Swali
Biblia inasema nini kuhusu ujumbe kwa ulimwengu?
Jibu
Biblia haitumii maneno 'ujumbe kwa ulimwengu' bali Mungu ana fikra za ujumbe wa ulimwengu(Luka 19:10), na mapenzi yake yanaenea ulimwenguni kote (Yohana 3;16). Wokovu wa mataifa yote ni jukumu la kila mkiristo kulingana na angalau sababu tatu kwenye maandiko:
Kwanza, ujumbe kwa ulimwengu ni muhimu kwa sababu Mungu ndiye muumba wa kila mtu; pili, Mungu anajali watu wote bila ubaguzi na tatu, Mungu anatarajia watu wote wapate wokovu na wapate hekima ya ukweli kumhusu Yesu Kristo (1 Timotheo 2:4). Kwa sababu ya mtazamo wa Mungu kwa watu wa ulimwengu, tunajua kuwa ujumbe kwa ulimwengu yani kupeleka injili kwa kila mtu ulimwenguni ni lengo la muhimu sana. Mungu alimtuma Mwana wake ulimwenguni ili atimize unabii huu: "Watu wanaotembea katika giza wameona nuru kuu, wale wanaoishi katika nchi ya uvuli wa mauti, nuru imewazukia" (Isaya 9:2).
Ujumbe kwa ulimwengu uko na msingi kwa ile amri Yesu alipea wanafunzi wake kuwa waende wakafanye 'wanafunzi wa mataifa yote' (Mathayo 28:19). Hili ndilo jukumu wanafunzi wanajitahidi kufanya. Uko Usamaria Antioki, Paulo na Baranaba walitumwa kila mtu kivyake na Roho Mtakatifu na kuitiwa kazi muhimu (Matendo ya mitume 13:2). Iyo kazi ilikua kueneza injili katika nchi za Cyprus na Asia.
Baadae, huduma ya Paulo ilimpeleka katika nchi za uropa, na kila wakati Paulo alijitahidi kuwa bora katika huduma za ulimwengu: " Shabaha yangu imekuwa nisihubiri mahali ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine" (Warumi15:20). Paulo alihubiri injili kutoka Yerusalemu mpaka kando ya Iliriko (mstari wa 19) na alikua na mpango wa kuenda uhispania (mstari wa 24), na mwishowe akafika Roma. Kitabu cha Matendo ya mitume kinaelezea jinsi kanisa la kwanza lilijitahidi katika huduma na kuhimiza umuhimu wa kuendeleza ujumbe kwa ulimwengu.
Mungu hana ubaguzi wa kabila ama kati ya mataifa( Matendo ya mitume 10:34-35). Biblia inasema kwamba bila Kristo sisi wote tuko pamoja kwa hali ya kiroho: wote wamepungukiwa na neema ya Mungu na wako chini ya laana ya Adamu. Kila mmoja wetu, kila kabila na mataifa yote yanafaa kusikia injili. Kila mtu anahitaji haki ya Mungu ambayo inakuja kupitia imani katika Yesu Kristo. "Lakini watamwitaje yeye ambaye hawajamwamini? Nao watawezaje kumwamini yeye ambaye hawajamsikia? Tena watamsikiaje bila mtu kuwahubiria? 15Nao watahubirije wasipopelekwa?" (Warumi 10:14-15). Neema imepewa kila mtu na Mungu anapenda watu wote bila kubagua.
Tunafaa kufuatilia ujumbe kwa ulimwengu kwa sababu Mungu anatamani watu wote wapate wokovu na wapate hekima ya ukweli(1Timotheo 2:4). Wokovu unapewa kwa yeyote yule anayetaka (Ufunuo 22:17). "Je, Mungu ni Mungu wa Wayahudi peke yao? Je, yeye si Mungu wa watu wa mataifa mengine pia? Ndio, yeye ni Mungu wa watu wa mataifa mengine pia" (Warumi 3:29). Ufunuo unaelezea ule mji mpya wa Yerusalemu ya mbinguni kama mahali ambapo mataifa yote yatatembea katika mwangaza wa mwana wa kondoo na mahali ambapo utukufu wa mataifa yote utaishi Ufunuo 21:22-27). Mungu anajali mataifa yote na wawakilishi wa mataifa yote watakua mbinguni.
Malaika alipea wachungaji wa Bethelehemu "…mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote" (Luka 2:10). Tunapopiga jeki ujumbe kwa ulimwengu , tunapoeneza habari njema ya wokovu ambayo ni Yesu Kristo tunamtukuza Mungu anayesema, "Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye Sayuni,Mungu wako anamiliki!" (Isaya 52:7).
English
Biblia inasema nini kuhusu ujumbe kwa ulimwengu?