settings icon
share icon
Swali

Je, ni hoja gani thabiti za kibiblia kwa uungu wa Kristo?

Jibu


Kwamba Agano Jipya limejaa kumbukumbu juu ya uungu wa Kristo ni vigumu kukataa. Kutoka Injili nne kuhusu sharia za kanisa kupitia kitabu cha Matendo na Barua za Paulo, Yesu sio tu anaonekana kama Masihi (au Kristo) lakini pia analinganishwa na Mungu Mwenyewe. Mtume Paulo anarejelea uungu wa Kristo wakati anamwita Yesu "Mungu Mkuu na Mwokozi wetu" (Tito 2:13) na hata anasema kwamba Yesu alikuwepo katika "mfano wa Mungu" kabla ya kuwa na umbo la mwanadamu (Wafilipi 2:5-8). Mungu Baba anasema juu ya Yesu, "Kiti chako cha enzi, Ee Mungu, ni cha milele na milele" (Waebrania 1: 8). Yesu anaitwa moja kwa moja kama Muumba Mwenyewe (Yohana 1:3; Wakolosai 1:16-17). Vifungu vingine vya kibiblia vinafundisha uungu wa Kristo (Ufunuo 1:7, 2: 8, 1 Wakorintho 10:4, 1 Petro 5:4).

Wakati dondoo hizi za moja kwa moja zinatosha kuthibitisha kwamba Biblia inadai kuwa Yesu ni Mungu, mbinu isio ya moja kwa moja inaweza kuthibitisha kuwa na nguvu zaidi. Yesu mara kwa mara alijiweka katika nafasi ya Bwana kwa kuchukua ridhaa ya Mungu ya Baba. Alikuwa akifanya mara nyingi na kusema mambo ambayo Mungu peke yake ana haki ya kufanya na kusema. Yesu pia alijirejelea Mwenyewe kwa njia ambazo zilizodokeza uungu Wake. Baadhi ya matukio haya hutupa ushahidi thabiti wa ufahamu binafsi wa Uungu wa Yesu.

Katika Marko 14, Yesu anasimama mshtakiwa katika majaribio Yake mbele ya Kuhani Mkuu. "Kuhani Mkuu akamwuliza tena, akamwambia, wewe ndiwe Kristo, Mwana wake Mtukufu? Yesu akasema, Mimi ndiye, nanyi mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija na mawingu ya mbinguni" (Marko 14:61-62). Hapa, Yesu anarejelea Agano la Kale kitabu cha Danieli ambapo nabii Danieli anasema, "Niliona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa"(Danieli 7:13-14).

Katika kumbukumbu hii ya maono ya Danieli, Yesu anajitambulisha Mwenyewe kama Mwana wa Adamu, mtu aliyepewa "mamlaka, utukufu, na ufalme, ili watu wote, mataifa, na watu wa lugha zote wamtumikie Yeye." Mwana wa Adamu ana mamlaka ambayo ni ya milele na haitapita. Mara moja mtu hujiuliza ni mtu wa aina gani ana mamlaka ambayo ni ya milele. Ni mtu wa aina gani anapewa ufalme na watu wote kumtumikia Yeye? Kuhani Mkuu, ambaye mara moja alitambua madai ya Yesu kwa uungu, akararua joho lake na kumtangaza Yesu kuwa na hatia ya kumtukana Mungu.

Matumizi ya Yesu ya jina "Mwana wa Adamu" ina thamani thabiti ya kuomba radhi kwa kushangaza. Mwenye kushuku uungu wa Kristo hawezi kataa kwa urahisi uteuzi huu maalumu wa Yesu. Kwamba Kristo alijirejelea Mwenyewe kwa namna hii anafurahia uthibitisho mwingi, kama inavyopatikana katika vyanzo vyote vya injili. Maneno "Mwana wa Adamu" hutumiwa kwa Yesu mara chache tu nje ya Injili yenyewe (Matendo 7:56, Ufunuo 1:13; 14:14). Kutokana na matumizi yake machache na kanisa la kwanza la mitume, haiwezekani kwamba cheo hiki kilisomwa tena kwenye midomo ya Yesu ikiwa, kwa kweli, hakuwa ametumia uteuzi huu maalumu. Na hata hivyo, ikiwa imethibitishwa kuwa Yesu alitumia jina hili kwake Mwenyewe, inakuwa wazi kwamba Yesu alijiona kuwa na nguvu za milele na mamlaka ya pekee zaidi ya ile ya mwanadamu.

Wakati mwingine, ilikuwa ni matendo ya Yesu ambayo yalifunua utambulisho wake. Uponyaji wa mtu aliyepooza na Yesu katika Marko 2 ilifanyika kuonyesha mamlaka Yake na uwezo Wake wa kusamehe dhambi (Marko 2:3-12). Katika mawazo ya wasikilizaji wake wa Kiyahudi, uwezo huo ulihifadhiwa kwa Mungu pekee. Yesu pia anapataka kusujudiwa mara kadhaa katika Injili (Mathayo 2:11; 28:9, 17; Luka 24:52; Yohana 9:38; 20:28). Kamwe Yesu hakukataa ibada hiyo ya kuabudu. Badala yake, aliona ibada yao kama iliyowekwa vyema. Kwingineko, Yesu alifundisha kwamba Mwana wa Adamu hatimaye atahukumu ubinadamu (Mathayo 25:31-46) na kufundisha kwamba matarajio yetu ya milele yanategemea majibu yetu kwake (Marko 8:34-38). Tabia hiyo ni dalili zaidi ya uelewa binafsi wa Yesu wa kiungu.

Yesu pia alisema kuwa ufufuo wake ujao kutoka kwa wafu unathibitisha madai ya kipekee ambayo alijifanyia Mwenyewe (Mathayo 12:38-40). Baada ya kusulubiwa na kuzikwa katika kaburi la Yosefu wa Arimathea, Yesu alifanya, kwa kweli, kufufuka kutoka kwa wafu, kuthibitisha madai yake kwa uungu.

Ushahidi kwa tukio hili la miujiza ni wa nguvu sana. Vyanzo vingi vya kisasa vinasema maonyesho ya Yesu baada ya kusulubiwa kwa watu binafsi na vikundi chini ya hali mbalimbali (1 Wakorintho 15:3-7, Mathayo 28:9, Luka 24:36-43; Yohana 20:26-30, 21:1- 14; Matendo 1:3-6). Wengi wa mashahidi hawa walikuwa tayari kufa kwa imani hii, na wengi wao walifanya! Clement wa Roma na mwanahistoria wa Kiyahudi Josephus anatupa taarifa za karne ya kwanza za ushahidi wa mateso yao kadhaa. Nadharia zote zilizotumiwa kuelezea mbali ushahidi wa ufufuo (kama vile Nadharia ya Njozi) haukufaulu kueleza habari zote zinazojulikana. Ufufuo wa Yesu ni ukweli ulio imara wa historia, na huu ndio ushahidi thabiti kwa uungu wa Yesu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni hoja gani thabiti za kibiblia kwa uungu wa Kristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries