Swali
Je! Tunahitaji kufahamu vita vya kiroho ambavyo hufanyika karibu nasi?
Jibu
Ni muhimu kwamba kila Mkristo aelewa kwamba yeye ako katika vita vya kiroho. Hakuna njia ya kuepukana nayo. Ufahamu wa vita vya kiroho karibu nasi ni muhimu sana. Sio tu uelewa, lakini uangalifu, utayarishi, ujasiri, na silaha sahihi ni mambo muhimu ya kushiriki katika mapambano ya kiroho.
Katika maneno ya Paulo katika 2 Wakorintho 10:3-5, "Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha nome; tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo." Ni wazi kwamba "vita vyetu" kama Wakristo ni kiroho. Hatupigani vita vya kimwili au vita vya kibinadamu. Ni juu ya ngazi ya kiroho-maadui zake, haki zake, ngome zake, na silaha zake zote ni za kiroho. Ikiwa tutajaribu kupigana na kiroho na silaha za kibinadamu, tutashindwa na adui atashinda.
Ni muhimu kutambua kwamba Paulo hazungumzi juu ya kupigana na mapepo hapa. Wakati Yesu na mitume walipotoa pepo nje, ilikuwa, pamoja na ishara na maajabu mengine waliyoonyesha, hasa kuthibitisha mamlaka ya yale waliyosema. Ilikuwa muhimu wakati huo kwa Mungu kuwapa mitume "uthibitisho" wenye nguvu kwamba walikuwa kweli kutoka kwa Mungu na walikuwa wasemaji Wake. Uaminifu wa Maandiko hutegemea mamlaka ya mitume, hivyo Mungu aliwapa mitume uwezo Wake wa kuthibitisha mafundisho yao. Hoja nzima ilikuwa ni kuonyesha kwamba mamlaka ya mwisho-na silaha yetu ya kiroho ya mwisho-ni Maandiko. Aina ya vita vya kiroho ambazo kila Mkristo huingilia ni hasa vita vya akili na moyo.
Vita vya kiroho ni binafsi hasa kwa kila Mkristo. Ibilisi ni kama "simba angurumaye" akitafuta kumeza, na lazima tuwe macho juu yake (1 Petro 5:8). Adui wa roho zetu ana "mishale ya moto" ambayo inaweza tu kuzimwa na ngao ya imani kama kushughulikiwa na muumini aliyetayarishwa na silaha kamili za Mungu (ona Waefeso 6:10-17). Yesu alituambia "tukeshe na kuomba" ili tusiingie katika majaribu (Marko 14:38).
Kulingana na 2 Wakorintho 10:4-5, kuna ngome za kiroho katika ulimwengu huu, zilizotengenezwa kwa "kisio" na "mambo ya juu." Neno kisio ni, katika Kigiriki, logismos. Inamaanisha "mawazo, dhana, mafikirio, falsafa." Watu wa ulimwengu hujenga logismos hizi kujikinga wenyewe dhidi ya ukweli wa Mungu. Kwa kusikitisha, ngome hizi mara nyingi hukuwa magereza na hatimaye makaburi. Kama Wakristo, tuna wito wa kuvunja ngome hizi na kuwaokoa wakaaji. Ni hatari na kazi ngumu, lakini tuna silaha ya Mungu daima katika udhibiti wetu. Kwa bahati mbaya, moja ya mbinu bora ya adui ni kutusababisha sisi kupambana na silaha za binadamu badala ya Mungu.
Wakati unapigana na falsafa za kidunia, akili na silaha za kibinadamu hazisaidii. Mbinu za elimu ya soko, kupinga falsafa, maneno ya ushawishi ya hekima ya binadamu (1 Wakorintho 2:4), falsafa mantiki, shirika, ujuzi, burudani, fumbo, taa bora, muziki bora — haya yote ni silaha za kibinadamu. Hakuna hata moja ya mambo haya yatashinda vita vya kiroho. Kitu pekee ambacho kinafaa-silaha tu yenye kinga tunamiliki-ni Upanga wa Roho, ambayo ni Neno la Mungu (Waefeso 6:17). Upanga huu hutupa uhuru mwingi kama askari katika vita hivi vya kiroho. Tuna uhuru kutokana na hofu, tukijua kwamba Mungu anatupigania (Yoshua 1:7-9) na kwamba hatatuacha. Tuna uhuru kutokana na hatia, tukijua kwamba sisi hatuajibikii roho za wale wanaokataa ujumbe wa Mungu baada ya kuutangaza kwao (Marko 6:11). Tuna uhuru kutoka kukata tamaa, tukijua kwamba, ikiwa tunateswa na kuchukiwa, Kristo aliteswa na kuchukiwa kwanza (Yohana 15:18) na kwamba majeraha yetu ya vita yatatuzwa kwa utajiri na upendo mbinguni (Mathayo 5:10).
Uhuru huu wote hutoka kwa kutumia silaha yenye nguvu ya Mungu-Neno Lake. Ikiwa tutatumia silaha za kibinadamu kupambana na majaribu ya yule mwovu, tutapatwa kushindwa na masikitiko. Kinyume chake, ushindi wa Mungu umejaa tumaini. "Na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi. Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu"(Waebrania 10:22-23). Mioyo ya wale wanaoisikia na kukubali ukweli, ujumbe kamili wa injili vile humetolewa na mitume ni "wanyunyiziwa safi" na "kuoshwa kwa maji safi." Je! Maji haya ni nini? Ni Neno la Mungu linatuimarisha tunapopigana (Waefeso 5:26; Yohana 7:38).
English
Je! Tunahitaji kufahamu vita vya kiroho ambavyo hufanyika karibu nasi?