settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu utakatifu? Je! ina maana gani kuwa mtakatifu?

Jibu


Katika 1 Petro 1:13-16, Petro anawaandikia waumini, “Kwa hiyo, tayarisheni nia zenu kwa kazi; mwe na kiasi, mkitumainia kikamilifu ile neema mtakayopewa Yesu Kristo atakapodhihirishwa. Kama watoto watiifu, msifuate tamaa zenu mbaya wakati mlipoishi kwa ujinga. Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, nanyi kuweni watakatifu katika mwenendo wenu wote. Kwa maana imeandikwa: “Kuweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu.” Petro ananukuu kutoka katika Walawi 11:44 na Walawi 19:2.

Kwanza, acha tuangalie utakatifu wa Mungu. Je, inamaanisha nini kuwa Mungu ni mtakatifu? Vifungu kama 1 Samweli 2:2 na Isaya 6:3 ni mifano miwili tu kati ya vifungu vingi kuhusu utakatifu wa Mungu. Njia nyingine ya kusema kuwa ni ukamilifu kabisa. Mungu hafanani mtu yeyote (angalia Hosea 11:9), na utakatifu wake ndio kiini cha huo “wingine.” Utu wake hauna kabisa chembe ya dhambi (Yakobo 1:13; Waebrania 6:18). Yeye yuko juu zaidi ya kila mtu, na hakuna mwenye anaweza linganishwa Naye (Zaburi 40:5). Utakatifu wa Mungu unaenea katika utu wake wote na kuunda sifa Zake zote. Upendo wake ni upendo mtakatifu, rehema zake ni rehema takatifu, na hata hasira na ghadhabu yake ni hasira takatifu na ghadhabu takatifu. Dhana hizi ni ngumu kwa wanadamu kuelewa, vile ilivyo ngumu kwetu kumwelewa Mungu na ukamilifu Wake.

Kisha, ina maana gani kwetu kuwa watakatifu? Wakati Mungu aliiambia Israeli kuwa watakatifu katika Walawi 11 na 19, alikuwa akiwaagiza wawe tofauti na mataifa mengine kwa kuwapa kanuni maalum za kutawala maisha yao. Israeli ni taifa teule la Mungu na Mungu amewatenga na makundi ya watu wengine wote. Wao ni watu wake maaulum, na kwa sababu hiyo walipewa viwango ambavyo Mungu alitaka waishi kwavyo ili ulimwengu ujue wao ni wa Mungu. Wakati Petro anarudia maneno ya Bwana katika 1 Petro 1:16, anazungumza hasa na waumini. Kama waumini tunapaswa “kutengwa” na dunia kwa ajili ya Bwana. Tunapaswa kuishi katika viwango vya Mungu, na sio viwango vya dunia. Mungu hatuiti tuwe wakamilifu, bali tuwe tofauti na ulimwengu. 1 Petro 2:9 inawaelezea waumini kuwa “taifa takatifu.” Ni ukweli tumetengwa kutoka kwa ulimwengu; tunapaswa kuishi ukweli huo katika maisha yetu ya kila siku, ambayo Petro anatuambia jinsi ya kufanya katika 1 Petro 1:13-16.

Hatimaye, tunawezaje kuwa watakatifu? Utakatifu unatokana tu na uhusiano mzuri na Mungu kwa kumwamini Yesu Kristo kama Mwokozi (kukubali zawadi yake ya uzima wa milele). Ikiwa hatujaiweka imani yetu kwa Mwana wa Mungu pekee ili atuokoe kutoka katika dhambi zetu, basi kutafuta kwetu utakatifu ni bure. Kwa hiyo, lazima kwanza tuhakikishe kwamba sisi ni waumini waliozaliwa mara ya pili (ona Yohana 3). Ikiwa kwa kweli sisi ni waumini, basi tunatambua kwamba nafasi yetu katika Kristo hututenga na ulimwengu (1 Petro 2:9). Baada ya yote tuna uhusiano na Mungu aliye hai. Kisha ni lazima kila siku tuishi maisha ya kujitenga bila kujaribu “kujichanganya” na ulimwengu, bali tuishi kulingana na Neno la Mungu tunapojifunza Biblia na kukua ndani yake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu utakatifu? Je! ina maana gani kuwa mtakatifu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries