settings icon
share icon
Swali

Je, wanawake wakristo wanapaswa kuvaa vipodozi au mapambo ya vito?

Jibu


1Samweli 16: 7b inatangaza, "Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; bali Bwana huutazama moyo. " 1 Timothy 2: 9-10 inatuambia,"Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; bali kwa matendo mema,kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu. " Paulo hakuwakataza wanawake kutovaa mapambo ya vito, vipodozi, au kusuka nywele - badala yake anawaambia wanawake wasiruhusu mtazamo wao wa nje uonekane kuwa wa muhimu zaidi kuliko urembo wao wa ndani.

Petero anatukumbusha kuhusu ukweli huu wa kiroho: "Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; Bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho wa upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu . Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao."(1 Petro 3: 3-5).Hakuna ubaya kwa kuvaa mapambo ya vito, vipodozi, au kusuka nywele bora tu iwe imefanywa kwa njia ya kisasa. Mwanamke hapaswi kulenga hasa kwa mtazamo wake wa nje hadi kwamba hajali maisha yake ya ndani ya kiroho. Biblia inalenga katika moyo. Kama mwanamke anatumia muda mwingi na fedha kwa vile anaonekana, tatizo ni kwamba vipaumbele vyake ni vibaya.Mapambo ya vito ya dhamani kubwa na mavazi ndio matokeo ya tatizo, wala sio tatizo lenyewe.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, wanawake wakristo wanapaswa kuvaa vipodozi au mapambo ya vito?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries