Swali
Je! Unaweza kunipa ushauri wa uhusiano wa Kikristo?
Jibu
Mara nyingi tunapokea maswali kwa mstari wa: "Ninavutiwa na watu wawili tofauti ... ni nani ninayepaswa kuchagua kuwa mpenzi wangu?" Au, "Mimi niko katika uhusiano na mpenzi wangu alifanya / alisema '_____', kwa hivyo, napaswa kuvunja uchumba naye?" Aina hizi za maswali ni ngumu sana kwetu kujibu. GotQuestions.org sio huduma ya ushauri wa uhusiano wa Kikristo. Tutajitahidi daima kukuambia kile Biblia inasema juu ya hali fulani. Hata hivyo, kuhusiana na masuala ya ushauri wa uhusiano, Biblia mara chache huzungumzia hali tunayoulizwa. Biblia inahusika zaidi na uhusiano wetu na Mungu.
Sisi husita sana kutoa ushauri wa uhusiano. Ni vigumu kutoa shauri la hekima kwa suala la kibinafsi kupitia kwa makala. Ni vigumu sana kutoa ushauri wa uhusiano wa Kikristo wakati hatujui watu wanaohusika, hatujapokea maelezo yote, na / au tunapata tu upande mmoja wa hadithi. Hatutaki kuongea kwa niapa ya Mungu kwa kutoa ushauri wa kimamlaka katika uhusiano wa Wakristo.
Kwa kusema hayo, ushauri wetu ni gani? Ni ushauri wetu kwamba unene na Mungu kuhusu uhusiano wako. Omba kwa Bwana, kumwomba akufunulie wazi kile anatak ufanye (Wafilipi 4: 6-7). Uombe Mungu akupe hekima na ufahamu (Yakobo 1: 5). Mungu anaahidi kujibu haja ambazo zinaulizwa kulingana na mapenzi Yake (1 Yohana 5: 14-15). Kuwa busara na fahamu ni dhahiri mapenzi ya Mungu. Mungu anataka ufanye maamuzi mazuri ya uhusiano. Mungu anataka Wakristo kuwa na furaha na kuimarishwa kama matokeo ya mahusiano yao. Ikiwa unamwomba Mungu kwa moyo wazi na roho wa unyenyekevu, atakupa ushauri wa uhusiano unaohitaji.
Hatimaye, pata ushauri wenye hekima na Wakristo wenye ukomavu ambao wamekuwa wameoa kwa miaka mingi na wametembea pamoja na Mungu wakati wote. Tafuta mwongozo kutoka kwa mchungaji wako, wazee au viongozi wengine wa kanisa. Miaka yao ya uzoefu huwawezesha kuzungumza kutokana na hekima na ujuzi wa Mungu katika maisha yao.
English
Je! Unaweza kunipa ushauri wa uhusiano wa Kikristo?