Swali
Utawala wa Kristo ni nini na maana yake halisi ni gani?
Jibu
Utawala wa Kristo ni fundisho linalozunguka mamlaka ya Yesu na asili Yake ya Mungu. Kwa maneno mafupi, kuadhibitisha utawala wa Kristo ni kudhibitisha kuwa Yesu ni Mungu.
Fafanusi ya kamusi ya neno utawala ni "mkuu katika kitengo au mamlaka" au "kuu kwa kiwango au sifa." Katika maana halisi, hakuna iliyo bora. Utawala wa kitu ndio mwisho wake. Yesu ndiye nguvu, utukufu, mamlaka na muhimu wa mwisho. Utawala wa Yesu juu ya vitu vyote imeanzishwa hasa katika Waebrania na Wakolosai.
Mada kuu ya kitabu cha Waebrania ni kuelezea kazi ya Yesu katika muktadha wa mfumo wa Agano la Kale. Yesu alikuwa utimizo wa utamaduni na jukumu la Kiyahudi katika Agano la Kale. Mada nyingine kuu kitabu cha Waebrania ni kuwa Yesu hawakilishi njia mpya ya kufanya mambo pekee. Badala yake, Yeye ni mkuu. Yeye ndiye timizo halisi la njia ya kale ya kufanya mambo na kwa hivyo Yeye ni mkuu kuliko njia hizo. Kuhusu mfumo wa hekalu chini ya sheria za Musa, mwandisho wa Waebrania anaandika, "Lakini sasa Yesu amepewa huduma ya kikuhani iliyo bora kuliko yao, kama vile agano alilothibitisha kati ya watu na Mungu ni bora zaidi, kwani lina msingi wake katika ahadi za mambo yaliyo bora zaidi" (Waebrania 8:6). Kwa uhalisi, Yesu ni mkuu kuliko mfumo wa Agano la Kale. Anaitunza na kuipita wakati mmoja namna ya zamani ya kufanya mambo. Hili ni dhahiri katika ulinganisho wa Yesu na majukumu na tamaduni za Agano la Kale. Kwa mfano, tunaambiwa kuwa "Lakini Yesu si kama wao, yeye anaishi milele; ukuhani wake hauondoki kwake. Hivyo, yeye anaweza daima kuwaokoa kabisa wote wanaomwendea Mungu kwa njia yake, maana yeye anaishi milele kuwaombea kwa Mungu" (Waebrania 7:24-25). Kwa hivyo Yesu anajumisha ukuhani wa Agano la Kale na utawala wake juu yake.
Waebrania inaelezea kuwa Kristo ndiye mkuu zaidi kulika majukumu na mifumo. Waebrania 1:3 inasema, "Yeye ni mngao wa utukufu wa Mungu, na mfano kamili wa hali ya Mungu mwenyewe, akiutegemeza ulimwengu kwa neno lake lenye nguvu." Vile vile, Wakolosai 2:9 inasema, "Maana, ndani yake Kristo katika ubinadamu wake, umo ukamilifu wote wa Mungu." Kihalisi, Yesu ni Mungu.
Wakolosai 1:15-23 imepewa kichwa "Utawala wa Kristo" katika baadhi ya Biblia. Katika kifungu hiki, Paulo anaiweka wazi kuwa Yesu yuko juu ya vitu vyote. Kristo anaitwa, "Kristo ni mfano wa Mungu asiyeonekana" na "mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote" (Wakolosai 1:15). Neno mzaliwa wa kwanza linaeza onekana la kunganya. Hii haimanishi kwamba Kristo aliumbwa (jinsi ilivyo katika mafundisho ya Mashahidi wa Yehova). Badala yake, neno mzaliwa wa kwanza hurejelea nafasi ya mamlaka. Kuwa "mzaliwa wa kanza" alikuwa anashikilia nafasi ya heshima. Papo hapo Paulo anaendelea na kuelezea jukumu la Kristo: "Maana kwake vitu vyote viliumbwa kila kitu duniani na mbinguni, vitu vinavyoonekana na visivyoonekana: Wenye enzi, watawala, wakuu na wenye nguvu. Vyote viliumbwa kwake na kwa ajili yake" (Wakolosai 1:16). Hii inamaanisha kwamba Yesu hakuumbwa bali Yeye ni Muumbaji. Yeye ni Mungu.
Paulo anaendelea na kusema, "Yeye alikuwako kabla ya vitu vyote; vyote huendelea kuwako kwa uwezo wake. Yeye ni kichwa cha mwili wake, yaani kanisa; yeye ni chanzo cha uhai wa huo mwili. Yeye ndiye mwanzo, mzaliwa wa kwanza aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, ili awe na nafasi ya kwanza katika vitu vyote" (Wakolosai 1:17-18). Paulo anaguzia sehemu nyingi ambazo Kristo ana mamlaka-juu ya viumbe, juu ya kanisa, juu ya kifo, na hatimaye "kwa kila kitu." Kristo alikuwapo kabla ya vitu vyote na Yeye ni vitu vyote ("vyote huendelea kuwako kwa uwezo wake"). Kwa hivyo Kristo ni mtawala.
Fundisho hili ni muhimu kwa mtazamo wetu wa na kumwabudu Kristo. Utawala wa Kristo unadhibitisha kuwa Yesu ni Mungu kamili. Yeye si mtu aliye juu ya wanadamu wenging bali yuu juu ya viumbe vyote, vile ni Mungu pekee anaweza kuu juu ya viumbe vyote. Ukweli huu in wa muhimu kwa wokovu wetu. Mungu hana mwisho na kwa hivyo, dhambi zetu dhidi Yake ni kosa lililo na mwisho. Ili tutakazwe na kosa hili, dhabihu lazima iwe isiyo na mwisho. Yesu kama Mungu, hana mwisho na hivyo dhabihu iwezayo kutakaza.
Yesu kuwa mkuu jumuisha sisi kusema kuwa Yeye pekee ndiye njia iendayo kwa Mungu. Yeye si mwalimu mwenye maadili mema ambaye tunaweza kuamua kumfuata; badala yake, Yeye ni Mungu na yuu mkuu wa vyote. Utawala wa Yesu pia huifanya dhahiri kuwa hatuwezi kujitakaza dhambi zetu. Kwa hakika, "Maana damu ya fahali na mbuzi haiwezi kamwe kuondoa dhambi" (Waebrania 10:4). Yesu alitimiza zote mbili na kubadilisha mfumo huo. Wokovu haupatikani kwa msisingi ya matendo (ona Waefeso 2:1-10). Na pindi tu tumeokolewa, utawala wa Yesu unatuonyesha kuwa hatuwezi tazamia kuwa kama Yeye kwa nguvu zetu wenyewe. Yesu ni msafi kabisa aliye juu ya yote. Wakristo wameitwa kumfanana Yesu, lakini hii ni kupitia kwa kazi ya Roho Mtakatifu (Wafilipi 2:12-13; Warumi 8).
Utawala wa Yesu unatufunza kuwa Yeye si kiumbe wa kiroho aliye juu ya vyote pekee. Paulo anatuambia kwamba kupitia Yeye vitu vyote vinanvyoonekana na visivyoonekana, mbinguni na duniani, kwa mfano., kiroho na kimwili, viliumbwa (ona Wakolosai 1:16). Waebrania 1:4 inamwita Yesu juu ya malaika. Ukweli huu unapinga mazoea yoyote ya kuabudu malaika. Yesu aliumba malaika na Yeye yuko juu yao. Tunaambiwa kwa uwazi kuwa Yeye ni mkuu kuwaliko. Kwa hivyo, tunastahili kumwabudu Yesu. Vile vile, kwamba Yesu aliumba vitu vya dunia inamaanisha kwamba viumbe havistahili ibada zetu. Yesu yuko juu ya ulimwengu wa mwili na kiroho, na hapo anatupa ulimwengu zote mbili huku akizalia kuwa mwenye enzi juu yao.
Wakati tunaelewa utawala wa Kristo, tutakuwa na mtizamo sahihi kumhusu. Tutaelewa zaidi kwa undani uzito wa upendo Wake; tutaweza zaidi kupokea na kuitikia upendo Wake. Wanatheolojia wanaamini kwamba kitabu cha Wakolosai kiliandikwa, kwa sehemu, kupambana na mafundisho potovu yaliyochibuka Kolosai. Ilionekana sahihi kwa Paulo kudhibitisha ukuu wa Kristo ili kuzima imani hizi potovu. Alidhibitisha utawala wa Kristo, ukuu wake, na vile anatutosha. Waebrania inaelezea uhusiano kati ya agano la Agano la Kale na agano jipya la Yesu. Agano hili linafunua mfumo wa kale kuwa kama kivuli cha itimilifu kamili katika Kristo. Utawala wa Kristo ni kiungo muhimu kwa mtizamo hakika wa Utu Wake, kazi Yake, hali yetu kama waumini na Ufalme.
English
Utawala wa Kristo ni nini na maana yake halisi ni gani?