settings icon
share icon
Swali

Mwanamke anawezaje kupona na kupata afueni baada ya kuavya mimba?

Jibu


Ni kitu cha kusikitisha kusema kuwa, baada ya kuavya mimba na kujutia jambo hilo baadaye ni uzoefu wa kawaida sana. Ingawa jambo limefanyika haliwezi kufutwa, wanawake wanaweza kupata uponyaji na afueni baada ya kuavya mimba. Mungu wa faraja na uponyaji wote ana uwezo zaidi wa kupunguza huzuni na majuto kuavya mimba na anaweza wa kurejesha wanawake katika maisha na furaha.

Ingawa watoto ni baraka daima, daima huwaji katika hali ya baraka zaidi. Moja ya matokeo ya ngono kabla ya ndoa mara nyingi ni mimba ya mtoto asiyehitajika. Hii inaweza kuwa jambo la kutisha kwa mtu ambaye hayuko tayari kifedha, kihisia, au kimwili kwa jukumu kama hilo. Wanawake wengi na wasichana wa ujana ambao wanaamua kutafuta kuavya mimba wanaogopa, huchanganyikiwa, hukata tamaa, na kuathiriwa sana. Katika hali ya wao kutafuta majibu, wao wamepotoshwa kuamini kwamba watoto wenye hawajazaliwa hutumia "uvimbe wa tishu," sio wanadamu ambao hawajazaliwa. Mara nyingi ufunuo huu unakuja baadaye, kwa namna ya ugonjwa wa shida baada ya utoaji mimba, hatia, na mfadhaiko.

Kuna habari njema kwa mtu yeyote ambaye ameavya mimba, na ni kwamba Mungu hutoa msamaha kwa yeyote anayeomba. Warumi 3:22 inasema, "Ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti." Haujachelewa sana kuja kwa Mungu kwa ajili ya uponyaji. Hakuna chochote tunaweza kufanya ambacho ni kibaya sana na hakiwezi kusamehewa. Mungu hutoa msamaha huu, na pia hutoa amani ya akili na moyo, ikiwa tutapokea tu kwa kuweka imani yetu katika Kristo, Yesu, kumruhusu kuishi na mamlaka ya kudumu katika maisha yetu.

Wanawake wengine ambao tayari ni Wakristo wanajikuta katika hali ambapo wanaweza kuamua kutoa mimba, labda kwa sababu ya hofu ya jinsi wataonekana na jamii ya Kikristo wakati uchaguzi wao wa kuwa na ngono kabla ya ndoa ni dhahiri sana. Hata kama mwanamke Mkristo anajua jinsi Mungu anavyohisi kuhusu utoaji mimba, anaweza kujisikia, kutokana na kukata tamaa, kwamba lazima aondoe "ushahidi." Hii labda, kwa sehemu, ni wajibu wa kanisa, ambayo haiwezi kuwasaidia wanawake katika hali hii na vile tunapaswa. Ni muhimu kuwahakikishia wanawake hawa kwamba, ingawa Mungu hakubali matendo yao, Yeye yuko tayari kutoa msamaha na ukombozi. Vile vile ni kweli kwa mwanamke Mkristo ambaye ameavya mimba. Naam, ni makosa, kuchukua maisha, lakini sio kosa lisilosamehewa. Biblia inasema kuwa hakuna hukumu kwa wale ambao ni wa Kristo Yesu (Waroma 8: 1), na hivyo tunapomwomba msamaha, Yeye hutoa kwa hiari. Hii si kwa sababu tunastahili, lakini kwa sababu hii ni hali ya upendo ya Bwana wetu.

Wakati mwanamke anapotambua matokeo ya utoaji mimba, anaweza kupata vigumu kujisamehe mwenyewe. Lakini Mungu hatutaki tuishi na hatia ya milele; Anataka sisi kujifunze kutokana na makosa yetu na kuwatumia kwa faida Yake, kama vile yetu wenyewe. Itahitaji maombi mengi, ambayo ni mazungumzo tu na Mungu. Hii na kujifunza Biblia inatusaidia kumjua Mungu vizuri ili tuweze kumtumaini kutuponya na kuwa na uwezo zaidi wa kufanya kazi Yake. Badala ya kukaa juu ya tendo, mwanamke anapaswa kuhimizwa kutumia uzoefu wake ili kuwasaidia wengine. Anaweza kwanza haja ya kupitia ushauri wa Kikristo ili kusaidia kupata uzoefu, kwa sababu anaweza kuwa na uchungu. Lakini baadaye, ikiwa amemtegemea Bwana, atakuwa na nguvu na zaidi kukomaa kiroho. Atakuwa na uzoefu ambao Mungu anaweza kutumia ili kuimarisha tabia yake na kumtayarisha kwa kuwahudumia wengine.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mwanamke anawezaje kupona na kupata afueni baada ya kuavya mimba?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries