovu ni pamoja na dhambi iliyotendwa dhidi ya watu wengine (mauaji, wizi, uzinzi) na uovu uliofanywa dhidi ya Mungu ni (kutoamini, kuabudu sanamu, kukufuru). Kuanzia uasi katika Bustani mwa Edeni (Mwanzo 2:9) hadi uovu wa Babeli Kuu (Ufunuo 18:2), Biblia inazungumza juu ya dhana ya dhambi, na mwanadamu anajukumika kwa kila uovu anoutenda: “Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa” (Ezekieli 18:20).
Kimsingi, uovu ni ukosefu wa wema. Uovu si kitu cha kimwili; ni ukosefu au kunyimwa kitu kizuri. Kama vile Mkristo mwanafalsafa J. P. Moreland alivyosema, “Uovu ni ukosefu wa wema. Ni wema uliharibiwa. Unaweza kuwa na wema bila uovu, lakini hauwezi kuwa na uovu bila wema.” Au kama vile mtetezi wa Ukristo Greg Koukl alivyosema, “Uhuru wa mwanadamu ulitumiwa katika njia ya kudunisha wema katika ulimwengu, na upungufu huo, kwamba ukosefu wa wema, ndio tunaita uovu.”
Mungu ni upendo (1 Yohana 4;8); ukosefu wa upendo ndani ya mtu ni jambo lisilo la kiungu na kwa hivyo ni uovu. Na ukosefu wa upendo unajidhihirisha wenyewe katika njia isiyo ya upendo. Kauli hiyo hiyo inaweza tumika katika neema ya Mungu, haki, uvumilivu n.k. Ukosefu wa sifa hizi za kiungu kwa mtu yeyote hufanyiza uovu. Uovu huo basi hujidhihirisha katika tabia isiyo ya huruma, isiyo ya haki, isiyo na subira, n.k. inayoleta madhara zaidi katika ulimwengu mzuri ambao Mungu ameufanya. Hakika, tumepungukiwa sana: “Kama ilivyoandikwa: “Hakuna mwenye haki, hakuna hata mmoja” (Warumi 3:10).
Uovu wa kimaadili ni ubaya uliotendewa wengine, na unaweza kuwepo hata bila kuambatanishwa hatua za nje. Mauaji ni tendo la uovu, lakini huanza na uovu wa maadili wa chuki moyoni (Mathayo 5:21-22). Kufanya uzinzi ni uovu, vile vile uovu wa maadili wa moyo wenye tamaa (Mathayo 5:27-28). Yesu alisema, “Akaendelea kusema, “Kile kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matukano, kiburi na upumbavu. Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi” (Marko 7:20-23).
Wale wanaoanguka katika mienendo ya uovu huwa wanaanza polepole. Paulo anaonyesha jinsi mtu anavyoendelea popepole hadi kwa uovu sugu katika Warumi 1. Huwa inaanza na kukataa kumtukuza Mungu au kumshukuru (Warumi 1:21), na huishia na Mungu kuwapeana kwa “mawazo yao potovu” na kuwaruhusu “kujawa na udhalimu wa kila namna” (mistari ya 28-29).
Wale wanaotenda mouvu wako katika mtego wa Shetani na wao ni watumwa wa dhambi: “Inampasa kuwaonya kwa upole wale wanaopingana naye, kwa matumaini kwamba Mungu atawajalia kutubu na kujua kweli, ili fahamu zao ziwarudie tena, nao waponyoke katika mtego wa ibilisi ambaye amewateka wapate kufanya mapenzi yake” (2 Timotheo 2:25-26; ona pia Yohana 8:34). Ni kwa neema ya Mungu pekee tunaweza kuwekwa huru.
Uovu wa kimwili ni shida inayowapata watu duniani, na inaweza kuhusishwa au kutohusishwa na uovu wa maadili au hukumu ya Mungu. Mhubiri 11:2 inatushauri kuwa uwekezaji wetu uwe sehemu mbalimbali, kwa sababu hii: “hujui ni baa gani litakalokuwa juu ya nchi.” Neno uovu katika kisa hiki linamaanisha “mkasa,” “bahati mbaya,” au “janga,” hivyo ndivyo tafsiri zingine zinavyolitaja. Wakati mwingine, uovu wa kimwili ni matokeo ya ajali au sababu zisizojulikana, bila sababu ya maadili inayojulikana; mifano hii inajumuisha majeraha, ajali za gari, vimbunga na mitetemeko ya ardhi. Wakati mwingine mouvu ya kimwili ni malipo ya Mungu kwa ajili ya dhambi za mtu binafsi au kikundi. Sodoma na miji iliyoizunguka iliharibiwa kwa ajili ya dhambi zao (Mwanzo 19), na Mungu, “kuifanya kuwa kielelezo kwa yale yatakayowapata wale wasiomcha Mungu” (2 Petro 2:6). Mara nyingi, Mungu aliwaonya Israeli dhidi ya majanga ambayo yangewatokea ikiwa wangeasi: “Hata hivyo yeye pia ana hekima na anaweza kuleta maafa, wala hayatangui maneno yake. Yeye atainuka dhidi ya nyumba ya mwovu, dhidi ya wale ambao huwasaidia watenda mabaya” (Isaya 31:2). Katika hali zote, Mungu hufanya kazi kupitia hali hiyo ili kuleta makusudi Yake mema (Warumi 8:28).
Mungu siye mwanzilishi wa maadili maovu, badala yake ni utakatifu Wake ndio unaoufafanua. Tumeumbwa katika mfano wa Mungu, tuna jukumu la kufanya uamuzi wa kimaadili ambao unamfurahisha Mungu na unaoambatana na mapenzi Yake. Yeye ndiye anaruhusu utakaso wetu (1 Wathesalonike 4:3) na hataki tutende dhambi (Yakobo 1:13). Katika toba na imani katika Kristo, tuko na msamaha wa dhambi na urejesho wa maadili mema ndani yetu (Matendo 3:19). Kama watoto wa Mungu, tunatembea kulingana na amri hii: “Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema” (Warumi 12:21).
English
Ufafanuzi wa uovu ni upi?