Swali
Je! Kuna umuhimu gani na udhaifu wa mtazamo wa unyakuo kabla ya ghadhabu?
Jibu
Kunayo maoni mengi kuhusu mambo ya nyakati za mwisho (fundisho la mambo ya baadaye). Walakini, takribani Wakristo wote wanakubaliana kwa mambo matatu: 1) kutakuwa na wakati baadaye wa dhiki, 2) baada ya wakati wa dhiki, Yesu atarudi kuanzisha ufalme Wake, na, 3) waumini watabadilishwa kutoka kwa mili yao ya uharibifu hadi mwili usio haribika-kwa maneno mengine kutakuwa na unyakuo (Yohana 14:1-3; 1 Wakorintho 15:51-52; 1 Wathesalonike 4:16-17). Swali moja limesalia ni, ni lini unyakuo utatokea kwa mjibu wa dhiki na kurudi mara ya pili kwa Kristo?
Nadharia tatu za kimsingi kuhusu wakati wa unyakuo ni dhiki kabla ya, ambao unaweka unyakuo kabla ya dhiki; katikati mwa dhiki, ambao huweka unyakuo karibu au katikati ya dhiki; na dhiki baada ya, ambayo inaweka unyakuo mwishoni mwa dhiki. Kwa karibu hii inahusiana sana na kipindi cha katikati mwa mateso ni imani kuwa unyakuo wa "kabla ya ghadhabu", ambayo ndio mada ya makala haya.
Nadharia ya unyakuo kabla ya ghadhabu inasema kuwa unyakuo utatokea kabla ya "siku kuu ya…ghadhabu" (Ufunuo 6:17). Kulingana na mtazamo wa unyakuo kabla ya ghadhabu, waumini hupitia mateso mengi lakini sio wakati wa ghadhabu ya Mungu kabla ya mwisho wa dhiki (Mathayo 24:21). Kanisa litastahimili mateso ya Shetani na mateso ya wanadamu, lakini watanusurika ghadhabu ya Mungu. Kabla ya Mungu kuimwaga hukumu yake ya mwisho kwa ulimwengu, kanisa litanyakuliwa mawinguni.
Nadharia ya unyakuo wa kabla ya ghadhabu inaona tarumbeta na hukumu za bakuli (Ufunuo 7-16) kama ghadhabu ya Mungu, ambayo kanisa limeondolewa (1 Wathesalonike 5: 9). Walakini, hukumu sita za kwanza za muhuri (Ufunuo 6) hazizingatiwi kuwa hasira ya Mungu; badala yake, zinaonekana kama "ghadhabu ya Shetani" au "ghadhabu ya mpinga-Kristo." Hii ni kwa sababu hakuna kutajwa moja kwa moja kwa ghadhabu ya Mungu mpaka baada ya muhuri wa sita kuvunjwa (Ufunuo 6:17). Kulingana na nadharia ya unyakuo kabla ya ghadhabu, kanisa litakuwepo ili lionje mihuri ya kwanza sita.
Ukilinganisha Ufunuo 6 na Mathayo 24, nadharia ya unyakuo kabla ya ghadhabu unatambua muhuri wa kwanza wa hukumu na elezeo lile la Yesu kwa nyakati za miwsho katika Mathayo 24:4-7. Baadaye Yesu anarejelea kwa tukio hili kama "Haya yote yatakuwa ndio mwanzo wa utungu" (Mathayo 24:8). Katika aya ya 29 na 30, "ishara ya Mwana wa Adamu" itaonekana mawinguni, na ni katika wakati huu, kulingana na nadharia ya unyakuo kabla ya ghadhabu, kwamba unyakuzi wa kanisa utafanyika.
Udhaifu mmoja wa msimamo wa unyakuo kabla ya ghadhabu ni dhana yake kwamba "wateule" waliotajwa katika Mathayo 24:22, 31 ni watakatifu wa umri wa kanisa. Watakatifu hawa wangeweza ni watu binafsi waliokolewa kwa urahisi wakati wa dhiki ya miaka saba; kwa kweli, Yesu anawaambia wale wanaoyakimbia mateso ya mpinga Kristo waombe kwamba kukimbia kwao kusitokee "siku ya Sabato" (Mathayo 24:20). Kwa kuwa kanisa haliko chini ya sheria ya Musa na halishiki Sabato, maneno ya Yesu hayawezi kuelekezwa kwa kanisa.
Udhaifu mwingine kataka nadharia ya unyakuzi kabla ya ghadhabu ni mafunzo yake kuwa hukumu ya muhuri wa kwanza sio ghadhabu ya Mungu. Maandiko yanaonyesha kwamba ni Mwanakondoo anayefungua mihuri (Ufunuo 5: 5; 6: 1). Hakuna mtu mwingine anayepatikana kustahili kuzifungua (Ufunuo 5: 3-4). Inaonekana, basi, hizi sio hukumu za mwanadamu, bali ni za Mungu. Dhiki huanza wakati Yesu anafungua muhuri wa kwanza, na kutoka wakati huo na kuendelea, ghadhabu ya Mungu inaachiliwa kwa ulimwengu wenye dhambi.
Udhaifu wa mwisho wa nadharia ya unyakuzi kabla ya ghadhabu nadharia zingine hushiriki mtazamo huo; kwa mfano, Biblia haitoi muda mwafaka kuhusu matukio ya baadaye. Maandiko hayafundishi wazi mtazamo mmoja juu ya mwingine, na ndio sababu tuna maoni tofauti tofauti juu ya nyakati za mwisho na maoni anuwai juu ya jinsi unabii unaohusiana unapaswa kuoanishwa.
English
Je! Kuna umuhimu gani na udhaifu wa mtazamo wa unyakuo kabla ya ghadhabu?