Swali
Je! Ni kwa nini Ukristo ni dini ya umwagaji damu?
Jibu
Ili uelewe ni kwa nini Ukristo ni "dini ya umwagaji damu," lazima turudi nyuma kwenye matamshi ya Mungu kuhusu damu katika Agano la Kale: "uhai wa kiumbe uko katika damu (Mambo ya Walawi 17:11,14). Hapa Mungu anatuambia kuwa uhai na damu kimsingi ni kitu kimoja na sawia. Damu hubeba virutubishi kwenye sehemu zote za mwili ambavyo hudumisha uhai. Inawakilisha kiini cha uhai. Kwa kulinganisha kumwaga damu kunawakilisha kupoteza maisha, kama vile kifo.
Damu pia imetumika katika Biblia kuwakilisha uhai. Wakat Adamu na Hawa walitenda dhambi katika bustani mwa Edeni kwa kutomtii Mungu na kula tunda walilokatazwa, walipatwa na kifo cha kiroho papo hapo, na miaka baadaye walipatwa na kifo cha mwili. Onyo la Mungu, "lakini kamwe usile matunda ya mti wa kujua mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa" (Mwanzo 2:17) lilitimia. Damu yao-maisha yao- hayakutiwa doa na dhambi. Katika mpango wake wa neema, walakini, Mungu alipeana "namna ya kutoka" katika mtanziko kwa kutangaza dhabihu hiyo ya damu, kwanza damu ya wanyama na kisha damu ya Mwanakondoo wa Mungu (Yesu Kristo), ingetosha kusafisha dhambi za mwanadamu aliyeanguka na kuturejesha kwa maisha ya kiroho. Alianzisha mfumo wa dhabihu, akianza na wanyama ambao Yeye mwenyewe aliwaua ili kutengeza kanzu ya kwanza na hapo kwa "kufunika" dhambi ya Adamu na Hawa (Mwanzo 3:21). dhabihu zote za Agano la Kale zilizofuatia baadaye zote zilikuwa za muda, zikihitaji kurudiwa tena na tena. Dhabihu hizo endelevu zilikuwa kivuli cha ile dhabihu moja ya mwisho, Kristo, ambaye damu yake ilimwagika msalabani italipa adabu ya dhambi milele yote. Kifo chake kilifanya kusihitajike umwagikaji wowote wa damu (Waebrania 10:1-10).
Ingawaje Ukristo ni wa umwagaji damu, naam ndivyo. Lakini ni dini ya umwagaji damu ya kipekee. Kinyume na dini zisizo za umwagaji damu, unachukulia dhambi kwa uzito, ukionyesha kuwa Mungu hachukulii dhambi hivi hivi na anatoa hukumu ya kifo kwa dhambi. Dhambi si kitu kidogo. Ni ishara fupi ya kiburi ambacho kilimgeuza Ibilisi kuwa pepo. Ilikuwa ishara fupi ya wivu ambayo ilimsababisha Kaini kumuua Abeli, nk. Adamu na Hawa kwa kulila tunda walilokatazwa, walimwamini yule mdanganyifu kuliko Mungu aliye mwema na mpenzi, na kuamua kuasi dhidi ya upendo wake na kukataa wema wa maadili Yake. Ukristo ni dini ya umwagaji damu kwa sababu unatizama dhambi jinsi vile Mungu mtakatifu anavyoitizama-kwa uzito.
Pia, kwa sababu Mungu ni mwenye haki, dhambi inahitaji adhabu. Mungu hawezi kuisamehe kwa huruma hadi pale matakwa ya haki yametimizwa. Hivyo, aja ya dhabihu kabla ya msamaha inawezekana. Umwagaji wa damu ya Wanyama, vile Wayahudi wanaelezea, inaweza tu "kufunika" dhambi kwa muda tu (Waebrania 10:4) hadi pale dhabihu iliyokusudiwa na inayotosha ilifanywa kupitia kifo cha Kristo cha msamaha. Hivyo, Ukristo ni tofauti toka kwa dini zingine zote za umwagaji damu kwamba ni Ukristo pekee ambao unatoa dhabihu ya kutosha kushughulikia shida ya dhambi. Mwisho, ingawa unawakilisha dhabihu ya damu kwa namna hii, mwishowe ndio dini pekee isiyomwaga damu. Kinyume cha kifo ni uzima. Katika kifo cha Yesu, Alileta uzima vile imeonyeshwa katika aya nyingi. Na katika kumwamini Kristo na dhabihu ya uridhisho kwa dhambi ya mtu, mtu ameokolewa kutoka kifo na kupelekwa kwenye uzima (Yohana 5:24); 1 Yohana 3:14). Ndani yake kuna uzima. Njia zingine zote zinaelekeza kwenye kifo (Matendo 4:16; Yohana 14:6).
English
Je! Ni kwa nini Ukristo ni dini ya umwagaji damu?