settings icon
share icon
Swali

Bibilia inasema nini kuhusu uumbaji dhidi ya mageuzi yasiyoingiliwa?

Jibu


Sio kwa mjibu wa jibu hili tulete jadilio la kisayansi katika swala la uumbaji dhidi ya mageuzi yasiyoingiliwa. Jadili la kisayansi juu ya uumbaji/ au kinyume na mageuzi yasiyoingiliwa ya asili, huwa tunapendekeza majibu katika Mwanzo na taasisi za utafiti wa uumbaji. Lengo la makala haya ni kuelezea ni kwa nini, kulingana na Bibilia, mjadala wa uumbaji dhidi ya mageuzi yasiyoingiliwa bado ungalipo hii leo. Warumi 1:25 yasema, “Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.”

Neno kuu tiririko katika mjadala ni kwamba wengi wa wanasayansi wanaoamini mageuzi yasiyoingiliwa pia ni watu wasiomwamini Mungu. Kunao wengine wanaonekana kushikilia kwa kadri imani ya kiadheisti kuhusu mageuzi yasiyoingiliwa na wengine wanachukua mtazamo bainifu juu ya Mungu (Mungu alikuwepo lakini hauzishwi na ulimwengu, na kila kitu kulitokea chenyewe). Kunao wengine ambao kwa kweli wanaliangalia habari na kuafikia tamatizo kwamba mageuzi yasiyoingiliwa kwa kweli yanaifaa habari hiyo. Ingawa, hii yawakilisha asili mia fulani ya wanasayansi wanaopendekeza mageuzi yasiyoingiliwa. Wengi wa wanasayansi wanshikilia kwamba maisha yalijibuka bila muingilio wowote wa kiumbe kikiuu. Mageuzi yasiyoingiliwa kwa elezo ni la sayansi ya falsafa ya asili.

Ili uatheisti uwe kweli, lazima kuweko elezo mbadala mbali na muumbaji-jinsi ulimwengu na maisha vilikuwemo. Ingawa imani katika miigo ya mageuzi yasiyoingiliwa inaenda nyuma ya Charles Darwin, alikuwa wa kwanza kuanzisha mtindo wa mageuzi yasiyoingiliwa-chaguo la kiasili. Darwin wakati mmoja alijiuzisha na imani ya Kikristo kwa sababu ya majanga fulani ambayo yalitukia katika maisha yake, baadaye aliikataa imani ya Kikristo na kuwepo kwa Mungu. Mageuzi yasiyoingiliwa yalianzishwa na mtu asiyeamini kuwa kuna Mungu. Lengo la Darwini halikuwa la kupinga kuwepo kwa Mungu, lakini huo ndio mwisho wa nadharia ya mageuzi yasiyoingiliwa. mageuzi yasiyoingiliwa ni wezesho la imani ya kutoamini kuwa Mungu yopo (kiatheisti). mwanasayansi ya mageuzi yasiyoingiliwa hawezi kukubali kuwa lengo lao ni kupeana elezo mbadala wa asili ya maisha, na papo hapo kutoa msingi wa kiatheisti, lakini kulingana na Bibilia hiyo ndio hakika sabau ya kwamba ni kwa nini nadharia ya mageuzi yasiyoingiliwa bado ingalipo.

Bibilia inatuambia, “Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matedno yao na kuyafanya chukizo”(Zaburi 14:1; 53:1). Bibilia pia yatangaza kuwa watu hawana sababu ya kutomwamini Mungu muumba. “Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na dhuru” (Warumi 1:20). Kulingana na Bibilia, mtu yeyote anayekataa kuwa Mungu hayupo ni mpumbavu. Ni kwa nini basi, watu wengi, tukijumlisha baadhi ya Wakristo, wako tayari kuwaamini wanasayansi ya megeuzi yasiyoingiliwa na yanaegemea upande mmoja kwa fasiri ya nadharia ya kisayansi? Kulingana na Bibilia wote ni wapumbavu! Upumbavu haumanishi kukosa hekima. Wanasayansi wa mageuzi yasiyoingiliwa ni watu werefu sana kiakili. Upumbavu unaonyesha kutokuwa na uwezo wa kutumia maarifa. Methali 1:7 yatuambia, “Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.”

Wanasayansi ya mageuzi yasiyoingiliwa hufanya mzaa kwa uumbaji/ maarifa ya mpangili kuwa sio wa kisayansi na hivyo haustahili kuangaliwa kisayansi. Ili kitu kichukuliwe kuwa cha “sayansi” wanapinga kuwa, lizima kiweze kuangaliwa na kuchunguzwa; lazima kiwe cha “asili.” Uumbaji katika maelezo ni “wa ulimwengu,” Mungu na viumbe visivyo vya ulimwengu hawezi kuangaliwa (pingamizo laendelea); kwa hivyo, viumbe/ hekima haiwezi kuchukuliwa kuwa ya kisayansi. Vilevile hata mageuzi yasiyoingiliwa haiwezi angaliwa au kuthibitishwa kuwa ya kisayansi, lakini hiyo haionekani kuwa jambo kwa wanasayansi wa mageuzi yasiyoingiliwa. Kwa sababu hiyo, nadharia yoteyote imechungwa kupitia; kuwaza kabla, dhanio la kabla, na nadharia iliyokubaliwa kabla ya mageuzi yasiyoingiliwa, bila elezo mpadala kuangaliwa kwanza.

Ingawa asili ya ulimwengu na asili ya maisha haiwezi oonekana. Vyote, viumbe na mageuzi yasiyoingiliwa ni mitindo iliyo katika misingi ya imani kuambatana na asili. Vilevile haiwezi kujaribiwa kwa sababu hatuwezi kuenda nyuma mabilioni ya miaka kuitazama asili ya ulimwengu au uai ulimwenguni. Wanasayansi ya mageuzi yasiyoingiliwa wanakataa uumbaji kwa misingi kwamba hiyo itawalazimu kukataa mageuzi yasiyoingiliwa kama elezo lililoanzishwa na sayansi. mageuzi yasiyoingiliwa kwa ufupi kuambatana na asili, haingiliani na elezo la “sayansi” zaidi ya vile uumbaji unavyoingiliana. mageuzi yasiyoingiliwa waaminika kuwa elezo ambalo haliwezi jaribiwa; kwa hivyo ndio nadharia pekee ya asili ambayo inaweza chukuliwa kuwa ya “kisayansi.” Huu ni upambavu! Wanasayansi wanaokubaliana na mageuzi yasiyoingiliwa wanakataa uwezekano wa nadharia ya asili bila kuchunguza uzuri wake, kwa sababu haingiliana na mawazo yao finyu ya elezo la “sayansi.”

Kama uumbaji uu kweli, basi kunayo muumbaji ambaye twawajibika kwake. mageuzi yasiyoingiliwa ni wezesho la kiatheisti. mageuzi yasiyoingiliwa inawapa wanaoamini kuwa Mungu hayupo kama msingi wa kuelezea vile uai upo bila kuwepo na muumbaji ambaye ni Mungu. mageuzi yasiyoingiliwa yakataa haja ya Mungu kuhusika na ulimwengu. mageuzi yasiyoingiliwa ni “nadharia ya uumbaji” katika dini ya kiatheisti. Kulingana na Bibilia, chaguo liko wazi. Tunaweza amini neno la Mungu ambaye anayajua mambo yote, Mungu aliye kila mahali, ama tunaweza kuamini mawazo maovu yanayoegemea upande mmoja ya “sayansi” na ya kiupumbavu.


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Bibilia inasema nini kuhusu uumbaji dhidi ya mageuzi yasiyoingiliwa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries