Swali
Je, imekubalika kuwa na ushirika nje ya kanisa? Je, watu wa familia wanaeza zingatia ushirika wakiwa nyumbani, kwa mikutano ya kikristo na marafiki ama ata kibnafsi, n.k?
Jibu
Huduma za ushirika ambayo pia inaitwa chakula cha bwana, mara nyingi hufanyika kanisani wakati wa kuabudu. Hata hivyo kwa kanisa la kwanza huduma za kuabudu zilifanyika nyumbani. Kwa kanisa la Yerusalem walikusanyika kwa nyumba ya Maria (Matendo ya mitume 12:12), uko Ufilipino kwa nyumba ya Lidia (Matendo ya mitume 16:40), na uko Efeso kwa nyumba ya Aquila na Priscilla ( 1Wakoritho 16:19). Uko Colossae kanisa ilifanyika kwa nyumba ya Filemoni ( Filemoni 2). Matendo ya mitume mbili inatufunza kwamba kanisa la kwanza lilikusanyika kupata mafunzo ya mitume, maombi,kuabudu na kushiriki mkate ambayo inaashiriwa kama ushirika (Matendo ya mitume 2:42).
Hata hivyo maandiko ijaelezea wazi mahali huduma ya ushirika inafaa kufanyiwa. Ushirika umepeanwa kwa wagonjwa hosipitalini na ata kwa nyumba za kuwalinda wazee. Wamishonari walio kwa utumwa wameshiriki chakula cha bwana na waumini ata penye kanisa hazijajengwa bado. Familia zingine huwa zinashiriki chakula cha bwana wakati hafla maalum kama vile krismasi. Ili kukumbuka pasaka, Bwana wetu alishiriki chakula na wanafunzi wake na hii ndo ilikua ushirika wa kwanza. Maagizo pekee ambayo tumepewa kuhusu ushirika ni yale Yesu mwenyewe alisema, "akamshukuru Mungu, akaumega akasema, ' huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu fanyeni hivi kwa kunikumbuka.' Vivyo hivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe akasema: 'hiki ni kikombe cha agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu,fanyeni hivi kila mnapokunywa kwa kunikumbuka,' maana kila mnapokula mkate huu na kunywa kikombe hiki, mwatangaza kifo cha Bwana mpaka atakapokuja." Kifungu hiki kinatupea maagizo ili tuweze kushiriki chakula cha Bwana na tuelewe umuhimu wa kenye tunafanya.
Kanisa ilijengwa baada ya pentekosti na apo ndo ushirika ulianza kufanyiwa kanisani na kuchukuliwa kama mojawapo ya agizo la kanisa. Kwa hivyo uongozi wa kanisa ambao unatambulika ndo ulikua unaongoza ushirika. Lakini hakuna sababu za kikiblia ambazo zinakana kuwa chakula ya bwana haiwezi peanwa nyumbani miongoni mwa marafiki na familia; ama kwa ibada ya kifamilia. Kitu ya muhimu si mahali penye unashiriki, bali ni kukumbuka mwili na damu ya Kristo ambayo imetuokoa.
English
Je, imekubalika kuwa na ushirika nje ya kanisa? Je, watu wa familia wanaeza zingatia ushirika wakiwa nyumbani, kwa mikutano ya kikristo na marafiki ama ata kibnafsi, n.k?