Swali
Je, mtazamo wa Kikristo kuhusu kuposa ni upi?
Jibu
Katika Biblia, kulikuwa na hatua tatu ambazo Wayahudi walipaswa kuchukua wakati wa kuolewa. Familia kwanza zilikubaliana kuhusu upanisho huo, kisha tangazo la umma lilifanyika. Kwa hatua hii, wanandoa walikuwa wameposana, au ahidiana. Mwishowe, walioana rasmi na kuanza kuishi pamoja. Kwa hiyo, ahadi ya ndoa ilikuwa sawia na kile tunachokiita siku hizi kuposa, isipokuwa kuwa jamii yetu haiheshimu uzito wa uposa kama walivyofanya wakati huo. Wakati wanandoa wa Kiyahudi walikuwa wameposana wakati wa nyakati za Biblia, tayari walikuwa wameunganishwa na mkataba ambao haungeweza kuvunjwa ila tu kwa njia ya kifo au talaka.
Mkristo yeyote anayezingatia ndoa anahitaji kutambua kina cha aina hii cha kujitolea na si kuingia kwa ndoa kiurahisi tu. Mungu anataka ndoa iwe ahadi ya milele, sio makubaliano ya muda. Biblia inasema hivi juu ya ndoa: "'Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe. Hata nyumbani tena wanafunzi wakamwuliza habari ya neno hilo" (Marko 10: 7-9).
Wakristo wanahitaji kuhakikisha wana ufahamu wa wazi wa mtu wanayeweza kuoa kabla ya kuposwa. Biblia inasema kwamba Wakristo hawawezi kushirikiana na kuishi kwa umoja na wasioamini (2 Wakorintho 6: 14-15). Mkristo anayeungana na asiyeamini anahakikisha kwamba Mkristo atachukuliwa mbali na Kristo kwa sababu, kama vile Biblia inasema, "ushirika mbaya huharibu tabia nzuri" (1 Wakorintho 15:33). Njia pekee ya kuwa na msingi wa kuheshimu Mungu na imara kwa ajili ya ndoa ni mtu kuwa imara katika Imani yake na kuhakikisha kuwa mpenzi ambaye ananuia kumwoa amejitolea sawia kwa Mungu.
Wakristo wanapaswa kuishi maisha yao na Mungu kama mkurugenzi. Anataka kuwa sehemu ya kila kipengele cha maisha yetu, ikiwa ni pamoja na yule ambaye tunamwoa. Kuwa na ufahamu wazi wa Neno la Mungu na kuendeleza uhusiano wa kibinafsi na Yeye kwa njia ya sala na kujitolea kwa uongozi wa Roho Mtakatifu ni hatua ya kwanza na muhimu katika kuamua mapenzi Yake kwetu. Ushauri wa dunia juu ya urafiki na uposa unapaswa kuchukuliwa tu kulingana na ukweli wa Mungu katika Maandiko. Ikiwa tunatafuta mapenzi Yake katika yote tunayofanya, Yeye ataongoza njia zetu (Methali 3: 5-6).
English
Je, mtazamo wa Kikristo kuhusu kuposa ni upi?