settings icon
share icon
Swali

Je! Mkristo anapaswa kuitikia aje utabiri wa siku ya mwisho ambo unatolewa?

Jibu


Katika miaka ya 1950 dunia iliogopa ilikuwa kwenye ukingo wa ufumup wa nyuklia. Karibu na mwanzo wa karne, kulikuwa na uvumi ulimwenguni kote kuhusu Y2K na uwezekano wa mwisho wa ulimwengu uliostaarabika kama matokeo. Machafuko ya utamaduni wa burudani ulizuka mwishoni mwa kalenda ya Mayan mnamo 2012. Halafu kulikuwa na majadiliano katika duru za Kikristo juu ya kuonekana kwa mbara miezi ya damu, ikidhaniwa pia ni ishara ya hafla mbaya. Je! Mkristo anapaswa kuitikia aje utabiri wa siku ya mwisho na habari zinazohusiana na matukio kama hayo?

Kutoka kwa mtazamo wa Kikristo, itikio letu la kwanza linapaswa kuwa kupumua kwa kasi na kutulia. Wakati mmoja katika maisha haya, dunia itaisha (2Petro 3:10). Kristo atarudi (Ufunuo 19:11-13) katika wakati ametayarisha (1 Wakorintho 15:51-52). Na huku kila mtu duniani hayuko mbali na siku yake ya mwisho sasa hivi (Zaburi 39:5). Mshutuko wa moyo, vita, ajali mambo kama hayo yatatuleta karibu na Muumba wetu kwa haraka sana kuliko janga la ulimwengu wote (Yakobo 4:13-15). Iwe siku za mwisho ziko karibu sana au kuwa mbali, tumeitwa kujitayarisha (2 Wakorintho 6:2), na sio kuwa na woga.

Wingi wa utabiri wa siku za mwisho ni uvumi, zimwi au hisia sisizo na ufahamu. Hata watu wa Mayan hawakufikiria juu ya msimu wa kalenda yao kuwa inatabiri juu ya mwisho wa dunia. Wataalam wa tarakilishi sio wao walikuwa wanapendekeza tishio la Y2K. Hakuna mwanteolojia wa Kikristo anayefikiria kuwa hali ya mbara mwezi mwekundu ni kiashiria kikuu cha hafla fulani. Kama ilivyo kwa mitindo mingine na uwendawazimu, mazungumzo hayo yanaongozwa na fikira mbaya na ukweli mbaya zaidi.

Mkristo ambaye ameokoka anaweza kuwa na ujaziri katika wokovu wake na kumwamini Mungu kushughulikia kila kitu (Mathayo 6:25-34). Tunaambiwa kwamba kuna uwezekano wa kusoma ishara wa nyakati za mwisho (Mathayo 16:3) lakini pia ni vigumu kwa mtu yeyote kujua kwa uhakika ni lini nyakati za mwisho zitatokea (Mathayo 24:36). Badala ya kuangazia siku, tofauti na uvumi, tunapaswa kuzingatia kuihubiri injili kwa watu wengi iwezakanavyo. Meli inateremka, lakini kabla ya kuwa na hofu juu ya ni lini nyakati za mwisho zatakuwa, tunahitaji kuleta watu wengi waingie katika mashua hii na zile nguo za kukinga maisha!

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mkristo anapaswa kuitikia aje utabiri wa siku ya mwisho ambo unatolewa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries