settings icon
share icon
Swali

Ni nini maana ya ufunuo wa jumla na ufunuo maalum?

Jibu


Ufunuo wa jumla na ufunuo maalum ndio njia mbili pekee Mungu amechagua mwenyewe kwa ili ajidhihirishe kwa mwanadamu. Ufunuo wa jumla unahusu ukweli kwa ujumla ambao unaweza kujulikana juu ya Mungu kwa njia ya asili. Ufunuo maalum unahusu ukweli maalum zaidi ambao unaweza kujulikana juu ya Mungu kwa njia isiyo ya kawaida.

Kulingana na suala la ufunuo wa jumla, Zaburi 19:1-4 inasema, "Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, na anga laitangaza kazi ya mikono yake. Machana husemezana na mchan, usiku hutolea usiku maarifa. Hakun lugha wal maneno, sauti yao haisikilikani. Sauti yao imeenea duniani mwote, na meneno yao hata miisho ya ulimwengu. Katika hizo ameliwekea jua hema." Kwa mujibu wa kifungu hiki, kuwepo na Nguvu za Mungu zinaweza kuonekana wazi kupitia kuchunguza ulimwengu. Kwa umaarufu, na uajabu wa uumbaji husungumzia kuwepo kwa Muumbaji aliye na nguvu na utukufu.

Ufunuo wa jumla pia unafundishwa katika Warumi 1:20, "Kwa sababu mambo yake yasioyoonekan tangu kuumbwa ulimwngu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa mille na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru." Kama Zaburi 19, Warumi 1:20 inatufundisha kwamba uwezo wa milele wa Mungu na asili ya Mungu ni "kuonekana wazi " na "kueleweka" kutokana na kile kimepatikana, na kwamba hakuna sababu ya kukataa ukweli huu. Kwa maandiko haya katika akili, labda kufanya kazi kwa ufafanuzi wa jumla ufunuo utakuwa "ufunuo wa Mungu kwa watu wote, wakati wote, na katika maeneo yote yale ambayo yanathibitisha kuwa Mungu yupo na kwamba yeye yu na akili, nguvu, na anapita uwezo wa bidnadamu."

Ufunuo maalum ni jinsi Mungu amechagua kujidhihirisha mwenyewe kwa njia ya miujiza. Ufunuo maalum ni pamoja na kuonekana kimwili kwa Mungu, ndoto, maono, neno la Mungu lililoandikwa, na muhimu zaidi, Yesu Kristo. Biblia imerekodi Mungu akionekana katika hali ya kimwili mara nyingi (Mwanzo 3:8, 18:1; Kutoka 3:1-4, 34:5-7), na Biblia imerekodi Mungu akizungumza na watu kwa njia ya ndoto (Mwanzo 28:12, 37:5; 1 Wafalme 3:5; Danieli 2) na maono (Mwanzo 15:1; Ezekieli 8:3-4; Danieli 7, 2 Wakorintho 12:1-7).

Cha msingi muhimu katika kudhihirisha kwa Mungu ni neno lake, Biblia, ambayo pia ni aina ya ufunuo maalum. Mungu kimiujiza aliwaongoza waandishi wa maandiko kwa usahihi kurekodi ujumbe wake kwa mwanadamu, huku bado akitumia mitindo yao wenyewe na haiba. Neno la Mungu li hai (Waebrania 4:12). Neno la Mungu lina pumzi,la faida, na latosha (2 Timotheo 3:16-17). Mungu aliamua kuwa na ukweli kumhusu Yeye kama kumbukumbu kwa maandishi kwa sababu alijua ukasoro na ukosefu wa uhakika wa masimulizi ya jadi. Yeye pia huelewa kwamba ndoto na maono ya mwanadamu inaweza tafsiriwa vibaya. Mungu aliamua kufunua kila kitu ambacho binadamu anahitaji ya kujua juu yake, kile anachotarajia, na chenye ametufanya sisi katika Biblia.

Aina ya mwisho ya ufunuo maalum ni utu wa Yesu Kristo. Mungu akawa binadamu (Yohana 1:1, 14). Waebrania 1:1-3 inatupa muhtasari ulio bora, "Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote...... Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake." Mungu akawa binadamu, katika utu wa Yesu Kristo, ili ajitambulishe na sisi, kwa mfano kwa ajili yetu, kutufundisha, kujifunua mwenyewe kwetu, na muhimu zaidi, kwa kutoa wokovu kwa ajili yetu kwa kunyenyekea mwenyewe katika mauti ya msalaba (Wafilipi 2:6-8). Yesu Kristo ndiye mwisho wa "ufunuo maalum" kutoka kwa Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nini maana ya ufunuo wa jumla na ufunuo maalum?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries