Swali
Je, uinjilisti ni nini?
Jibu
Uinjilisti ni neno pana kwa kiasi fulani ambalo linalotumika kuelezea harakati ndani ya Kiprotestanti ambalo linaelezea sifa kwa mkazo wa kuwa na uhusiano wa kibinafsi na Yesu Kristo. Uhusiano huu huanza wakati mtu anapokea msamaha wa Kristo na kuzaliwa tena kiroho. Wale ambao wanadhani kwa imani hii wanaitwa wainjilisti.
Neno la uinjilisti linatokana na maneno ya Kiyunani euangelion, ambalo inamaanisha "habari njema," na euangelizomai, ambalo lina maana "kutangaza kama habari njema." Habari njema hii ni kwamba "ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo Maandiko; nay a kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo Maandiko; na ya kuwa alimtokea Petro; tena na wale Thenashara" (1 Wakorintho 15:3b-5). Habari njema hii, ambayo ni injili ya Kristo, na kuhubiriwa kwake ndio msingi wa uinjilisti.
Mizizi ya uinjilisti hurudi nyuma ya Mageuzo ya Kiprotestanti, wakati ambapo Biblia ililetwa kwa umma. Ukweli wa kibiblia uliopuuzwa awali ulitambuliwa tena na kufundishwa. Haikuwa mpaka ufufuo mkubwa wa karne ya 18 na 19 huko Ulaya na Marekani, ingawa, uinjilisti huo ulianza kweli kama harakati. Kama ilivyotokea wakati wa Mageuzo, harakati ya kiinjilisti na lengo lake la kuwa na uhusiano wa kibinafsi na Yesu Kristo ulileta nguvu mpya katika kutafsiri na kutumia neno la Mungu kwa usahihi. Hii imebebwa hadi leo, ingawa neno limekuja kutumiwa vibaya na matumizi mabaya.
Kijadi, uinjilisti umekuwa ukilinda kiteolojia. Hii imekuwa tofauti kidogo, hata hivyo. Matumizi ya sasa ya neno hayawezi tena kuwa Wakristo halisi waliookoka, wala kwa wale wanaofikiriwa kuwa wahifadhi au wafuasi wa misingi ya kale. Kwa kweli, baadhi hulinganisha tu uinjilisti na Uprotestanti wenyewe, ukarimu au vinginevyo. Kwa kusikitisha, uinjilisti sasa mara nyingi unawekwa sawa na siasa za kuhifadhi. Wakati mtazamo wa kidunia wa kiijilisti wa Kikristo utasababisha mara kwa mara mtazamo wa kuhifadhi kisiasa, siasa sio lengo la uinjilisti wa kweli.
Hivyo, ufafanuzi wa uinjilisti unatofautiana machoni mwa ulimwengu. Moyo wa kweli wa uinjilisti, ingawa, ni katika kutangaza ujumbe wa injili katika neno na matendo yote. Kwa Mkristo wa kiinjilisti, hakuna wito mkubwa kuliko kuishi na kushiriki ujumbe huu na ukweli wa upendo wa Mungu.
English
Je, uinjilisti ni nini?