settings icon
share icon
Swali

Ukamilishaji dhidi ya uswa—ni mtazamo upi uu sawa kibiblia?

Jibu


Ikiwekwa kwa muhtasari na "Barasa la Biblia la maswala ya Uume na Uuke," ukamilishaji ni mtazamo kwamba Mungu huwaruhusu wanawake kutumikia katika majukumu ya uongozi wa kanisa na badala yake Amewaita wanawake kutumikia, lakini katika yale majukumu ya kusaidia kukamilisha jukumu. Ikifupishwa na "Wakristo kwa Usawa wa Kibiblia" usawa ni mtazamo kwamba hukuna vizuizi kibiblia vya kijinsia katika huduma kanisani. Mitazamo yote miwili kudai kuwa na msingi wa kibiblia, ni muhimu ya kutosha kuchunguza kabisa ni nini Biblia inasema juu ya suala la utimilifu dhidi ya usawa.

Tena, kufupisha upande mmoja ni kuna waunga mkono usawa ambao wanaamini kuwa hakuna tofauti ya kijinsia na gangi sisi wote tu kitu kimoja katika Kristo, wanakwe na wanaume wanaeza kubadilishana majukumu ya uongozi na ya pale nyumbani. Mtazamo ulio kinyume umeshikiliwa wanao unga mkono itimilifu. Mtazamo wa umilifu unaamini katika sifa maalum za wanaume na wanawake kama watu (kwa mfano, kama binadamu walioumbwa kwa mfano wa Mungu), walakini waunga utimilifu wanashikilia tofauti za kijinsia inapofikia masuala ya majukumu katika jamii, kanisani, na nyumbani.

Hoja inayounga mkono utimilifu inaweza kutolewa kutoka 1 Timotheo 2: 9-15. Mstari huo haswa ambao unaonekana kupinga mtazamo wa usawa ni 1 Timotheo 2:12, ambayo inasoma hivi, "Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya mwanaume. Mwanamke inampasa kukaa kimya." Paulo anatoa maoni sawia katika 1 Wakorintho 14 ambapo anaandika, "wanawake wanapaswa kuwa kimya kanisani. Hawaruhusiwi kusema, bali wanyenyekee kama sheria isemavyo" (1 Wakorintho 14:34) Paulo anahoji kwamba wanawake hawaruhusiwi kufundisha na / au kuwa na mamlaka juu ya wanaume katika mazingira ya kanisa. Vifungu kama vile 1 Timotheo 3: 1-13 na Tito 1: 6-9 vinaonekana kutenga uongozi wa kanisa kuwa "ofisi" ya wanaume, vile vile.

Usawa kimsingi hufanya kauli yake ikiegemea Wagalatia 3:28. Katika mstari huo Paulo anaandika, "Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu." Mtazamo wa usawa unakauli kwamba katika Kristo tofauti za kijinsia ambazo zinaonyesha uhusiano ulioanguka zimeondolewa. Lakini je! hivi ndivyo Wagalatia 3:28 inapaswa kueleweka? Je! Muktadha unadhibitisha tafsiri kama hiyo? Ni wazi kabisa kwamba tafsiri hii inaharibu muktadha wa aya hii. Katika Wagalatia, Paulo anaonyesha ukweli mkuu wa kuhesabiwa haki kwa imani tu na sio kwa matendo (Wagalatia 2:16). Katika Wagalatia 3: 15-29, Paulo anaunga kauli ya kuhesabiwa hakina tofauti iliyoko kati ya sheria na ahadi. Wagalatia 3:28 inafaa kauli ya Paulo kwamba wote walio katika Kristo ni uzao wa Abrahamu kwa imani na warithi wa ahadi (Wagalatia 3:29). Muktadha wa kifungu hiki unaifanya iwe wazi kuwa Paulo anazungumzia juu ya wokovu, sio majukumu katika kanisa. Kwa maneno mengine, wokovu umetolewa bure kwa wote bila kuzingatia mambo ya nje kama kabila, hali ya uchumi, au jinsia. Kwa kupanua muktadha huu zaidi ili pia utumike kwa majukumu ya kijinsia kanisani unakiuka zaidi kauli ambayo Paulo alikuwa anaitoa.

Je! Ni nini tatizo la kuli hii, na kile watu wengi wanao unga dhana ya usawa wanakosa kuelewa, ni kwamba tofauti katika jukumu sio sawa na tofauti ya ubora, umuhimu, au thamani. Wanaume na wanawake wanathaminiwa sawia mbele za Mungu na mpango Wake. Wanawake hawajadunisha mbele za wanaume. Badala yake, Mungu ametoa majukumu tofauti kwa wanaume na wanawake kanisani na hata nyumbani kwa sababu hivyo ndivyo alivyotuumba tufanye kazi. Ukweli wa tofauti na usawa unaweza kuonekana katika safu ya utendaji katika Utatu (angalia 1 Wakorintho 11: 3). Mwana humtii Baba, na Roho Mtakatifu humtii Baba na Mwana. Uwasilishaji huu kikazi haumaanishi kuwa kuna udhalali katika usawa wa kiini; Watu wote watatu ni Mungu katika njia sawa, lakini wanatofautiana katika utendaji kazi wao. Vivyo hivyo, wanaume na wanawake ni wanadamu sawia na kwa usawa wanashiriki sura ya Mungu, lakini wana majukumu na kazi walizotengewa na Mungu zinazoonyesha ngazi za utendaji kazi katika Utatu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ukamilishaji dhidi ya uswa—ni mtazamo upi uu sawa kibiblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries