settings icon
share icon
Swali

Je, Ukonifusiani ni nini?

Jibu


Ukonifusiani, dini ya uaminifu wa kibinadamu, imekuwa na athari kubwa juu ya maisha, muundo wa jamii, na falsafa ya kisiasa ya China. Kuanzishwa kwa dini hurudi nyuma kwa mtu mmoja, anayejulikana kama Confucius, aliyezaliwa miaka 500 kabla ya Kristo. Ukonifusiani unahusika hasa na tabia za kimaadili na maisha ya kimaadili na mara nyingi jumuiya ndio mfumo wa maadili, badala ya dini. Unasisitiza duniani, sio mbinguni. Mafundisho ya Ukonifusiani msingi huwa kwa:

1. Uabudu wa mababu — ibada ya mababu waliokufa ambao mioyo yao inaaminika kudhibiti utawala wa wanao.

2. Utakatifu wa wana au binti- unyenyekevu na utiifu kwa wazee wa familia kwa wale walio wadogo.

Kanuni za msingi za Ukonifusiani ni:
1. Jen — utawala wa dhahabu
2. Chun-tai — mtu mpole na mwema
3. Cheng-ming — kutimiza vizuri wajibu wa jamii
4. Te — nguvu ya wema
5. Li — viwango bora vya mwenendo
6. Wen — sanaa za amani (muziki, mashairi, nk)

Mfumo wa kimaadili wa Ukonifusiani una mengi ya kuushukuru kwa sababu wema daima ni kitu kinachohitajika, wote katika kwa mtu binafsi na jamii. Hata hivyo, falsafa ya kimaadili Confucius alimtumaini sana ilikuwa ya juhudi za kujitegemea, bila kuacha nafasi au haja ya Mungu. Confucius alifundisha kwamba mtu anaweza kufanya yote ambayo ni muhimu ili kuboresha maisha yake na utamaduni wake, akitegemeana wema ndani yake mwenyewe ili kuifikia. Ukristo wa Kibiblia, hata hivyo, hufundisha hasa kinyume chake. Sio tu kwamba mtu hana uwezo wa "kusafisha tendo lake," hawezi kumpendeza Mungu peke yake au kupata uzima wa milele mbinguni.

Biblia inafundisha kwamba mwanadamu ni mwenye dhambi tangu kuzaliwa (Yeremia 17: 9) na hawezi kufanya kazi nzuri za kutosha ili akubalike na Mungu mtakatifu na mwenye haki kabisa. "kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria" (Warumi 3:20). Mwanadamu kwa ufupi, amewekwa katika hali ambayo anahitaji Mwokozi kufanya hivyo kwa ajili yake. Mungu ametoa Mwokozi katika Mwanawe, Yesu Kristo, ambaye alikufa msalabani kulipa adhabu ya dhambi zetu na kutufanya sisi kukubalika kwa Mungu. Alibadilisha maisha yake kamilifu kwa ajili ya dhambi zetu: "Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye" (2 Wakorintho 5:21).

Ukonifusiani, kama dini zingine zote za uwongo, hutegemea kazi na uwezo wa mwanadamu. Ukristo peke yake ndio unatambua kuwa "wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu" (Waroma 3:23), na wafuasi wake wanategemea tu juu ya Yesu Kristo, ambaye sadaka yake msalabani huwapa wokovu kwa wote wanaomwamini na wasioweka imani yao nafsi zao wenyewe, bali Yeye pekee.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Ukonifusiani ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries