settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inasema nini kuhusu uthibitisho wa Kikristo?

Jibu


Uthibitisho ni sakramenti au tambiko inayofanyika katika madhehebu fulani kama njia ya kuashiria kukomaa kwa kiroho. Katika baadhi ya tamaduni, kwa ujumla Katoliki na Anglikani, sakramenti ya kuthibitisha ni tambiko ambalo mtu mchanga anakuwa mwanachama rasmi wa Kanisa. Hii mara nyingine hujumuisha kutakazwa "jina la kuthibitisha," kwa kawaida jina la mtakatifu, ambayo mara nyingi hutumiwa kama jina la pili la kati. Wale ambao hufanya uthibitisho wanaamini kwamba inaashiria mwanzo wa kubatizwa katika uanachama kamili wa kanisa na kibinafsi,kukubali kukomaa kwa imani. Wakatoliki na Waanglikani wanaona uthibitisho kama moja ya sakramenti saba.

Biblia, hata hivyo, ni kimya juu ya suala la tambiko hilo. Kwa kweli, wazo kwamba mtu anaweza "kuthibitisha" kwa mwingine kuwa yeye ako katika imani imekataliwa katika Maandiko. Kila mtu lazima atambue hali ya nafsi yake mwenyewe kulingana na vigezo kadhaa. Kwanza, wokovu wetu unathibitishwa na Roho Mtakatifu ambaye anaishi ndani ya mioyo yetu. "Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu" (Warumi 8:16). Tunapokubali Kristo kama Bwana na Mwokozi, Roho Mtakatifu huchukua makaazi ndani ya mioyo yetu na anatuhakikishia kuwa yupo na kwamba sisi ni Wake, na pia hufundisha na kuelezea vitu vya kiroho kwetu (1 Wakorintho 2: 13- 14), na hivyo kuthibitisha kwamba sisi ni uumbaji mpya katika Kristo (2 Wakorintho 5:17).

Pia tunathibitishwa katika imani na ushahidi wa wokovu wetu. 1 Yohana 1: 5-10 inatuambia kwamba ushahidi wa wokovu wetu umefunuliwa katika maisha yetu: tunatembea katika Nuru, hatusemi uongo, tunakiri dhambi zetu. Yakobo 2 inaweka wazi kwamba ushahidi wa imani ni kazi tunayofanya. Hatuokolewi kwa kazi zetu, lakini kazi zetu ni ushahidi wa imani ya kuokoa ndani yetu. Yesu alisema, "Kwa matunda yao mtawajua" (Mathayo 7:20). Matunda ya kiroho yanayozalishwa ndani yetu na Roho Mtakatifu (Wagalatia 5:22) ni thibitisho kwamba anaishi ndani yetu.

Tunaambiwa "Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa "(2 Wakorintho 13: 5). Kwa kuongeza, Petro anatuambia "kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu" ili tuweze "maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo" (2 Petro 1: 10-11).

Mwisho "uthibitisho" wa wokovu wetu bila shaka, ni katika siku zijazo. Wale ambao ni Wakristo wa kweli watahifadhi mpaka mwisho, "mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye atawathibitishia hata mwisho" (1 Wakorintho 1: 7-8 NKJV). Tumetiwa muhuri na Roho Mtakatifu wa ahadi, "Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmkwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu. Ndiye aliye arubani ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake "(Waefeso 1: 13-14). Hii, basi, ni maana ya kweli ya uthibitisho-wokovu ulinunuliwa kwa damu ya Kristo ambaye ndani yake tuna imani, inashuhudiwa na kutembea kwatu pamoja Naye, na imethibitishwa kwetu na Roho Mtakatifu aliye ndani.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inasema nini kuhusu uthibitisho wa Kikristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries