settings icon
share icon
Swali

Je, onyo la Ufunuo 22: 18-19 linahusu Biblia nzima au kitabu cha Ufunuo tu?

Jibu


Ufunuo 22: 18-19 ina onyo kwa mtu yeyote anayeharibu maandiko ya kibiblia: "Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki." Je! Mistari hii inahusu Biblia nzima au tu kitabu cha Ufunuo?

Onyo hili limetolewa hasa kwa wale wanaopotosha ujumbe wa kitabu cha Ufunuo. Yesu mwenyewe ndiye mwandishi wa Ufunuo na mtoaji wa maono kwa Mtume Yohana (Ufunuo 1: 1). Kwa hivyo, Yeye anahitimisha kitabu kwa kuthibitisha mwisho wa unabii. Haya ni maneno Yake, na anaonya dhidi ya kuyapotosha kwa njia yoyote, iwe kwa njia ya nyongeza, uondoaji, uhaini, mabadiliko, au tafsiri isiofaa kwa makusudi. Onyo ni dhahiri na linalofaa. Mapigo ya Ufunuo yatatembelewa juu ya mtu yeyote aliye na hatia ya kuharibu mafunuo katika kitabu, na wale wanaofanya hivyo hawana sehemu ya uzima wa milele mbinguni.

Ijapokuwa onyo la Ufunuo 22: 18-19 linaelezea kitabu cha Ufunuo, kanuni inayofuata inahusu mtu yeyote ambaye hupotoza Neno la Mungu kwa makusudi. Musa alitoa onyo sawa katika Kumbukumbu la Torati 4: 1-2, ambako aliwaonya Waisraeli kuisikiliza na kutii amri za Bwana, wala kuongezea au kuondoa kutoka Neno Lake. Mithali 30: 5-6 ina mwongozo sawa kwa mtu yeyote ambaye angeongeza maneno kwa Neno la Mungu: atashutumiwa na kuthibitishwa kuwa mwongo. Ingawa onyo la Ufunuo 22: 18-19 linahusisha hasa kitabu cha Ufunuo, kanuni yake inapaswa kutumika kwa Neno lote la Mungu. Lazima tuwe makini kushughulikia Biblia kwa uangalifu na heshima ili tisipotoshe ujumbe wake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, onyo la Ufunuo 22: 18-19 linahusu Biblia nzima au kitabu cha Ufunuo tu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries